Silinde: Ni aibu kwa Halmashauri zetu hadi leo watoto wanakaa chini na wengine hawana madarasa, ni fedheha kwa Serikali

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,777
141,651
Naibu waziri Tamisemi mh David Silinde amesema ni aibu na fedheha kwa halmashauri/serikali hadi leo watoto wanakaa chini na wengine hawana madarasa.

Chanzo: Radio One

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Kwa hiyo anapingana na waliomhifadhi nakumpa unaibu waziri.Ajiulize gari analotembelea ina thamani gani,kwanini mbinu ya yakupata gari ya thamani badala ya shule.
Angekuwa nje ya mfumo angeeleweka.
 
Naibu waziri Tamisemi mh David Silinde amesema ni aibu na fedheha kwa halmashauri/serikali hadi leo watoto wanakaa chini na wengine hawana madarasa.

Source: Radio One

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Anailaumuje serikali wakati yeye ni sehemu ya serikali hio hio? Atengeneze madawati, badala ya kulalamika. Atafute suluhisho. Naona bado akili yake iko upinzani, ingawa mwili uko CCM.
 
Naibu waziri Tamisemi mh David Silinde amesema ni aibu na fedheha kwa halmashauri/serikali hadi leo watoto wanakaa chini na wengine hawana madarasa.

Source: Radio One

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Kwa Sasa tumewekeza kudhibiti kongamano la katiba mpya, mengine yasubiri kwanza kwani hao ndio wanaotuchelewesha kupata madawati.
 
Maendeleo ya nchi ni wananchi kuwa na uwezo wa kipato kinachoweza kuchangia shughuli za kijamii hata pale ambapo serikali imechelewa.
Fikra potofu za viongozi wengi wa nchi masikini kuwafukarisha wananchi kwa kodi kubwa badala ya kuwawezesha kiuchumi kabla ya kodi.
Ili kupata utajiri lazima ukusanye zaidi kutoka nje na utoe kidogo.
Ni lazima serikali itazame sera ya kuwezesha sector binafsi (wazawa) kusaidia kupambana zaidi nje na ndani ya nchi.
 
Kwa Sasa tumewekeza kudhibiti kongamano la katiba mpya, mengine yasubiri kwanza kwani hao ndio wanaotuchelewesha kupata madawati.
Umeona eeh. Mbowe na wenzake wametuchelewesha sana yaani. 😀 😀 😀 😀
 
Anailaumuje serikali wakati yeye ni sehemu ya serikali hio hio? Atengeneze madawati, badala ya kulalamika. Atafute suluhisho. Naona bado akili yake iko upinzani, ingawa mwili uko CCM.
Umeona eeh. Mbowe na wenzake wametuchelewesha sana yaani. 😀 😀 😀 😀
Huo ni kwa mujibu wa wanaotua akili geti la mtaa wa kijani.
 
Huo ni kwa mujibu wa wanaotua akili geti la mtaa wa kijani.
Kabisa. Kwa sasa wamejaa wao bungeni, wamepitisha takataka nyingi sana, ngoja tuone Tanzania ikifikia uchumi nchi zilizoendelea kama Sweden, Marekani, Japan nk
 
Back
Top Bottom