Simba avamia Kijiji cha Sitalike Tarafa ya Nsimbo Wilayani Mlele Katavi na kuua wawili

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,800
34,189
Mnyama Simba amevamia Kijiji cha Sitalike Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi na kuuwa watu wawili.

Waliouawa ni baba na mtoto wake ambapo simba huyo kula mtoto na kuacha kichwa huku akinyonya damu ya mzazi hadi kupoteza maisha.

Tukio la Simba huyo kuua watu wawili limetokea jana majira ya saa kumi na moja alfajiri katika Kijiji hicho cha Sitalike .

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher Anjelo aliwaambia waandishi wa habari waliouawa kuwa ni John Jeremia (45) na mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka mitano .

Alisema siku ya tukio wanafamilia hao walikuwa wamelala ndani ya nyumba yao ndipo simba huyo jike alipovamia na kuingia ndani ya nyumba hiyo .

Alieleza baada ya Simba huyo kuingia ndani alimvamia baba wa mtoto huyo na kuanza kumnyonya damu hadi alipohakikisha amefariki dunia ndipo alipomwachia marehemu huyo.

Mwenyekiti huyo wa Kijiji alisema simba huyo baada ya kuona John Jeremia amemnyonya damu hadi kufa alihamia kwa mtoto wake na marehemu na kuanza kumshambulia na kisha alianza kumtafuna na kubakiza kichwa tuna kwenda nacho hadi kwenye kichaka kilichokuwa jirani na nyumba ya marehemu hao.

Alisema taarifa za simba kuua watu hao zilifika kwenye uongozi wa Kijiji hicho ambao nao walitoa taarifa kwa askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambapo walianza kufanya msako wa kumsaka simba huyo kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Sitalike.

Wakati wakifanya msako waliona nyayo za simba na walizifuata kule zilipoelekea na walipofika kwenye kichaka walimuona simba huyo akiwa amekaa na pembeni yake kukiwa na kichwa cha mtoto .

Mwenyekiti wa Kijiji alisema askari wa Hifadhi ya Katavi walimfyatulia simba huyo risasi lakini aliweza kuikwepa na kusogea mbele zaidi .

Hata hivyo waliendelea kumfuata kwa kushirikiana na wananchi ndipo Askari wa TANAPA walipofanikiwa kupiga risasi na kufa hapo hapo.

Alieleza baada ya Simba huyo kuwa ameuawa kwa kupigwa risasi baadhi ya wananchi waliomba wamchukue kama kitoweo cha mboga lakini askari wa TANAPA waliwakatalia na walimchukua simba huyo aliyekuwa amekufa na kwenda nae kwenye hifadhi yao kwa kile walichoeleza kuwa wanakwenda kumchoma moto kwa kutumia mafuta ya petroli.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kuuawa kwa watu hao na Simba huyo aliyetokea kwenye Hifadhi ya mbuga ya Katavi .

Alisema ameisha peleka askari wake kwenda kuangalia eneo la tukio hilo na ametoa wito kwa wananchi kuacha kujenga makazi karibu na hifadhi ya Katavi.

mkono.jpg


simba.jpg
 
Last edited by a moderator:
Tukio kama hili liikumbushe serikali ipunguze vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze kujenga nyumba imara
 
Yaani simba amekula mtu muda usio mrefu then watu wanataka kula nyama yake
 
Masahihisho Nsimbo sio Tarafa kwasasa bali ni Wilaya/Halmashauri kamili ya Nsimbo.
 
Mi huwa sielewi pale starike wanaishije maana makazi yapo kalibu na mbuga je wale viboko siku wakicharuka wavamie vijiji itakuweje sijui mi huwa najiuliza sijui waliplan vipi yale makazi afu kitu kingine serikali ijalibu kupunguza vifaa vya ujezi sehemu kama zile maana watu wengi kule wanajenga nyumba za miti afu mlangoni mtu anaweka sarufeti ambayo ni hatari sana.
 
Mi huwa sielewi pale starike wanaishije maana makazi yapo kalibu na mbuga je wale viboko siku wakicharuka wavamie vijiji itakuweje sijui mi huwa najiuliza sijui waliplan vipi yale makazi afu kitu kingine serikali ijalibu kupunguza vifaa vya ujezi sehemu kama zile maana watu wengi kule wanajenga nyumba za miti afu mlangoni mtu anaweka sarufeti ambayo ni hatari sana.
Mkuu unashangaa ya Sitalike!!!nenda Kanoge ndio ushangae zaidi.
 
Back
Top Bottom