Silinde timiza Ahadi yako ya kufungua matawi ya CHADEMA jimbo la Ileje Mbeya.:!

Mbundumale

Senior Member
Dec 30, 2013
150
0
Wananchi wa jimbo/wilaya ya ILEJE tunasubiria ahadi ya mbunge wa Mbozi Magharibi mh DAVID Ernest Silinde (CHADEMA) kuungana na makamanda wa Ileje kufungua matawi mapya wilaya va Ileje kama ulivyo ahidi tarehe 22/8/2013 mbele ya mwenyekiti wa CHADEMA taifa mheshimiwa Freeman Mbowe na wananchi kwa ujumla.Pamoja na kwamba kuna makamanda machachari kabisa kama Daniel Ezekiel, Gwamaka Mbughi, Emmanuel Msyani, Riziki Mbembela, Cosmas Mwampashi, Victor Msokwa, Mathayo Kibona nk wanaendeleza mapambano kuyaangamiza magamba lakini ni vema ukasaidiana nao ili utimize ahadi yako na pia kama mlezi wa chama Ileje Kama ulivyokabidhiwa ulezi na mwenyekiti wa CHADEMA taifa.


Wananchi wanakusuburi sana kwani uliahidi kufanya hivyo kabla ya bunge la bajeti yaani ndani ya miezi sita.


Mapambano yanaendelea. Karibu sana mheshimiwa David Silunde,mbunge wa Mbozi magharibi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom