Silly Politics: Sasa tunashindanisha Umati na kuamua kwa kufuata uzuri wa sauti?


Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,033
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,033 280
1220_D45.jpg

chadema%2Bsupporters.jpg


" border="0">

Sijui ni kitu gani kinaendelea; hatushindanishi hoja tena, hatupingani kwa hoja tunaanza kushindanisha umati. Kwamba ni mwanasiasa gani anapata watu wengi na ni mwanasiasa gani hapati watu wengi kwenye mikutano yake. Kwamba kwa kuangalia umati wa watu kwenye mikutano tunaamua ni yupi anakubalika na yupi hakubaliki na hivyo tunachagua nani wa kumfuata na nani wa kutomfuata?

Fikiria habari inaletwa kuwa kuna mkutano wa CHADEMA mahali ambao utahutubiwa na viongozi fulani. Kwa haraka watu wanataka "waone picha". Utasikia mtu anakimbia na kusema "nitawaletea picha hivi punde". Na kweli watu wanasubiria kuona picha "za mkutano" zilivyo na watu nyomi. Sasa kwa vile mkutano unaweza kuwa na watu wengi kweli basi baadhi ya watu wanajisikia furaha kuwa CDM imepata watu wengi.

Upande mwingine nao ni vile vile. Kiongozi wa CCM anaenda kufanya mkutano au kundi la viongozi wanaenda kufanya mkutano na wao wanafanya haraka kuleta picha. Na kama taarifa za kuwa watu wanakusanywa na mabasi nazo ni kweli basi na CCM nao wanataka kuwa na 'watu wengi' kwenye mikutano yao. Hivyo, picha itafanyiwa haraka kuonesha kuwa "hata" kwenye mikutano ya CCM watu wengi wanakusanyika.

Na katika sehemu zote mbili picha haziwezi kunoga bila watu (mamia au maelfu) kuvaa nguo za rangi za chama. Na kwa hivi tunaamua ni hali gani ya kisiasa iliyopo. Na pamoja na rangi sasa wapiga picha wetu (ambao wengi nao wana maslahi na vyama husika) hawapigi picha za kuonesha upande mbaya kwani wote watatafuta sehemu ambapo watapiga picha kuonesha umati. Na tunapoona umati kuna kitu kinatufanya tujisikie vizuri kuwa kwa kweli mambo siyo mabaya; tunashindanisha umati.

Lakini jingine ambalo nalo nimeliona na linaendelea kuonekana ni kuwa tunashindanisha nani anazungumza vizuri na kwa ukali wa maneno au kwa mwamko na jazba ya kutufanya tuamini kuwa ni mzungumzaji mzuri. Hivi majuzi kijana mmoja aliniuliza kuhusu kiongozi mmoja wa chama cha upinzani na kuniambia "anajua kujenga hoja" na kuwa "ni mzungumzaji mzuri". Nilimuuliza kijana huyo kijana juu ya hoja zinazotolewa na kiongozi huyo na kijana akashindwa kuelezea isipokuwa kuzirudia hoja zilivyo. Nilipoanza kuonesha fallacy za hoja hizo kijana wa watu akaona kama najaribu kumtusi huyo kiongozi!

Tunawaangalia wanasiasa wetu na kuwasikiliza wanavyozungumza majukwaani na kufurahia jinsi wanavyozungumza kwa ukali, kwa mbwembwe na kwa kuonesha wana uchungu sana. Sasa hili linanoga zaidi kama linafanyika kwenye umati mkubwa basi sauti, mbwembwe na mwamko wa umati unatufanya tulinganishe vyama hivyo hivyo. Sasa utaona CCM na wenyewe wakisimama majukwaani wanazungumza kwa ukali na kwa mbwembwe huku wakishangiliwa - wengi tunakumbuka Mr. Kudadadeki!

Sasa hakuna ubaya kuwa na umati wa watu na wala hakuna ubaya wa watu kuzungumza kwa mbwembwe na kwa jazba. Lakini kuna tatizo kama hatujui kusikiliza hoja zinazotolewa na kushindanishana kwa hoja, kwa sera, kwa mitazamo na kwa maono. Kuna faida gani watu kubishana nani amezaa na nani au nani ni fisadi kama hatusikii tofauti ya sera, mitazamo, maono na mwelekeo wa vyama vyetu vya siasa.

Binafsi ningependa kusikia CCM ikitetea sera zake na mafanikio yake na kueleza kwanini sera zake ziendelee kutumika nchini. Lakini kwa vile ninaamini sera hizo zimeshindwa kuliongoza taifa letu ningependa kusikia zaidi CDM wakizikosoa sera hizo na kutueleza wao wangefanya nini tofauti. CDM haipaswi kutuambia nyumba iliyojengwa na CCM ni mbovu na kuwa mafundi waliotumika ni wabovu na kuwa haiwezi kuhimili mafuriko au matetemeko. Watu wanachotaka kusikia ni kuwa wao wakiibomoa hiyo nyumba watajenga nyumba ya aina gani ambayo itakuwa tofauti na ile ya CCM?

Na sisi wananchi, wanachama na mashabiki wa vyama vyetu tuanze kukataa kuambiwa stori za kusemezana na kurushiana vijembe; tudai hoja. Tudai kusikia mwelekeo mpya wa taifa letu; tuulize "wanafanya nini" ama "watafanya nini". Kwa CCM ni rahisi kwani wao wanahitai kuulizwa "kwanini hawajafanya x,y" kwa sababu wao wako madarakani. wanatakiwa wajibu - siyo wasema "mbona". CDM wasiachwe waendelee kusema "waone wanafanya x,y" tunataka wao nao wasema watafanya nini? Watuambie ubaya wa sera za CCM na matokeo yake na uzuri wa sera zao.

Lakini tusipoanza kudai haya na kuyaoana haya tutaendelea kuletewa picha, tutashangilia na kufurahia na kujisikia vizuri. Na kwa kadiri inavyoonekana picha zitazidi kuletwa za kila aina huku watu wakibishana ni yupi ana picha nzuri. Silly Politics. Picha zitufanye tuhoji 'walisema nini"? "Je kilichosemwa kina ukweli"? "Je kilichosemwa kina makosa gani?". Picha ziwe alama za kutuelekeza kwenye maswali ya hoja na tupate majibu. Sasa watu wanatuwekea picha mtu akivikwa mgololo au amekaa mezani halafu haisemwi kimezungumzwa nini wanafikiria watu watahisi kwa kutumia njia ya mnunurisho kujua kilichosemwa.

Tusiridhike na picha, turidhishwa na hoja.

Hoja zijibiwe kwa hoja.
 
F

FredKavishe

Verified Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,091
Likes
19
Points
135
F

FredKavishe

Verified Member
Joined Dec 4, 2010
1,091 19 135
Asante sana mwanakijiji hili tatizo wanalo vijana wa chadema wanashindana kuona picha baada ya kusikia hoja.

Na hoja za juzi kwenye mkutano wa kina lema moshi zote wazungumzaji watatu wamuongelea kinana na ufisadi wake kweli kabisa.

Kwa eneo kama moshi nigetarajiwa hoja.
1.Tutafuaje kahawa irudi kwenye chati kama zamani
2.Katiba mpya
3.Vipi sekta utailii inawezwa boreshwa tukatoa ajira hasa kipindi hiki cha mwezi wa 12 wachaga wengi wanarudi makwao kwanini tusibuni mfumo wa kuwashawashi japo wapande mlima kilimanjaro japo waende mbuga za wanyama kwa siku moja.
4.Tuwazaje kupambana na ushawashi wa kenya kuufanya mlima kilimanjaro ni wao.
5.Tunawazaje kufaidika na soko kubwa likijengwa rombo na wananchi wa kenya waje pale kununua mazao
6.Tunawezaje kuifanya rombo itajirike kwa barabara ya sasa.
7.Tunawezaje kuwakomboa wale kina mama wanaouza ndizi,nyanya vituoni

Lakini kuendelea kucheza na ngoma za ccm ni upuuzi eti kinana sio raia kweli mnaenda ongea majukwaani mnatupotezea muda.

Fred kavishe
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,903
Likes
2,462
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,903 2,462 280
mwana kijiji! umeonesha njia nzuri.ulichosema ni ukweli!Pengine tatizo ninaloliona mimi ni kukosekana kwa itikadi zinazoeleweka kwa vyama vya siasa nchini.hali hiyo husababisha wasiwe na muelekeo na maono ya kisiasa yaliyonyooka,hivyo kujikuta wakiwa wanapigana majungu tu. Mfano CHADEMA, (kumradhi!) ukiachilia mbali kuwalaaumu ccm kuwa ni mafisadi,na kuona kwa kufanya hivyo wana washabiki wengi! kila nikisikia mkutano au mahojiano na viongozi wa chama hiki ajenda kubwa ni ufisadi wa ccm!lakini mimi ninachojua ni kwamba ufisadi ni mfano wa rushwa! suala hili ni zaidi ya ccm.wengi wanaoonekana kupata nafasi nzuri wanafanya ufisadi;wawe ccm au wasiwe!lakini kwa kuwa ccm ndo wako kwenye ulaji kwa sasa ndo maana wanaonekana zaidi.sasa pengine chadema walitakiwa watuambie kwamba wao wakiingia madarakani watafanya nini kuhakikisha hakuna rushwa na ufisadi.
 
POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
6,691
Likes
17
Points
135
POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
6,691 17 135
Umenikumbusha mbali...-The Law of the Picture- "People do what people see" John C.Maxwell, ok kidogo umejichanganya huo ujumbe ni kwa reporter wa JF or kwa Wanasiasa? who is the Stupid?

Well, unataka kujua kinachozungumzwa na wanasiasa? kuna watu wanaenda kukusanyika kila siku, tena mara kwa mara na wasijue nini kimezungunzwa? ama mwanasiasa hasa upinzani wasitoe mbadala wa sera ama hoja za chama tawala? YES who is the stupid!?

Kuna hopja ngapi mbadala zinatolewa tena hata kwa matamko mbali na mikutano? Kuna tofauti kubwa sana wa kisera/ hoja kati ya CCM na CHADEMA, utofauti huu ni kama usiku na mchana...
 
WOWOWO

WOWOWO

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2011
Messages
584
Likes
50
Points
45
WOWOWO

WOWOWO

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2011
584 50 45
Nadhani kuna mambo hayako sawa katika siasa zetu na binafsi nategemea CDM ndiyo wangekuwa dira katika kuleta siasa zenye tija, siasa zitakazotutoa kwenye nyomi kwenda kwenye dira ya taifa.Tutoke kwenye kujadili mambo madogomadogo kwenda kwenye kujadili mambo makubwa na yaliyobeba mustakabali mpana zaidi wa taifa letu.

Ukweli taifa limesimama, mipango hakuna na halieleweki wapi linaenda. Ukimuuliza hata JK leo Tanzania itakuwa wapi baada ya miaka 50 hana jibu, si Kinana, Si Dkt. Slaa, si Mbowe jibu hili litakuwa gumu sana kwao. Wananchi nao wameparaganyika,maisha yamewapiga hawana huduma zozote za msingi na za maana. Ni kama wagonjwa mahututi waliobebwa kwenye machela ya matambala.

Natamani kuona CDM inakuja na Development map ya taifa. Ije na projections za taifa kwa miaka 50 ijayo. Kinachotutesa sasa kama taifa hatuna dira ya muda mfupi, wa kati na mrefu.Tukipata chama kitakacho chora mikakati hiyo na kuiweka hadharani huku kikieleza periodically targets za kitaifa hakika tutabadili upepo wa siasa za sasa.

Ndiyo maana wengi tumekuwa tukisema CDM should go beyond M4C, Vua gamba Vaa Gwanda nk. Ni kweli operesheni hizo ni za muhimu sana lakini Wananchi wanataka pia promise zilizo kwenye mipango na dira ya maendeleo ya Taifa. Shime CDM sasa ikae chini iwatumie wataalamu tulionao ibuni dira ya maendeleo (National Development Map/Vision) ya miaka mingi huko mbele. Ieleze periodically wapi tutakuwa tumefikia miaka kama 30 ijayo.

Tumekwama, tunahitaji kukwamuliwa sasa.Mikutano yetu ya siasa ijikite katika kueleza namna ya kutoka kwenye mkwamo tuliomo.
 
kisu

kisu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Messages
830
Likes
66
Points
45
kisu

kisu

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2009
830 66 45
Kwani sera za CDM hazieleweki? Si mliambiwa ikishika dola, mfuko wa simenti itakuwa sh. 5,000/-, shule bure mpaka chuo kikuu, mafisi wote watafungiwa segerea, nk. au hamkumbuki?
 
R

raymg

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2012
Messages
845
Likes
4
Points
35
R

raymg

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2012
845 4 35
Nmekuelewa MMJ, Wowowo,.....siasa za Tanzania zimekuwa za kishabiki tangia kuasisiwa kwa vyama vingi na hili ndio linaendelea hadi leo, uelewa wa wananchi 1995 kisiasa utakua umebadirika sana mpaka sasa japokua bado tushabikia pengine ni kutokana na kuichoka CC au uelewa wetu bado hadi humu JF!.....lakini CDM au CCM bila kutuambia itikadi ya taifa letu ni ipi bado tutaendelea kutapata tu hata 50 years ijayo hatutaendelea kamwe....
 
K

KGARE

Senior Member
Joined
Jul 31, 2012
Messages
102
Likes
1
Points
35
K

KGARE

Senior Member
Joined Jul 31, 2012
102 1 35
Mzee Mwanakijiji Na sisi wananchi, wanachama na mashabiki wa vyama vyetu tuanze kukataa kuambiwa stori za kusemezana na kurushiana vijembe; tudai hoja. Tudai kusikia mwelekeo mpya wa taifa letu; tuulize "wanafanya nini" ama "watafanya nini". Kwa CCM ni rahisi kwani wao wanahitai kuulizwa "kwanini hawajafanya x,y" kwa sababu wao wako madarakani. wanatakiwa wajibu - siyo wasema "mbona". CDM wasiachwe waendelee kusema "waone wanafanya x,y" tunataka wao nao wasema watafanya nini? Watuambie ubaya wa sera za CCM na matokeo yake na uzuri wa sera zao.
[/QUOTE]

Tunahitaji post zenye maana za namna hii. Big up Mwanakijiji!! Hoja zako zote huwa zimefikiriwa vizuri, sio za ushabiki tu..!Kwa kweli ifikie wakati wanasiasa wetu waache siasa za kizamani zisizo za kimaendeleo, zisizo kwa ajili ya wananchi na za kupeleka nchi yetu mbele.
Walioko madarakani huwa siku zote wanajisifia tu na kujustify mabaya na mazuri waliyoyafanya bila kuleta suluhu mpya kwa kila kero inayoletwa.
Wapinzani nao on the other hand wamekuwa na tabia ya kusema watu na hiki na kile serikalini bila kutoa mawazo mbadala ya kisera na kidira kwa wananchi kuona njia ya suluhu mpya. Wanaogopa nini? Wanogopa sera zao Zitatumika na walio-madarakani halafu iwe ndio strength yao katika uchaguzi!?
Tujitahidi jamani wananchi na wanasiasa tufanye siasa za maana...tuwachague kwa nguvu ya hoja zenu!
 
Last edited by a moderator:
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined
Jun 24, 2011
Messages
7,609
Likes
1,650
Points
280
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined Jun 24, 2011
7,609 1,650 280
Ninapoiona thread kama hii nafarijika sana, kitu kinachonifariji ni kuwa huwezi kuona pro vyama wanachangia wengi kwa sababu wao wamezoea ule mtindo wao wa kila siku
 
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Messages
10,986
Likes
4,041
Points
280
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2011
10,986 4,041 280
Mwanakijiji kweli inaelekea siku hizi unaelekea kufilisika kimawazo! Yaani kwa mfano mikutano anayohutubia Dr.Slaa huoni tofauti ya sera na mikutano inayohutibiwa na ccm au vyama vingine??Mbali na umati wa watu Slaa akienda kwenye halmashauri yoyote anatembea na vitabu vya halmashauri na kuwaeleza mapato na matumizi ya halmashauri zao na namna wanavonyonywa na chadema ikiingia madarakani itafanyia nini maovu hayo hizo kwako wewe sio sera??chadema kama chama cha upinzani wamekuwa siku zote kwenye mikutano yao wakikosoa sera za ccm na kuonyesha sera mbadala ccm wao wanaishambulia chadema badala ya kueleza wametekeleza kwa asilimia ngapi ahadi zao na ilani yao sasa wewe unaposema huoni tofauti ya sera nakushangaa sana!
Chadema wanahamasisha watu kujitokeza na kutoa maoni kwenye katiba mpya,wanafichua maovu kama wizi kwenye halmashauri, wizi TANESCO na wizi kwa ujumla wa mali za umma , wanaeleza kwa masikitiko elimu inavoporomoka, kilimo kinavoporomoka n.k kweli hayo huyaoni?? UMEFILISIKA MWANAKIJIJI!!
 
N

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2010
Messages
999
Likes
5
Points
135
N

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2010
999 5 135
Value for money:
Huwezi mwansiasa ukatoka DAR hadi Singida kuhutubia watuishirini, ni hasara kwa chama.
Kwa hiyo kwa chama kinachoweza kuwavutia watu wengi kujakusikiliza sera zake kinauwezekano wakupauata wanachama au wafusi wengi.

Kwa hiyo hata CCM wanavyo beba watu kwenye malori wajewasikilize sera zao lengo lao kubwa NI KUPATA WAFUASI NA WANACHAMA KADHAAmiongoni mwa watakaohudhuria.

Idadi ya watusi Ishara ya Kukubalika kwa chama auwanasisiasa husika lakini pia ni kigezo cha ufanisi katika kufikisha ujumbe (sera)zako kwa watu wengi zaidi.

Ijulikane si wote wanaokuja kwenye mikutano hiyo ni wananchamawa vyama husika. Kama wataukuja wengi ni rahisi kupata wananchama miongonimwao.

 
E

Earthmover

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Messages
14,523
Likes
4,343
Points
280
E

Earthmover

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2012
14,523 4,343 280

Kwako mwanakijiji :

mwanakijiji kifupi ccm wameshapoteza mwelekeo sababu ya kushindana na chadema!! Chadema ni chama makini (TAASISI) na kinazidi kukubalika kwa watanzania mfano kizazi kipya....ni ajabu kukuta kijana ni mfuasi wa ccm labda akapimwe akili ingawa katiba inamruhusu!!

Mfano mdogo tu Chadema inatetea raslimali za taifa ziwanufaishe watanzania wote ccm NI MWIKO KWAO.

Kituko cha juzi Arusha CCM inasomba watu toka Monduli na A to Z eti ionekane imejaza mkutano...Chadema wakiitisha mkutano watu nyomi (UMATI) wanakuja bila kusombwa na mabasi wala pilau!!!

Mwanakijiji juzi Lema kaitisha mkutano Arusha ndani ya masaa mawili watu wakajaa...mizani hiii inaonyesha CHADEMA katika medani za kisiasa iko stage ya juu tofauti na CCM bado wanamambo ya kizamani tena kama watoto wadogo kuigiliza....ukiona mtu mzima anaigiliza basi KAISHIWA!!!

