Simanjiro: Auawa Kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga kwa kumpa ujauzito Mke wa mtu

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,702
Simanjiro Manyara

Mke wa mtu ni sumu walisema wahenga sote tujihadhari

Mkazi wa Simanjiro Mkoani Manyara ambaye ni Daktari wa Mifugo ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya mchepuko wake ambaye ni mke wa mtu kukiri Ujauzito alionao sio wa mumewe bali wa mchepuko huyo

Ndugu wa mume aliyeibiwa mke wakishirikiana na ndugu yao aliyeibiwa mke kwa ghadabu walichukua Sheria mkononi kwa kuamua kumuua mgoni wao kwa mapanga

RPC Manyara Kamanda Mwakyoma amethibitisha tukio hilo na uchunguzi unaendelea

------
Daktari wa mifugo wa kijiji cha Loiborsoit A wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, Malipe Ole Kisota ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu waliomtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao.

Imeelezwa kuwa alikatwa na sime sehemu mbalimbali mwilini na ndugu watatu, Lazaro, Mamei na Supek Mamei, wakimtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao Kinaruu Mamei.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Marrison Mwakyoma akizungumza Novemba 13,2021 ameieleza Mwananchi Digital kwa njia ya simu kuwa mauaji hayo yametokea Novemba 11,2021.

Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi, akidai marehemu alikuwa akituhumiwa kutembea na mke wa mtu na alikuwa anatafutwa akawa anajificha na siku ya tukio walimkibiza, kumkamata na kufanya mauaji hayo.

"Mwanamke alipohojiwa alikubali kuwa na mimba ya mtu mwingine ndipo mume wake akachukua uamuzi wa kikatili wa kumuua akishirikiana na ndugu zake," amesema kamanda Mwakyoma.

Kamanda Mwakyoma amesema watuhumiwa hao watatu walitoroka kusikojulikana mara baada ya mauaji hayo ila wanaendelea kuwatafuta ili wawafikishe mahakamani.

"Natoa wito mtu anapobaini mwanamke ameolewa kisha amepewa mimba na mwanaume mwingine ni bora waachane au kusuluhisha kuliko kufanya mauaji," amesema kamanda Mwakyoma.

Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo, Alais Sasinee amesema Ole Kisota (mume wa mwanamke anayedaiwa kupewa ujauzito) aliuawa na ndugu hao kwa kucharangwa sime baada ya kutoka kuangalia mpira wa miguu baina ya timu ya Taifa ya Tanzania na DRC-Congo.

Chanzo: Mwananchi
 
Simanjiro Manyara

Mke wa mtu ni sumu walisema wahenga

Mkazi wa Simanjiro Mkoani Manyara ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya mchepuko wake ambaye ni mke wa mtu kukiri Ujauzito alionao sio wa mumewe bali wa mchepuko huyo

Ndugu wa mume aliyeibiwa mke kwa ghadabu walichukua Sheria mkononi kwa kumuua kwa mapanga

RPC Manyara amethibitisha tukio hilo na uchunguzi unaendelea

MCL
Simanjiro Hakuna serikali
 
Simanjiro Manyara

Mke wa mtu ni sumu walisema wahenga

Mkazi wa Simanjiro Mkoani Manyara ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya mchepuko wake ambaye ni mke wa mtu kukiri Ujauzito alionao sio wa mumewe bali wa mchepuko huyo

Ndugu wa mume aliyeibiwa mke kwa ghadabu walichukua Sheria mkononi kwa kumuua kwa mapanga

RPC Manyara amethibitisha tukio hilo na uchunguzi unaendelea

MCL
Safi kabisa
 
Kwani hao si ndio jadi yao mwanaume akitaka kumla mke wa mtu anasimika mkuki mlangoni anazama bomani anajilia vyake, au now days wamestaharabika
 
Hakuna serikali pale. Mji Hauna lami 1/4 kms . Ole sendeka mungu anakuona.
Lami ndio serikali mkuu? Anyway serikali ipo pale Ila kuhusu lami wangejitahidi hata waweke kuanzia KIA Ila najua hii njia ya kupitia Oljoro ndio karibu sema Ina madaraja mengi ya kujenga kushinda upande wa KIA.

WAKIWEKA LAMI KUTAKUWA POA SANA SABABU PIA KULE KUNA MASHAMBA MAKUBWA YA MAZAO NA NI SHORT CUT NZURI YA KONDOA, KILOSA, SAME NK.
 
Back
Top Bottom