Simanjiro: Wananchi wachachamaa Katibu wa CCM kumsimamisha kazi mwenyekiti wa Kijiji

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wananchi wa Kijiji Cha Kilombero kata ya Chambarai wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara wametishia kuandamana Kwa mkuu wa wilaya hiyo kupinga kusimamishwa uongozi Kwa mwenyekiti wao Nguti Kirusu kulikofanywa na katibu wa CCM wilayani humo ,Ally Kidunda kinyume Cha utaratibu.

Wakiongea katika mkutano wa hadhara kijijini hapo,mamia ya wananchi hao wakiwa na jazba walitoa siku Saba mwenyekiti wao Nguti Kirusi awe amerejeshwa madarakani wakidai kuwa shughuli nyingi za maendeleo zilizoanzishwa na mwenyekiti wao zimesimama.

Robert Matua ambaye ni mkazi wa kijiji hicho alisema kwamba wao kama wakazi wa Kijiji hicho bado wanamhitaji kiongozi wao kwa kuwa kuna miradi mbalimbali ambayo walishaanza kuitekeleza lakini kwa sasa imekwama.

Aliitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule ya msingi,zahanati na nyumba ya walimu lakini kwa sasa vyote vimesimama kwasababu ya chuki za kisiasa.

"Sisi bado tunamhitaji kiongozi wetu kwa kuwa kuna miradi mbalimbali alikuwa anatuhamasisha sana kuchangia leo wanamsimamisha kwa chuki tu za kisiasa sisi hatukubali"alisema Matua.

Swalehe Abubakar na Mary Christopher wao walisema kwamba kijiji chao kimekuwa na mgogoro wa muda mrefu wa mpaka na kijiji cha Olbiri na kufafanua kwamba Mwenyekiti wao amekuwa mstari wa mbele kutetea ardhi ya kijiji chao na ndio sababu yake kusimamishwa.

Salome Leng'atu alidai kwamba diwani wao,Julius Lendau ambaye anatokea kijiji cha Olbiri amekua chanzo cha mgogoro wa mpaka huo kwa kuwa sehemu kubwa ya ardhi ambayo ni eneo la malisho ya mifugo limemegwa kinyemela na Mwenyekiti wao amekuwa mstari wa mbele kupigania ardhi iliyomegwa.

Alipoulizwa diwani huyo kuhusu taarifa hizo alipinga vikali yeye kuchochea mgogoro huo huku akifafanua kwamba tayari kuna tume imeundwa kutoka halmashauri kufuatilia mipaka halali ya vijiji hivyo na kuwataka wananchi wavute subira majibu ya tume hiyo.

Katibu wa Ccm wilayani Simanjiro,Ally Kidunda alipoulizwa chanzo cha chama hicho kumsimamisha mwenyekiti huyo alisema kwamba wao kupitia kamati ya siasa wilaya waliamua kumsimamisha mwenyekiti huyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Alifafanua kwamba Ccm wana haki ya kumsimamisha kwa kuwa chama chao ndio kilimpa dhamana na kumsimisha kuwania nafasi aliyonayo.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Seleman Serera alisema kwamba ameshtushwa na taarifa kwa kuwa mwenyekiti aliyesimamishwa ni mtumishi wa serikali huku akifafanua kuwa chama kilipaswa kikae na serikali kushauriana kabla ya kupitisha maamuzi yake.

Alisema kuwa tayari amemuagiza katibu tawala wa wilaya ya Simanjiro,Musa Waziri kufuatilia kwa kina suala hilo na Kisha kumpatia majibu ya uhakika kabla hajatoa tamko lolote.

Mwisho


IMG_20211004_162812_172.jpg
 
Wananchi wa Kijiji Cha Kilombero kata ya Chambarai wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara wametishia kuandamana Kwa mkuu wa wilaya hiyo kupinga kusimamishwa uongozi Kwa mwenyekiti wao Nguti Kirusu kulikofanywa na katibu wa CCM wilayani humo ,Ally Kidunda kinyume Cha utaratibu.
Izuri kwa Sasa wapinzani hawamo,mnajiangushia jumba bovu wenyewe.
 
Labda nieleweshwe kidogo,

Huyo Mwenyekiti amesimamishwa uanachama au Uenyekiti wa Kijiji...!

Ki utaratibu Katibu wa CCM Hana Mamlaka ya kumsimamisha Mwenyekiti wa Kijiji.
 
Mhh! Chama kumsimamisha mwenyekiti wa serikali ya kijiji imekaaje hii! Au katibu wa ccm amewaona wamasai ni hamnazo? Na ajitafakari! Yeye ni "lumeghi" tu asitake kutuchanganya sisi ma laigwanan! Syieeee inarugumenye
 
Haya ndiyo madhara ya kupitishwa bila kupingwa,utakoromewa na kuondolewa kwenye nafasi ya mwenyekiti hata na kibaka ambaye hana hata mamlaka ya kukuondoa kwenye nafasi yako na usifanye kitu chochote kwa kuwa nafasi yenyewe uliipata kiharam.
 
Huyo Katibu wa CCM anatoa wapi mamlaka ya kumsomamisha kazi Mwenyekiti wa Kijiji?
 
Ni zipi taratibu sahihi Za kumuondoa Mwenyekiti wa Kijiji uongozi? kama hafai na ni kero kwa wananchi anaowaongoza?
 
Ni zipi taratibu sahihi Za kumuondoa Mwenyekiti wa Kijiji uongozi? kama hafai na ni kero kwa wananchi anaowaongoza?
Mkutano Mkuu wa Kijiji au Mkuu wa Wilaya ndiyo mwenye Mamlaka hayo, viongozi wa chama wanachoweza labda kumvua uanachama kwa taratibu zao zilizowekwa na chama ili akose sifa ya kuwa Mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom