Silly Politics: Sasa tunashindanisha Umati na kuamua kwa kufuata uzuri wa sauti?

Asante sana mwanakijiji
hili tatizo wanalo vijana wa chadema wanashindana kuona picha baada ya
kusikia hoja.

Na hoja za juzi kwenye mkutano wa kina lema moshi zote wazungumzaji
watatu wamuongelea kinana na ufisadi wake kweli kabisa.

Kwa eneo kama moshi nigetarajiwa hoja.
1.Tutafuaje kahawa irudi kwenye chati kama zamani
2.Katiba mpya
3.Vipi sekta utailii inawezwa boreshwa tukatoa ajira hasa kipindi hiki
cha mwezi wa 12 wachaga wengi wanarudi makwao kwanini tusibuni mfumo wa
kuwashawashi japo wapande mlima kilimanjaro japo waende mbuga za wanyama
kwa siku moja.
4.Tuwazaje kupambana na ushawashi wa kenya kuufanya mlima kilimanjaro ni
wao.
5.Tunawazaje kufaidika na soko kubwa likijengwa rombo na wananchi wa
kenya waje pale kununua mazao
6.Tunawezaje kuifanya rombo itajirike kwa barabara ya sasa.
7.Tunawezaje kuwakomboa wale kina mama wanaouza ndizi,nyanya vituoni

Lakini kuendelea kucheza na ngoma za ccm ni upuuzi eti kinana sio raia
kweli mnaenda ongea majukwaani mnatupotezea muda.

Fred kavishe

Mkuu tunaitaji wachambuzi wengi kama wewe ili kweli JF iwe home of GT
 

Kwako
mwanakijiji :

mwanakijiji kifupi ccm wameshapoteza mwelekeo sababu ya kushindana na
chadema!! Chadema ni chama makini (TAASISI) na kinazidi kukubalika kwa
watanzania mfano kizazi kipya....ni ajabu kukuta kijana ni mfuasi wa ccm
labda akapimwe akili ingawa katiba inamruhusu!!

Mfano mdogo tu Chadema inatetea raslimali za taifa ziwanufaishe
watanzania wote ccm NI MWIKO KWAO.

Kituko cha juzi Arusha CCM inasomba watu toka Monduli na A to Z eti
ionekane imejaza mkutano...Chadema wakiitisha mkutano watu nyomi (UMATI)
wanakuja bila kusombwa na mabasi wala pilau!!!

Mwanakijiji juzi Lema kaitisha mkutano Arusha ndani ya masaa mawili watu
wakajaa...mizani hiii inaonyesha CHADEMA katika medani za kisiasa iko
stage ya juu tofauti na CCM bado wanamambo ya kizamani tena kama watoto
wadogo kuigiliza....ukiona mtu mzima anaigiliza basi KAISHIWA!!!

Uzi wako mwanakijiji usomeke hivi:
VIONGOZI
WAPYA WA CCM WANAZOA MAPESA KWA KIGEZO CHA
KUPAMBANA NA CHADEMA
(DEMOKRASIA)!!

Mkuu hii thread si level yako ngoja thread ya Le mutuz
 
M/kijiji umeleta thread yenye kufikirisha na naona inajadiriwa na ma gt kwa hoja...NAONA YULE CHIZI WA MZEE TINGA2 HAJAPITA KUHARIBU NA mwenzi yule wa gongolamboto
 
Bila watu utakuwa unahutubia hewa? Mkuu Mzee Mwanakijiji naona na wewe umeshaanza kuzeeka sasa unataka waende radio Tanzania kuhutubia lazima kwenye mkutano wa hadhara nyomi lionekane mkuu na waje wenyewe sio kwa fuso
 
Last edited by a moderator:
Niongeze swali la kichokozi; kwenye nchi ambapo kundi kubwa la vijana hawana ajira na wanajishughulisha kwa kubangaiza hapa na pale kuna uwezekano wa mtu kukosa umati wa watu kweli? Ushahidi upo kwenye matamasha mbalimbali, ajali zinapotokea n.k kuweza kukusanya watu wengi mahali pamoja kwenye tukio siyo kigezo cha kukubalikwa kwa sera au hata uwezo wa vyama kuvutia watu - watu wetu hawana la kufanya so ukiwapa cha kufanya au cha kuangalia watakuja tu! Think about it.

