SIMANZI: Ajinyonga baada ya kusalitiwa na mpenzi wake, aacha barua yenye ujumbe mzito

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,353
Kijana mmoja kwa Jina la Fredrick Richard amefikia hatua ya kujinyonga baada ya mpenzi wake (Rose) kumsaliti na kugawa tunda kwa rafiki yake kwa jina Robert. Kabla ya kufikia maamuzi ya kujitoa uhai, kijana huyo aliandika barua ya simanzi kusikitishwa kwa kitendo alichofanyiwa na wawili hao.

index.jpeg

15179075_138270363318863_6455862868763144313_n.jpg


06623bf58e3cb78ac6434f0efbe5fb06.jpg


NOTE: Sitaki ushahidi, nimeiweka hapa baada ya kujiridhisha kutoka kwa rafiki zake kuwa ni kweli amejinyonga kisa mapenzi.
----

MOYO SUKUMA DAMU, SI VINGINE..

=====

Tazama mjadala kuhusu mkasa huu ukisomwa kwenye JamiiLeo
 
Kupenda kupitiliza wakati mwingine ni tatizo sana hasa kwetu sisi weusi, linapokuja suala la mapenzi hasa usaliti, kama unaona huwezi peke yako ni bora ushirikishe rafiki zako wa karibu ili waweze kukusaidia kuliko kutaka kumaliza jambo hilo peke yako! Hatuna la kusema zaidi ya kumtakia mema huko aendako, apumzike kwa amani huko alipo!
 
Mzazi nimehangaika kusomesha weee, mwenyewe hata kiwanja sikujinunulia nikawekeza kwa huyu mtoto now amepata kazi nasema afadhali nuru inakuja halafu leo naletewa barua eti kajiua kisa demu, haki ya Mungu nitamfuata huko huko kuzimu kudadeki
 
Maji ya moto yamekuwa baridi..
Acha waoane.
Tumuombee kwa MUNGU apunguziwe adhabu
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom