Simanjiro: Auawa Kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga kwa kumpa ujauzito Mke wa mtu

Naamini Sio kila kifo amepanga Mungu...inawezekanaje ukajimilikisha mke wa mtu hadi kufikia hatua ya kumpa mimba?..marehemu alijitakia...
 
Simanjiro Manyara

Mke wa mtu ni sumu walisema wahenga

Mkazi wa Simanjiro Mkoani Manyara ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya mchepuko wake ambaye ni mke wa mtu kukiri Ujauzito alionao sio wa mumewe bali wa mchepuko huyo

Ndugu wa mume aliyeibiwa mke kwa ghadabu walichukua Sheria mkononi kwa kumuua kwa mapanga

RPC Manyara amethibitisha tukio hilo na uchunguzi unaendelea

MCL
Mke wa mtu ni SUMU wahenga walisemaga
 
Daktari wa mifugo wa kijiji cha Loiborsoit A wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, Malipe Ole Kisota ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu waliomtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao.

Imeelezwa kuwa alikatwa na sime sehemu mbalimbali mwilini na ndugu watatu, Lazaro, Mamei na Supek Mamei, wakimtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao Kinaruu Mamei.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Marrison Mwakyoma akizungumza Novemba 13,2021 ameieleza Mwananchi Digital kwa njia ya simu kuwa mauaji hayo yametokea Novemba 11,2021.

Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi, akidai marehemu alikuwa akituhumiwa kutembea na mke wa mtu na alikuwa anatafutwa akawa anajificha na siku ya tukio walimkibiza, kumkamata na kufanya mauaji hayo.

"Mwanamke alipohojiwa alikubali kuwa na mimba ya mtu mwingine ndipo mume wake akachukua uamuzi wa kikatili wa kumuua akishirikiana na ndugu zake," amesema kamanda Mwakyoma.

Kamanda Mwakyoma amesema watuhumiwa hao watatu walitoroka kusikojulikana mara baada ya mauaji hayo ila wanaendelea kuwatafuta ili wawafikishe mahakamani.

"Natoa wito mtu anapobaini mwanamke ameolewa kisha amepewa mimba na mwanaume mwingine ni bora waachane au kusuluhisha kuliko kufanya mauaji," amesema kamanda Mwakyoma.

Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo, Alais Sasinee amesema Ole Kisota (mume wa mwanamke anayedaiwa kupewa ujauzito) aliuawa na ndugu hao kwa kucharangwa sime baada ya kutoka kuangalia mpira wa miguu baina ya timu ya Taifa ya Tanzania na DRC-Congo.

Chanzo: Mwananchi
 
Simanjiro Manyara

Mke wa mtu ni sumu walisema wahenga sote tujihadhari

Mkazi wa Simanjiro Mkoani Manyara ambaye ni Daktari wa Mifugo ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya mchepuko wake ambaye ni mke wa mtu kukiri Ujauzito alionao sio wa mumewe bali wa mchepuko huyo

Ndugu wa mume aliyeibiwa mke wakishirikiana na ndugu yao aliyeibiwa mke kwa ghadabu walichukua Sheria mkononi kwa kuamua kumuua mgoni wao kwa mapanga

RPC Manyara Kamanda Mwakyoma amethibitisha tukio hilo na uchunguzi unaendelea

MCL
Wamemuonea bure huyo jamaa wangemcharanga na huyo malaya mwenzake wakazikwe kaburi moja
 
Ya nini kuua mzinzi? Unamuachi mazima huyo mke awe wake, inauma sana kugongewa mke mpaka anajazwa mimba
 
Kungekua na sheria kali kwa wezi wa wake za watu yasingetokea haya, ni wakati serikali iweke sheria ya wizi wa wake za watu, mke ni property kama property nyingine
 
Simanjiro. Daktari wa mifugo wa kijiji cha Loiborsoit A wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, Malipe Ole Kisota ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu waliomtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao.

Imeelezwa kuwa alikatwa na sime sehemu mbalimbali mwilini na ndugu watatu, Lazaro, Mamei na Supek Mamei, wakimtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao Kinaruu Mamei.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Marrison Mwakyoma akizungumza Novemba 13,2021 ameieleza Mwananchi Digital kwa njia ya simu kuwa mauaji hayo yametokea Novemba 11,2021.

Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi, akidai marehemu alikuwa akituhumiwa kutembea na mke wa mtu na alikuwa anatafutwa akawa anajificha na siku ya tukio walimkibiza, kumkamata na kufanya mauaji hayo.

"Mwanamke alipohojiwa alikubali kuwa na mimba ya mtu mwingine ndipo mume wake akachukua uamuzi wa kikatili wa kumuua akishirikiana na ndugu zake," amesema kamanda Mwakyoma.

Kamanda Mwakyoma amesema watuhumiwa hao watatu walitoroka kusikojulikana mara baada ya mauaji hayo ila wanaendelea kuwatafuta ili wawafikishe mahakamani.
 
Safi sana... halafu kanakuja kabinti kamoja eti sheria mkononi, sheria mkononi wakati mtu amenizinia mke wangu! Wakafie mbele huko
 
Back
Top Bottom