But they are still voters,wawe na ajira wasiwe na ajira,muulize Obama atakueleza alivyoshinda majuzi pamoja na matatizo lukuki ya uchumi nchini mwake,chezeiya wapiga kura wewe!
Remember Adolf Hitler uchaguzi wa 1933?
 


Mkuu hapa nilipopaka rangi ya bluu kwa heshima kubwa naomba kutofautiana na wewe.
Mtaji mkuu wa mwanasiasa ni watu kama vile ambavyo mtaji wa benki ni pesa taslim.

Wapo wanaoamini hivyo; lakini ukweli ni kuwa mtaji wa mwanasiasa ni uzuri wa hoja zake na siyo watu. Ukiwa na hoja nzuri watu watakuja lakini siyo tu watu watakuja lakini watakubali hoja zako na watakupigia kura. Ukilenga kukusanya watu wengi tu na ukajisifia kuwa una watu wengi ni kweli itakufanya uamini una mtaji mkubwa!! Lakini hawa watu wasipokupigia kura utasema kama CUF "mtaji haukutosha"? Hatulengi kukusanya watu wengi kwenye mikutano tunataka kuwafikia watu wengi kwa ujumbe unaowapa matumaini na kuwafanya wakubali kupigia kura chama.

Ukiendekeza kukusanya watu wengi hautapata shida; watakuja wengi kwenye mikutano, na watakuja wengi kwenye kampeni lakini kwenye siku ya kupiga kura hawaji- hawajui mnataka kufanya nini? Kuwaambia watu wengi ubaya wa CCM na serikali yake ni mwanzo tu. Lakini katika nchi ambayo tayari watu wengi wanajua udhaifu wa serikali iliyoko madarakani kuwahubiria udhaifu huo kila kukicha unaamini ni mkakati mzuri? Au mnafikiri Watanzaniawana vichwa vya nazi kwamba hawajaelewa tatizo lao ni nini?

Lakini ambacho nilichokuwa ninazungumzia sana - labda hakijawa wazi sana - ni hii tabia ya kupenda umati kwenye mitandao na kwenye habari. Tunataka tuone picha zina umati wa watu kiasi gani na hatuulizi kwenye umati huo kilisemwa nini? Tunajiuliza "wangapi walijiunga na chama" au wangapi walirudisha kadi za chama kingine na tukiona ni wengi basi tunaona mambo ni mazuri.

Hii ni silly politics.
 
Mkuu mada yako nzuri lakini mtazamo wako kuhusu vyama vya siasa na umati umepwaya.

Umeonekana kana kwamba we si Mchambuzi mahari katika uwanja wa siasa.

Kwa ufupi mkuu SIASA(chama) ni UMATI (watu). Chama bila umati si chama, na kipimo cha chama imara ni wingi wa watu unaounga mkono hicho chama.

Chama kinapoungwa mkono na watu wengi ni udhibitisho kwamba sera za chama hicho au at least mikakati yake inakubalika na watu hao au huo umati. Katika kila mkutano wananchi huelezwa baadhi ya sera za chama. Haiwezekani sera zote zikaelezwa katika mkutano mmoja. Katika mikutano vile vile wananchi huelimishwa mambo mbali mbali yanayowahusu na wakati mwingine hufafanuliwa baadhi ya mambo ambayo huletawa kwao na serikali.

Kwa ujumla Mkuu usidhani kwenye mikutano ya vyama ni kitu cha aina moja kama vile uoza tu wa chama tawala ndio huelezwa. Mambo mengi kama vile mikakati na sera za chama husika huelezwa.

Najua Mkuu wewe umefikiria kuwa umati si hoja nadhani kwa sababu ya uchakachuaji wa matokea unaofanywa na chama tawala kwa kutumia mbinu mbali mbali.

Kungekuwa na taratibu halali za upigaji kura ungehakikisha nayo yasema. Lakini hata hivyo Mkuu haya mambo ya uchakachuaji yana mwisho wake!
 
Kwa ufupi mkuu SIASA(chama) ni UMATI (watu). Chama bila umati si chama, na kipimo cha chama imara ni wingi wa watu unaounga mkono hicho chama.

Chama kinapoungwa mkono na watu wengi ni udhibitisho kwamba sera za chama hicho au at least mikakati yake inakubalika na watu hao au huo umati.

Angalia sana hoja yangu ya "umati kwenye picha" sijasema kuungwa mkono na watu wengi ni tatizo!
 
Hoja? Vijana wa fasta fasta wana muda gani na hoja au kushindana kwa hoja? JF yenyewe ushindani wa hoja uliisha mwaka 2010 na kilichobaki sasa ni uwingi wa wapiga makofi kwenye yale wanayokubaliana nayo na kurusha matusi kwa yale wasiyokubaliana nayo. Tunataka elimu ya fasta fasta bila kusoma vitabu vingi. Tunataka utajiri wa fasta fasta bila kuchapa kazi. Na sasa hata siasa zetu ni fasta fasta. Mwisho wake hata elimu ambayo wengi wanapata hapa na kuiamini ni ile ambayo huenda sio sahihi sana. Mkumbo na uwingi wa washangiliaji una nafasi kubwa kuliko uwingi wa maarifa au hekima ndani yake.

Hata kwenye wanachama ni yale yale, lete kadi tugawe huku. Kadi kugawiwa kama njugu ndio siasa zetu za karne ya 21. Hao wengi ni wapenzi tu na wala hawastahili hata kuwa wanachama. Ndio maana kila baada ya muda tunashuhudia wakihama vyama kama mlimani wanavyohama madarasa ya lectures. Ingelikuwa uwingi wa wanachama unasaidia, basi CCM wangeshinda majimbo yote ambayo yamegombewa huko nyuma. Na ingelikuwa umati wa watu ndio kigezo cha ushindi, basi CHADEMA wangelichukua viti vyote vya udiwani mwezi wa 10.

Kikubwa tunashindwa kuwaandaa viongozi wa kesho kwasababu hatuwaulizi maswali magumu. Tunatumia muda mwingi kuwatukuza kama wafalme au kuwatukana kama vibaka. Matokeo yake huko mbele tutakuwa na viongozi ambao hawana uwezo wa kushughulikia matatizo ambayo ni complicated. Wengi wao wanaishi katika a 2-demensional world; a black and white world; dunia ya common sense. Wanasahau kwamba in reality, issues mbalimbali ni complicated, zinahitaji N-demensional thinking; common sense au status quo haitoshi tena kutatua matatizo yetu. Tunahitaji watu ambao sio tu wanaweza kuangalia the common sense bali pia the un common sense issues ambazo zinatukabili.

Tunatengeneza taifa la waongo maana hakuan fact checks. Mtu anaweza kuahidi kuibadili dunia kuwa mbingu na washabiki watashangilia. Hakuna wenye courage hata ya kuuliza maswali rahisi, je pesa utatoa wapi? Itagharimu kiasi gani? Italeta faida kiasi gani? Nk.
 
1220_D45.jpg

chadema%2Bsupporters.jpg


" border="0">

Sijui ni kitu gani kinaendelea; hatushindanishi hoja tena, hatupingani kwa hoja tunaanza kushindanisha umati. Kwamba ni mwanasiasa gani anapata watu wengi na ni mwanasiasa gani hapati watu wengi kwenye mikutano yake. Kwamba kwa kuangalia umati wa watu kwenye mikutano tunaamua ni yupi anakubalika na yupi hakubaliki na hivyo tunachagua nani wa kumfuata na nani wa kutomfuata?

