Simba hatarini kupokonywa kombe; TFF kufungiwa na FIFA kwa sababu ya Yanga

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,476
17,674
Jambo wakuu!

Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha. Naomba niwatonye jambo moja la hatari linaloinyemelea soka ya Tanzania endapo TFF hawatachukua hatua zinazofaa kuepushia mbali hatari hii.

Mechi iliyopita kati ya Simba na Yanga ilishindikana kuchezeka baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kugoma kupeleka timu kiwanjani kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni zinazoendesha ligi kuu (VPL). Huenda kweli madai yao yalikuwa na mashiko ndio maana hadi leo hawajachukuliwa hatua zozote za kinidhamu kama ilivyo kawaida. Na kwa bahati mbaya, hadi leo hakuna mtu yeyote (sio serikali, TFF, bodi ya ligi au wizara ya michezo) aliyetoa sababu za msingi za kuahirishwa kwa mechi ile, licha ya kwamba Yanga wanainyooshea kidole TFF kwa kuvuruga muda wa mchezo bila sababu zinazoeleweka.

Mimi sio mtu wa mpira kiviiiiile lakini nadhani Yanga wapo sahihi kwa asilimia 90% kwa kuwa TFF wameshindwa kuwaadhibu kwa kugomea mchezo au kutoa maelezo kuhusu kadhia nzima. Nina wasiwasi mchawi ama yupo ndani ya TFF au bodi ya ligi. Ndio maana wanashindwa kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe ili kuepuka aibu. Pia wanakwepa kudaiwa fidia na timu za Yanga na Simba kwani awali timu hizi zililalamika kutumia gharama kubwa za maandalizi ya mchezo husika na hivyo kutaka aliyeharibu mchezo kuwalipa fidia.

Jambo jingine linalowaumiza vichwa TFF ni kuhusu mamilioni ya fedha za mashabiki walizokusanya kama viingilio. Je, fedha hizi zinarejeshwaje kwa wahusika na watawatambuaje? Tukumbuke kuwa tiketi za mashabiki zilichanwa kabla ya kuingia kiwanjani.

Utamu wa utata huu unaanzia hapa. Sikiliza kwa makini. Kwa muijbu wa sheria na kanuni za TFF, ili timu itangazwe kuwa bingwa wa ligi ni lazima iwe imecheza jumla ya mechi 34 kwa msimu huu wa ligi (2020/2021). Hii ni kwa sababu kuna jumla ya timu 18 katika ligi, ambapo kila timu ikicheza dhidi ya timu zote (home and away) inapaswa kukamilisha jumla ya mechi au michezo 34.

Lakini mwelekeo unaonyesha Yanga hawapo tayari tena kupeleka timu kucheza dhidi ya Simba. Viongozi wao wameishasema tena na tena kwamba wao wameishacheza huo mchezo na hawako tayari kupeleka timu kiwanjani kwa namna yoyote ile. Kwa maana hiyo, ikiwa Yanga wataendelea na msimamo huu maana yake ni kuwa, mpaka msimu unamalizika Simba watakuwa wamecheza jumla ya michezo 33, hivyo kukosa uhalali wa kisheria kukabidhiwa kombe la ushindi. Na kwa kuwa dalili zote zinaonyesha kuwa hata Simba wakicheza michezo 33 wana uwezo wa kuchukua kombe, Yanga wamewatega TFF walikoroge walinywe. Wanawasubiri wausage mtama wabugie wenyewe!

Movie nzima iko hivi: endapo TFF wataogopa kuwakabidhi Simba kombe lao kwa kuogopa kuadhibiwa na Yanga, basi serikali itaingilia kati ili Simba wakabidhiwe kombe kwa nguvu na kinyume cha sheria za FIFA. Ifahamike kwamba sheria za FIFA zinakataza serikali kuingilia mambo ya michezo na adhabu ya papo kwa papo itakayotolewa ni kuifungiwa kwa TFF, hivyo kupelekea ligi yetu kufutwa na timu zetu kutoshiriki mechi za kimataifa. Aidha, Yanga nao watakimbilia mahakamani kuwashitaki TFF kwa kuwakabidhi Simba kombe kinyume cha sheria. Hapa sasa movie itakuwa imefikia patamu sana. Matokeo yake TFF watapigwa rungu ya pili na FIFA kwa kusababisha masuala ya soka kupelekwa mahakamani. Yanga wanafanya hivi kwa makusudi ya kuwakomoa Simba (watani wa jadi) ama kwa kujua au kutokujua madhara yake ya ujumla kwa mpira wa Tanzania.

The ultimate END of this fantastic movie is that TFF will be banned forthwith by FIFA and Simba will not be crowned the championship of VPL this season. Kwa hiyo sasa nchi itaingizwa kwenye migogoro ya FIFA moja kwa moja na ligi ya VPL itasahaulika duniani. Wapenzi wa mpira katika nchi hii wajiandae kisaikolojia kutazama mashindano ya ndondo. Hakutakuwa na mashindano ya VPL msimu ujao.

Nawasilisha.​
 
Nendeni tu fifa baada ya kushushwa daraja ili mje huku mtunishiane misuli vizuri na serikali maana watasema walisogeza mbele masaa mawili kutokan an asababu za kiusalama ila kiukweli bora msilete hiyo team maana mmeandaliwa kipondo cha kufa mtu na kombe la FA wiki hii bora tu mfungwe na biashara sababu fainali mtapigwa nyingi sana na simba na hiyo ni kama hamtakimbia
 
huwezi amini haya majamaaa ndiyo yanalilia kwenda kuwakilisha nchi ,last time walipata kundi kama hili..FOR GOD SAKE kundi kama hili tena shirikisho unafanya makorokocho? ndiyo maana tulivyopangwa safari hii na kina as vita kila dakika kututishia maana majitu haya hayajitambui kabisa
Screenshot_2021-06-21 Shaffih Dauda - USM Alger na Rayon Sports zimefuzu robo fainali ya kombe...png
 
Naomba nisaidie kujua kanuni zinasemaje kuhusu athari za tukopeleka timu uwanjani?
Nani anapata athari chanya na nani anapata athari hasi kati ya aliyepeleka timu na asiyepeleka timu?
Nawasilisha
Kanuni zinasema klabu isipopoleka timu kiwanjani inaadhibiwa lakini mpaka sasa Yanga hawajaadhibiwa whichi means walikuwa sahihi kutopeleka timu kiwanjani. Kwa mantiki hii, wao wanachukulia kwamba tayari wameishacheza huu mchezo kwa kuwa hawajapewa adhabu yoyote. Na hata wasipopeleka timu kiwanjani tarehe 3/7 hakutakuwa na shida yoyote kwa upande wao kwa kuwa TFF walivunja kanuni wao wenyewe.

Watakaopata athari chanya ni Yanga kwani wachezaji wao hawatapata usumbufu wa kuingia kiwanjani kucheza mpira.

Watakaopata athari hasi ni Simba kwa kunyimwa kombe kwa sababu ya kutocheza michezo yote 38 kwa mujibu wa sheria. Wengine ni washabiki waliolipa viingilio vyao lakini hawakutazama mchezo. Aidha TFF nao wataathirika kwa kufungiwa na FIFA. Pia mashabiki wa nchi hii watakosa kutazma uhondo wa VPL msimu ujao.
 
Naomba nisaidie kujua kanuni zinasemaje kuhusu athari za tukopeleka timu uwanjani?
Nani anapata athari chanya na nani anapata athari hasi kati ya aliyepeleka timu na asiyepeleka timu?
Nawasilisha
Kwanza kabisa kanuni inasema muda wa kubadilisha muda wa kuanza.mchezo atleast ile masaa 24, na body ya ligi ilibadilisha muda kutoka saa 11 jioni mpaka saa moja nje ya wakati yaani saa nane mchana ndiyo wakabadilisha mechi, inamaana masaa 3 tu na kanuni inasema.kiwangu kifupi ni masaa 24.

Yanga wakiingiza timu saa kumi na moja kasoro na wakaa uwanjani kwa mpaka saa kumi na moja na nusu, wakaondoa timu, inamaana mshindani wake ambae ni Simba hakuingia uwanjani, hapo adhabu yake ni Yanga kupewa point 3 na magori 3 na Simba inaweza kushushwa daraja.

Kama Yanga haitapeleka timu uwanjani tarehe 3 TFF haiwezi kuichukulia hatua yoyote Yanga, kama itachukuliwa hatua Yanga ikienda FIFA watataka kujua sababu, na kama wataeleza iluvyokuwa TFF itapigwa ban kwa serikali kuingilia mambo ya mpira, maana body ya ligi walisema qakipokea simu kutoka kwa waziri wa michezi mchezoi usogezwe mbele ili rais aje uwanjani kama.mgeni rasmi.
 