Uzi wako mwanakijiji usomeke hivi:
VIONGOZI WAPYA WA CCM WANAZOA MAPESA KWA KIGEZO CHA KUPAMBANA NA CHADEMA (DEMOKRASIA)!!
 
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Messages
10,986
Likes
4,041
Points
280
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2011
10,986 4,041 280
Value for money:
Huwezi mwansiasa ukatoka DAR hadi Singida kuhutubia watuishirini, ni hasara kwa chama.
Kwa hiyo kwa chama kinachoweza kuwavutia watu wengi kujakusikiliza sera zake kinauwezekano wakupauata wanachama au wafusi wengi.

Kwa hiyo hata CCM wanavyo beba watu kwenye malori wajewasikilize sera zao lengo lao kubwa NI KUPATA WAFUASI NA WANACHAMA KADHAAmiongoni mwa watakaohudhuria.

Idadi ya watusi Ishara ya Kukubalika kwa chama auwanasisiasa husika lakini pia ni kigezo cha ufanisi katika kufikisha ujumbe (sera)zako kwa watu wengi zaidi.

Ijulikane si wote wanaokuja kwenye mikutano hiyo ni wananchamawa vyama husika. Kama wataukuja wengi ni rahisi kupata wananchama miongonimwao.
umefafanua vizuri sana mkuu big up commander!
 
babalao 2

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
4,596
Likes
1,582
Points
280
babalao 2

babalao 2

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
4,596 1,582 280
Mimi kwa maoni yangu ni kwamba kuna kila sababu ya kuwa na umati wa kuhutubia kwani kama una mkusanyiko wa watu wengi basi na ujumbe lazima uwafkie watu wengi zaidi na ndiyo utamaduni mzuri wa kujua watu wamehamasika vp. Nadhani utamaduni wa kubeba au kutoa fedha ili watu waje kwa wingi hapo ndipo tatizo lilipo. Pili juu ya kutangaza sera kila chama kinajitangaza kwa mapana yake. Ila tusisahau kuwa kupambana na rushwa na kuipigia kelele kila siku ni vizuri kuliko kuzuia watu wasiongelee UFISADI wakati tunataka mabadiliko. Usipofanikiwa kupunguza UFIDADI KUBADILIKA KIMAENDELEO NI NDOTO TUTABAKI KUSHANGAA MAJIRANI WAKITUPITA KILA LEO.
WATU FURIKENI KWENYE MIKUTANO YA SIASA MPATE KUIJUA SERIKALI YENU INAFANYA NINI KWA MUSTAKABALI WETU TENA TUJAZANE KUPIGA KURA. TUPATE VIONGOZI IMARA.
TANZANIA ADUI YETU NI UFISADI, UVIVU NA WATAALAMU WETU KUTUMIWA KWA MASLAHI YA WACHACHE.
 
POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
6,691
Likes
17
Points
135
POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
6,691 17 135

Kwako mwanakijiji :

mwanakijiji kifupi ccm wameshapoteza mwelekeo sababu ya kushindana na chadema!! Chadema ni chama makini (TAASISI) na kinazidi kukubalika kwa watanzania mfano kizazi kipya....ni ajabu kukuta kijana ni mfuasi wa ccm labda akapimwe akili ingawa katiba inamruhusu!!

Mfano mdogo tu Chadema inatetea raslimali za taifa ziwanufaishe watanzania wote ccm NI MWIKO KWAO.

Kituko cha juzi Arusha CCM inasomba watu toka Monduli na A to Z eti ionekane imejaza mkutano...Chadema wakiitisha mkutano watu nyomi (UMATI) wanakuja bila kusombwa na mabasi wala pilau!!!

Mwanakijiji juzi Lema kaitisha mkutano Arusha ndani ya masaa mawili watu wakajaa...mizani hiii inaonyesha CHADEMA katika medani za kisiasa iko stage ya juu tofauti na CCM bado wanamambo ya kizamani tena kama watoto wadogo kuigiliza....ukiona mtu mzima anaigiliza basi KAISHIWA!!!

Uzi wako mwanakijiji usomeke hivi:
VIONGOZI WAPYA WA CCM WANAZOA MAPESA KWA KIGEZO CHA KUPAMBANA NA CHADEMA (DEMOKRASIA)!!
Nimi nshamwambia atulie andike vitabu yake vya mapenzi, huu mziki wa Chadema hauwezi tena, miaka20 ya chadema anasema haoni sera za chadema ama hoja mbadala kuwa tukiingia madarakani tutafanya nini? so kama haelewi hilo si bora aachane na kutoa michango yake kwenye siasa? anyway anazeeka vibaya
 
Bishanga

Bishanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2008
Messages
15,343
Likes
86
Points
0
Bishanga

Bishanga

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2008
15,343 86 0

Tunawaangalia wanasiasa wetu na kuwasikiliza wanavyozungumza majukwaani na kufurahia jinsi wanavyozungumza kwa ukali, kwa mbwembwe na kwa kuonesha wana uchungu sana. Sasa hili linanoga zaidi kama linafanyika kwenye umati mkubwa basi sauti, mbwembwe na mwamko wa umati unatufanya tulinganishe vyama hivyo hivyo. Sasa utaona CCM na wenyewe wakisimama majukwaani wanazungumza kwa ukali na kwa mbwembwe huku wakishangiliwa - wengi tunakumbuka Mr. Kudadadeki!

Sasa hakuna ubaya kuwa na umati wa watu na wala hakuna ubaya wa watu kuzungumza kwa mbwembwe na kwa jazba. Lakini kuna tatizo kama hatujui kusikiliza hoja zinazotolewa na kushindanishana kwa hoja, kwa sera, kwa mitazamo na kwa maono. Kuna faida gani watu kubishana nani amezaa na nani au nani ni fisadi kama hatusikii tofauti ya sera, mitazamo, maono na mwelekeo wa vyama vyetu vya siasa.

.


Mkuu hapa nilipopaka rangi ya bluu kwa heshima kubwa naomba kutofautiana na wewe.
Mtaji mkuu wa mwanasiasa ni watu kama vile ambavyo mtaji wa benki ni pesa taslim.Vyama vyote duniani (katika nchi zenye mfumo wa demokrasia) vinapotafuta mgombea kati ya vipa umbele vikuu vinavyoangaliwa kwenye sifa za mgombea ni uwezo wa kubwabwaja (rhetoric). Sifa nyingine bila shaka ni ukomavu wa kisiasa,historia ya mchango wake katika chama chake ,haiba,uadilifu,uwezo binafsi wa kufikiri,elimu n.k.
Asikudanganye mtu uwezo wa kumudu jukwaa ni muhimu sana tena sana kwa mwanasiasa. Angalia historia wanasiasa wengi waliofanikiwa kunyaka madaraka (hasa kuanzia enzi za radio/TV) wamekuwa ni mabingwa wa kucheza na jukwaa. Mifano ni mingi Kennedy,Mwalimu Nyerere,Tony Blair,Maathir Mohamed n.k. Kiongozi anayesinzia jukwaani hana nafasi katika siasa za leo. Populism ndo mchezo wenyewe, ahadi kwanza mikakati baadae. Waache kina kina Kinana,Zitto ,Slaa ,Maalim seif na wengineo wavute watu viwanjani,that is the 'in' thing ,na mwisho wa siku hao ndo wapiga kura.Remember Kikwete's crowd 2005? Real politik meeeeeen!!
 
Ng'wamapalala

Ng'wamapalala

JF Gold Member
Joined
Jun 9, 2011
Messages
6,332
Likes
123
Points
145
Ng'wamapalala

Ng'wamapalala

JF Gold Member
Joined Jun 9, 2011
6,332 123 145
MMK naomba ujue kuwa siasa za Tanzania zinaendeshwa kwa itikadi za matukio. Wanasiasa wanaishi kwa polojo za matukio na udaku, Mwanasiasa anaonekana mahili katika jamii pale anapoweza kupata polojo na udaku mapema na kuutoa kwenye mikutano ya kisiasa huku akitaka wananchi wamuone ana machungu na huo udaku, hii kasumba imeikumba pia sekta ya habari Tanzania. Mitandao (blogs) mingi ya watanzania inajaa picha na habari za udaku badala ya habari na makala zenye chambuzi mbali mbali katika maswala yanayoihusu na kuigusa jamii. mitandao michache yenye kudadavua habari na makala mbalimbali inakuwa haipati watu wengi wa kuitembelea kwa sababu jamii inaona kama habari na makala zake ni ndefu na zinachosha kusoma.

Ukilinganisha mikutano yetu ya siasa na ile ya wanasiasa wa nchi za magharibi, utaona tofauti ni kubwa sana.

Kwa sasa Magazeti yenye habari za udaku nchini ndiyo yenye wasomaji wengi ukilinganisha na magazeti mengine ambayo nayo pia hata habari zake huwa zinakuwa ziko nusunusu.

Ni nadra kumuona mtu anasoma kitabu nyumbani au kwenye public transport na hii inaonyesha kuwa tumekuwa taifa la udaku na polojo ndiyo maana wanasiasa wanaona mtaji wa siasa pia ni udaku na polojo tupu.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,033
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,033 280
Niongeze swali la kichokozi; kwenye nchi ambapo kundi kubwa la vijana hawana ajira na wanajishughulisha kwa kubangaiza hapa na pale kuna uwezekano wa mtu kukosa umati wa watu kweli? Ushahidi upo kwenye matamasha mbalimbali, ajali zinapotokea n.k kuweza kukusanya watu wengi mahali pamoja kwenye tukio siyo kigezo cha kukubalikwa kwa sera au hata uwezo wa vyama kuvutia watu - watu wetu hawana la kufanya so ukiwapa cha kufanya au cha kuangalia watakuja tu! Think about it.
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
80,940
Likes
46,580
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
80,940 46,580 280
In politics everything goes...

Hata kampeni za Marekani zilizoisha mambo ya umati yalikuwa 'hoja' wakati mwingine.

Ilipotokea Obama katika moja ya campaign stops zake akashindwa kujaza arena wapo waliofurahia kwa sababu mwaka 2008 kitu kama hicho kilikuwa unthinkable.

Watu wanaongeleaga nywele sembuse kutambiana umati? Usicheze na siasa bana....they don't call it mchezo mchafu for nothing.
 
R

raymg

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2012
Messages
845
Likes
4
Points
35
R

raymg

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2012
845 4 35
Niongeze swali la kichokozi; kwenye nchi ambapo kundi kubwa la vijana hawana ajira na wanajishughulisha kwa kubangaiza hapa na pale kuna uwezekano wa mtu kukosa umati wa watu kweli? Ushahidi upo kwenye matamasha mbalimbali, ajali zinapotokea n.k kuweza kukusanya watu wengi mahali pamoja kwenye tukio siyo kigezo cha kukubalikwa kwa sera au hata uwezo wa vyama kuvutia watu - watu wetu hawana la kufanya so ukiwapa cha kufanya au cha kuangalia watakuja tu! Think about it.[/QUOTE hapa MMJ unapoteza dira kabsa, kwa jinsi nikujuavyo mimi umekua mchambuzi mzuri sana wa mambo ya siasa! Unataka kutuambia umati unaojitokeza kwenye mikutanao ya CDM hawana cha kufanya? Kwa nini wasiende mikutano ya CCM ambako angarau wanapewa chochote? MMJ acha kuleta hoja za kijiwen bwana!
 

Forum statistics

Threads 1,238,176
Members 475,830
Posts 29,312,038