Fikiria habari inaletwa kuwa kuna mkutano wa CHADEMA mahali ambao utahutubiwa na viongozi fulani. Kwa haraka watu wanataka "waone picha". Utasikia mtu anakimbia na kusema "nitawaletea picha hivi punde". Na kweli watu wanasubiria kuona picha "za mkutano" zilivyo na watu nyomi. Sasa kwa vile mkutano unaweza kuwa na watu wengi kweli basi baadhi ya watu wanajisikia furaha kuwa CDM imepata watu wengi.

Upande mwingine nao ni vile vile. Kiongozi wa CCM anaenda kufanya mkutano au kundi la viongozi wanaenda kufanya mkutano na wao wanafanya haraka kuleta picha. Na kama taarifa za kuwa watu wanakusanywa na mabasi nazo ni kweli basi na CCM nao wanataka kuwa na 'watu wengi' kwenye mikutano yao. Hivyo, picha itafanyiwa haraka kuonesha kuwa "hata" kwenye mikutano ya CCM watu wengi wanakusanyika.

Na katika sehemu zote mbili picha haziwezi kunoga bila watu (mamia au maelfu) kuvaa nguo za rangi za chama. Na kwa hivi tunaamua ni hali gani ya kisiasa iliyopo. Na pamoja na rangi sasa wapiga picha wetu (ambao wengi nao wana maslahi na vyama husika) hawapigi picha za kuonesha upande mbaya kwani wote watatafuta sehemu ambapo watapiga picha kuonesha umati. Na tunapoona umati kuna kitu kinatufanya tujisikie vizuri kuwa kwa kweli mambo siyo mabaya; tunashindanisha umati.

Lakini jingine ambalo nalo nimeliona na linaendelea kuonekana ni kuwa tunashindanisha nani anazungumza vizuri na kwa ukali wa maneno au kwa mwamko na jazba ya kutufanya tuamini kuwa ni mzungumzaji mzuri. Hivi majuzi kijana mmoja aliniuliza kuhusu kiongozi mmoja wa chama cha upinzani na kuniambia "anajua kujenga hoja" na kuwa "ni mzungumzaji mzuri". Nilimuuliza kijana huyo kijana juu ya hoja zinazotolewa na kiongozi huyo na kijana akashindwa kuelezea isipokuwa kuzirudia hoja zilivyo. Nilipoanza kuonesha fallacy za hoja hizo kijana wa watu akaona kama najaribu kumtusi huyo kiongozi!

Tunawaangalia wanasiasa wetu na kuwasikiliza wanavyozungumza majukwaani na kufurahia jinsi wanavyozungumza kwa ukali, kwa mbwembwe na kwa kuonesha wana uchungu sana. Sasa hili linanoga zaidi kama linafanyika kwenye umati mkubwa basi sauti, mbwembwe na mwamko wa umati unatufanya tulinganishe vyama hivyo hivyo. Sasa utaona CCM na wenyewe wakisimama majukwaani wanazungumza kwa ukali na kwa mbwembwe huku wakishangiliwa - wengi tunakumbuka Mr. Kudadadeki!

Sasa hakuna ubaya kuwa na umati wa watu na wala hakuna ubaya wa watu kuzungumza kwa mbwembwe na kwa jazba. Lakini kuna tatizo kama hatujui kusikiliza hoja zinazotolewa na kushindanishana kwa hoja, kwa sera, kwa mitazamo na kwa maono. Kuna faida gani watu kubishana nani amezaa na nani au nani ni fisadi kama hatusikii tofauti ya sera, mitazamo, maono na mwelekeo wa vyama vyetu vya siasa.

Binafsi ningependa kusikia CCM ikitetea sera zake na mafanikio yake na kueleza kwanini sera zake ziendelee kutumika nchini. Lakini kwa vile ninaamini sera hizo zimeshindwa kuliongoza taifa letu ningependa kusikia zaidi CDM wakizikosoa sera hizo na kutueleza wao wangefanya nini tofauti. CDM haipaswi kutuambia nyumba iliyojengwa na CCM ni mbovu na kuwa mafundi waliotumika ni wabovu na kuwa haiwezi kuhimili mafuriko au matetemeko. Watu wanachotaka kusikia ni kuwa wao wakiibomoa hiyo nyumba watajenga nyumba ya aina gani ambayo itakuwa tofauti na ile ya CCM?

Na sisi wananchi, wanachama na mashabiki wa vyama vyetu tuanze kukataa kuambiwa stori za kusemezana na kurushiana vijembe; tudai hoja. Tudai kusikia mwelekeo mpya wa taifa letu; tuulize "wanafanya nini" ama "watafanya nini". Kwa CCM ni rahisi kwani wao wanahitai kuulizwa "kwanini hawajafanya x,y" kwa sababu wao wako madarakani. wanatakiwa wajibu - siyo wasema "mbona". CDM wasiachwe waendelee kusema "waone wanafanya x,y" tunataka wao nao wasema watafanya nini? Watuambie ubaya wa sera za CCM na matokeo yake na uzuri wa sera zao.

Lakini tusipoanza kudai haya na kuyaoana haya tutaendelea kuletewa picha, tutashangilia na kufurahia na kujisikia vizuri. Na kwa kadiri inavyoonekana picha zitazidi kuletwa za kila aina huku watu wakibishana ni yupi ana picha nzuri. Silly Politics. Picha zitufanye tuhoji 'walisema nini"? "Je kilichosemwa kina ukweli"? "Je kilichosemwa kina makosa gani?". Picha ziwe alama za kutuelekeza kwenye maswali ya hoja na tupate majibu. Sasa watu wanatuwekea picha mtu akivikwa mgololo au amekaa mezani halafu haisemwi kimezungumzwa nini wanafikiria watu watahisi kwa kutumia njia ya mnunurisho kujua kilichosemwa.

Tusiridhike na picha, turidhishwa na hoja.

Hoja zijibiwe kwa hoja.
Mzee mwana kijiji huwa na
nipasoma thread zako nazisoma kwa utaratibu wa nidhamu ya hali ya juu mara nyingi naogopa kuchangia nikiamini kuwa nitaharibu madini safi ya hoja ulizojenga. Mzee kwa hili leo nasema nachangia japo kidogo tu. ulichokiongea ni kweli tupu. Ila Wapinzani na sio CDM tu hata SAU,DP,CUF navyo vinatamani kupata watu wengi kwenye mikutano yao. Pamoja na malengo ya Vyama vya siasa kuwa kukamata dola. Bila watu na kujitangaza watakuwa hawajafanya kitu. Na Tangazo ni lazima lionwe na kusikiwa na watu sio miti. Mahudhurio kwenye mikutano yanatangaza hali halisi ya uelewa kutoka eneo moja hadi lingine. Labda tu MM mada hii ingeikomalia CCM ambayo pamoja na kutuibia kwa kalamu huko serikalini lakini wanashuka mpaka Grass root na kutuchangisha kinguvu fedha.diesel kwa ajili ya kutetea Ufisadi kwenye mikutano yao.
 
Ni hoja nzuri sana hasa kwa wakati huu ambao taifa limepoteza mwelekeo CHADEMA kweli wanavuta umati kwenye mikutano lakini tatizo ambalo limeingia katika siasa zetu ni kudili na propoganda bila ya hoja&sera mbadala kulingana na changamoto na mahitaji ya eneo la mkutano.Kwa mfano ningependa kusikia kero za barabara,elimu pamoja na afya inabidi kuwe na semina elekezi kwa makada wetu ili kuweza kuenda na mahitaji ya kisiasa juu ya kero za wananchi ifike mahali tuwe wakweli wananchi wanahtaji kujua jins ya tutakavyotatua kero zao sio ufisadi wa mtu au chama au serikali ni hoja mbadala tu juu ya kero zao
 
inawezekana mzee mwanakijiji ukawa na hoja ya msingi kabisa,ila kinachohitajika sasa hv tanzania ni wazo mbadala yaani mabadiliko,ili tusonge mbele zaidi,kwahiyo CCM ipishe CHADEMA na wenyewe waonyeshe uwezo wao ndivyo demokrasia ya kweli!
 
Niongeze swali la kichokozi; kwenye nchi ambapo kundi kubwa la vijana hawana ajira na wanajishughulisha kwa kubangaiza hapa na pale kuna uwezekano wa mtu kukosa umati wa watu kweli? Ushahidi upo kwenye matamasha mbalimbali, ajali zinapotokea n.k kuweza kukusanya watu wengi mahali pamoja kwenye tukio siyo kigezo cha kukubalikwa kwa sera au hata uwezo wa vyama kuvutia watu - watu wetu hawana la kufanya so ukiwapa cha kufanya au cha kuangalia watakuja tu! Think about it.

At least wakija wanaweza kupata jambo au fikra mpya.....haina haja ya ku ignore.MMJ,Ina element ya kukubalika pia kwa sababu ukifanyika mkutano sehemu moja wote CCM na CDM wakafanya mkutano pale,Lazima idadi ya wahudhuriaji itatofautiana.Why?
 
Jamani hili suala ni zito ni fahari iliyoje kama umati mkubwa unapenda kuja kukusikiliza. Leo watu nyomi kesho ukirudi eneo hilo nyomi maradufu hiyo ni salamu kwamba umeeleweka kama nyomi inapungua jua watu hawakuelewi.
Kwa nini Leo chadema inaonekana kikwazo kwa ccm? Ni kwamba kila wanapoenda mjini au kijijini nyomi hapo ndipo wanapokosa raha. Kwa nini si TLP wala CCK wanaohofiwa? Sababu ni ileile watu wanawapokeaje kiduchu au nyomi. Tuache utani kama vyama viwili vikifanya kampeni eneo fulani wahudhuriaji katika mikutano wakiwa sawa hata matokea yanakuwa si ya kupishana sana.
Sera za chama zinataka mtu mwenye uzalendo wa hali ya juu kuzitekeleza kama kiongozi ni dhaifu hata sera zitungwe na MALAIKA ni kazi bure. Sera ni ngonjera za siasa kazi ni kuzitekeleza kwa vitendo.
 
Wapo wanaoamini hivyo; lakini ukweli ni kuwa mtaji wa mwanasiasa ni uzuri wa hoja zake na siyo watu. Ukiwa na hoja nzuri watu watakuja lakini siyo tu watu watakuja lakini watakubali hoja zako na watakupigia kura. Ukilenga kukusanya watu wengi tu na ukajisifia kuwa una watu wengi ni kweli itakufanya uamini una mtaji mkubwa!! Lakini hawa watu wasipokupigia kura utasema kama CUF "mtaji haukutosha"? Hatulengi kukusanya watu wengi kwenye mikutano tunataka kuwafikia watu wengi kwa ujumbe unaowapa matumaini na kuwafanya wakubali kupigia kura chama.

Ukiendekeza kukusanya watu wengi hautapata shida; watakuja wengi kwenye mikutano, na watakuja wengi kwenye kampeni lakini kwenye siku ya kupiga kura hawaji- hawajui mnataka kufanya nini? Kuwaambia watu wengi ubaya wa CCM na serikali yake ni mwanzo tu. Lakini katika nchi ambayo tayari watu wengi wanajua udhaifu wa serikali iliyoko madarakani kuwahubiria udhaifu huo kila kukicha unaamini ni mkakati mzuri? Au mnafikiri Watanzaniawana vichwa vya nazi kwamba hawajaelewa tatizo lao ni nini?

Lakini ambacho nilichokuwa ninazungumzia sana - labda hakijawa wazi sana - ni hii tabia ya kupenda umati kwenye mitandao na kwenye habari. Tunataka tuone picha zina umati wa watu kiasi gani na hatuulizi kwenye umati huo kilisemwa nini? Tunajiuliza "wangapi walijiunga na chama" au wangapi walirudisha kadi za chama kingine na tukiona ni wengi basi tunaona mambo ni mazuri.

Hii ni silly politics.

Mkuu sina ugomvi na umuhimu wa wapiga kura kuamua wamchague nani kwa kigezo cha ubora wa sera na mikakati ya kuitekelza sera hiyo. Lakini ukweli unabakia pale pale kuwa 'politics is about numbers' period.Hivi unadhani kwa nini duniani kote wakati wa kampeni wagombea huwa wanabandika picha zao kila mahali? Jiulize hizo picha huwa zina ujumbe wowote wa kisera zaidi ya kusema 'chagua MMJ,chagua mabadiliko' yapi mbona huwa hayaelezwi kwenye bango? You know why,lengo linakuwa ni kuuza sura tu,sera baadae. Ushawahi kujiuliza kwa nini vyama vingi duniani huwa vinasimamisha wagombea ma handsome na ma beautiful? Cameron,Tony Blair,Obama,Clinton,Kikwete,Sally wa senegal, just mention it. Seriously speaking imagine CCM imsimamishe Mzee Wassira ? (though namweshimu as a person),atalipa kweli?
ndugu yangu Mwanakijiji,just spare your breath,the name of the game is 'kupiga longo longo' mpaka uingie 1 Magogoni Road ndio uanze serious thinking and strategising,too sad though.Come 2015 i can assure you CCM wataahidi mabomba yanayotoa maziwa,Chadema wataahidi helikopta za kupeleka watoto shule,CUF wataahidi machinga kumilikishwa ma VX,NCCR wataahidi kuleta teknolojia ya kina mama kuzaa bila uchungu,mvua artificial.....the list goes on.Hii ndio dunia tunayoishi mkuu.
 


''''''mwanakijiji kifupi ccm wameshapoteza mwelekeo sababu ya kushindana na chadema!! Chadema ni chama makini (TAASISI) na kinazidi kukubalika kwa watanzania
mfano kizazi kipya....ni ajabu kukuta kijana ni mfuasi wa ccm labdaakapimwe akili ingawa katiba inamruhusu!!''''''

:A S angry::A S angry::A S angry:kizazi kipya!!!!!!! sijui wapi nilipata kusikia neno hili?????!!! ial kama kizazi chenyewe ndio hiki tunachokiona vyuoni,, vijana wanaopenda starehe kuliko kazi!!! wanaokimbilia taaliuma zitakazowafanya kuwa matajiri haraka(mafisadi) kuliko taaluma zinazoijenga nchi!!! hawa wasiojua hata ku-budget fedha kutoka loan board????? hawa wanaotumia boom kwa ajili ya starehe then baada ya wiki mbili wanaamua kuwa MAKAHABA ili waweze kujikimu????? hawa wanaoendeshwa na USHABIKI na maneno ya FARAJA yanayoambatana na ahadi hewa toka kwa politicians bila kusumbua akili ya kupima kila neno?????? hawa kazazi kipya wanoshinda kwenye FACEBOOK,bbm, TWITTER na mitandao mingine ya ngono huku wakiacha kazi zikifanywa na watu wengine????
hawa vijana wenu wakipewa nchi hata kwa seconds 60 watachemsha... kizazi kipya ni kizazi cha nyoka na ndio maana watu wa kawaida kabisa(in every aspect) kama ZITTO KABWE,MNYIKA,MDEE,JANUARY MAKAMBA,NAPE NAUYE, MTATIRO nk,nk,nk tunawaona kama mashujaa na watu uwezo mkubwa sana wakati ni watu wa kawaida saaaana ila tofauti na wengine!!!!WAO WANAJITAMBUA
 
Umesema ukweli babu yangu ila imenipasa kucheka nakumbuka makala yako ila uliyowahi kutoa na kusema sisi tumekuwa makasuku ya siasa hii ni kweli kabisa ila hii inasababishwa na hasa na vyombo ya habari mzee wangu wa village
 
Back
Top Bottom