Kwanza kabisa kanuni inasema muda wa kubadilisha muda wa kuanza.mchezo atleast ile masaa 24, na body ya ligi ilibadilisha muda kutoka saa 11 jioni mpaka saa moja nje ya wakati yaani saa nane mchana ndiyo wakabadilisha mechi, inamaana masaa 3 tu na kanuni inasema.kiwangu kifupi ni masaa 24...
Hapo nimekuelewa vizuri sana mkuu. Lakini Simba walishindwa kupeleka timu baada ya Yanga kuondoka kiwanjani. Wangepeleka timu icheze na nani wakati Yanga wameishasepa kitambo? Na pia hapakuwepo na marefa wa kuchezesha mchezo.
 
Kanuni zinasema klabu isipopoleka timu kiwanjani inaadhibiwa lakini mpaka sasa Yanga hawajaadhibiwa whichi means walikuwa sahihi kutopeleka timu kiwanjani. Kwa mantiki hii, wao wanachukulia kwamba tayari wameishacheza huu mchezo kwa kuwa hawajapewa adhabu yoyote...
Asante.

Naomba pia ufafanuzi hapo kwenye kucheza mechi 38. Kwa Mfano timu ikacheza mechi 37, alafu mechi moja mpinzani wake akashindwa kutokea uwanjani.

Una maana kuwa hiyo timu iliyocheza michezo 37 na ikawa na points nyingi kuliko timu zote haitakua bingwa kwa kushindwa kucheza mechi 38 ? Hivi ndivyo ulivyotafsiri kanuni hiyo?
 
Uongozi wa Yanga wameishakataa kata kata ( kupitia kwa msemaji wao) kupeleka timu kiwanjani. Wewe unaishi duniani gani mkuu?
Uongozi wa yanga kwa maana ya Mzee mpili?

Kama ni huyo mbona alipingwa na walidai kua kwenye uongozi wa club ya yanga katiba haitambui hao wazee

Yanga kabakiza mechi tatu, huku simba akiwa na mechi 6 mkononi. Kinachomuuma yanga zaidi ni kuona kasi ya simba na u serious wake kwenye viporo vyake, kua simba anahitaji ushindi wa mechi mbili na sare moja ili atangazwe official bingwa.

Yanga wamesha give up kimsingi wamekata ringi wanatafuta pakupapasa hawapaoni they got no one to blame so they blame Karia and TFF.

Jana wameshinda, kelele zinazotamba mtaani mpaka sasa ni kua wao ni magwiji, wamefanya comeback ya kibabe ndani ya dakika moja wame penetrate bao mbili. Lakini matokeo yangekuja tofauti na hapo lawama zingeenda kwa karia na TFF.

Mwakalebela aliyekua akilalamika daily kua TFF inaipendelea simba na kua kifungo chake kinejaa uonevu na hujuma ame comfess na kukiri kua alikua anakosea bali tatizo ni yeye na yanga ambao hawakua wakijua namna sheria zinavyo operate ila baada ya kupewa mchanganuo aka admit kua adhabu aliyopewa ni halali na alistahili ku adhibiwa

Hao ndio yanga na ndio maana metacha aliwapa salute ya kidole kimoja
 
Asante.
Naomba pia ufafanuzi hapo kwenye kucheza mechi 38. Kwa Mfano timu ikacheza mechi 37, alafu mechi moja mpinzani wake akashindwa kutokea uwanjani. Una maana kuwa hiyo timu iliyocheza michezo 37 na ikawa na points nyingi kuliko timu zote haitakua bingwa kwa kushindwa kucheza mechi 38 ? Hivi ndivyo ulivyotafsiri kanuni hiyo?
Ndio maana yake mkuu. Ili ushindi uwe VALID lazima mshindi acheze mechi zote; vinginevyo huo ushindi utakuwa BATILI. Kama TFF watarogwa wakatoa kombe kwa Simba (hata kama watakuwa na pointi nyingi), Yanga watawashikisha adabu ambayo hawatakuja kuisahau hapa duniani.
 
Mfano timu ikakusanya points ambazo hazitafikia na timu nyingine yoyote kabla ya kumaliza michezo 34 ndiyo kusema hiyo timu haitakabidhiwa kombe kusubiri kumaliza michezo 34?
Exactly!
 
Kanuni zinasema klabu isipopoleka timu kiwanjani inaadhibiwa lakini mpaka sasa Yanga hawajaadhibiwa whichi means walikuwa sahihi kutopeleka timu kiwanjani. Kwa mantiki hii, wao wanachukulia kwamba tayari wameishacheza huu mchezo kwa kuwa hawajapewa adhabu yoyote...
Duh! Hivi Haji Mfikilwa ni nani pale yanga na alisemaje kuhusu hiyo machi ya tarehe 3?

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom