Simba 1-0 Azam FC | Simba yatwaa ubingwa kombe la Mapinduzi

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
4,319
2,000
Michuano ya Mapinduzi Cup 2022 inafikia tamati leo kwa mechi ya fainali kupigwa, AzamFC dhidi ya Simba SC. Katika fainali za mwaka 2017 na 2019 timu hizi zilikutana na zote AzamFC kaibuka bingwa. Je, AzamFC kutwaa taji hili kwa mara ya tatu mbele ya Simba SC ama Simba SC kulipa kisasi?

Tunakuletea LIVE mech hi kuanzia
saa 2:15 usiku.

Leo pia

Kutakuwa na VITA YA UFUNGAJI BORA: Hawa ndiyo vinara wa mabao kwenye Mapinduzi Cup 2022 , kila mmoja akiwa ametupia mabao mawili. Sasa leo kutakuwa na vita kati ya Iris Ilunga Mbombo wa Azam dhidi ya Pape Ousmane Sakho, wote wana mabao mawili kila mmoja...Je, unampa nani nafasi ya kuibuka mfungaji bora mwaka huu? Wengine walioaga mashindano wakiwa wamefunga magoli mawili kila mmoja ni:

Hussein Mwinyi - Meli 4 City.
Heritier Makambo - Yanga.
Abrahman Othman - KMKM SC

Tukutane saa 2:15 kwenye fainali LIVE


==========

2:16 Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi anakagua na kusalimia vikosi vya timu zote mbili

2:19 Rais Mwinyi anamaliza kupiga picha na timu zote

==

00' Kabumbu linaanza uwanja wa Aman

01' Bwalya anapiga free kick inayopaa juu ya lango baada ya Shomari kuangashwa

15' Almanusura Ajibu aandike Azam bao la kwanza kwa kutandika shuti kali kutoka nje ya 18, Manula anapangua

30' Kola anaachia mkwaju unaogonga besela, Simba 0-0 Azam

31' Sakho anaachia mkwaju unaopaa juu kidogo ya lango la Azam

32' Mlinda mlango wa Azam, Mathias Kigoya yuko chini baada ya kugongana na mlinzi wake katika purukushani za kuokoa

36' Kigonya anapangua mkwaju matata wa Kibu Denis

45+1' Simba wanapiga kona, inashindwa kuleta matokeo

45+2' Mpira mapumziko

55' ⚽ Simba wanaandika goli la kwanza kupitia mkwaju wa Penalt, Meddie Kagere

90+4' Mpira umekwisha, Simba mabingwa kombe la mapinduzi
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
25,579
2,000
Baada ya kumkanyaga Namungo na kusepa, hivi ndivyo tulivyomgeukia aliyebaki

giphy (9).gif
 

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,472
2,000
Naam Naam kama kawaida mnyama anaua mtu Leo ushindi upo ila nitafurahi zaidi kushinda Kwa clean sheet Ili tumalize haya mashindano bila kufungwa goli hata Moja.

Mechi za Simba na Azam siku zote huo zinatoa game nzuri sana sababu wote ni waumini wa Soka safi Soka biriyani wote wanaweka mpira chini hivyo natagemea kuwa mchezo wenye burudani kubwa ya soka hasa katikati ya kiwanja.

Kikosi changu naweza kiweka hivi
1 Manula
2 Kapombe
3 Zimbwe Jr
4 Onyango
5 Inonga Baka
6 Mkude
7 Kibu Denis
8 Kanoute
9 Kagere
10 Bwalya
11 Pape Sakho

Morrison namuweka benchi kama game changer ikiwa ufanisi wa Kibu utakuwa mdogo upande wa kulia na Azam hawashambulii sana basi hapo Kibu atampisha Morrison huku Dillunga akimsubiri Sakho.

Mugalu Hana mechi fitness hivyo ataanzia benchi.
Muzamiru atakuwa Benchi kusoma upepo wa viungo wa Azam pale katikati ikiwa watajaza viungo wengi basi Ataingia Muzamiru kuchukua nafasi ya Bwalya sababu si mkabaji mzuri timu ikishambuliwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom