Silinde, mkosamali wametupa funzo kubwa wasomi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Silinde, mkosamali wametupa funzo kubwa wasomi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by jambo1, Dec 3, 2010.

 1. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  SILINDE, MKOSAMALI WAMETUPA FUNZO KUBWA WASOMI
  Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni ambao mchakato wake ulitawaliwa na vituko kibao tangu mchakato wa kura za maoni mpaka uchaguzi mkuu umeacha somo kubwa sana kwa wasomi wa vyuo vikuu.
  Katika uchaguzi huu tumeona kuwa vijana wasomi wakijitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za kiungozi kupitia vyama mbalimbali, ni haki ya kila mtu kuwa mfuasi au mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo kundi la kwanza la wasomi ni waliolelewa kwenye mifumo ya kifisadi hawa walitupa karata zao kupitia chama tawala CCM, kundi la pili ni vijana wanaoishi maisha ya kuganga njaa wao waliamua kwa dhati kujitoa mhanga kupitia vyama vya upinzani kama vile CUF,NCCR, Chadema nk,
  Kwa kifupi nitajaribu kuyaangalia makundi haya yote ya wasomi na ushiriki wao katika uchaguzi.
  Kundi la kwanza la wasomi waliojitosa kupitia chama tawala hawa waliishi kwa fikra na kuamini kuwa ni kupitia CCM pekee mtu anaweza kupata nafasi ya uongozi kiulaini, ukiangalia historia ya hawa waliishi katika maisha hayo, wakati mwingine iliwalazimu kuwasaliti wenzao vyuoni au kuingia kwenye serikali za wanafunzi si kwa lengo la kutetea maslahi ya wanafunzi bali kwa lengo la kujitafutia umaarufu na kuzima harakati za kuwapigania wanafunzi hasa wanapokuwa na matatizo, katika hili mifano ipo mingi mno. Hivyo kuingia kwao kwenye kinyangÂ’anyiro kulitokana na matendo yao waliyoyafanya ya kuwakacha wanafunzi wenzao na kuwabeba watawala wakidhani eti kwa kile walichokifanya wanaweza kukumbukwa na kupewa nafasi. Kilichotokea wenyewe wanakijua walitupwa nje mapema kwenye mchakato wakura za maoni.,kama tunavyojua kura za maoni za CCM mwaka huu ziligubikwa na rushwa na hili hata katibu mkuu wa CCM alithibitisha kwa kusema walizidiana viwango vya rushwa.,Hivyo wasomi hawa hawakuwa na dau la kuwapa wanachama kama rushwa ili wawachague hivyo mabwanyenye walewale walipata nafasi huku wale wanaojiita wasomi waliodhani watapata nafasi wakabwagwa. Na walivuna walichopanda.
  Kundi la Pili la wasomi walijitosa kupitia vyama vya Upinzani, hawa ukifuatilia historia yao wengi waliishi katika maisha ya kuwapigania wanyonge na fikra zao zilikuwa kuwa mabadiliko yanawezekana kupitia chama chochote ili mradi tu kiwe na malengo na mtazamo madhubuti wa kuwakomboa watanzania. Hivyo bila kujali kushindwa au la walijitosa na kushinda katika mchakato wa kura za maoni, wengi wa wasomi hawa waliibuka na ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu.Mifano ni Mh Silinde David Mbunge wa Mbozi Magharibi-Chadema na Mh Felix Mkosamali Mbunge wa jimbo la Muhambwe-NCCR, pia wapo ambao kutokana na mifumo mibovu ya kiuchaguzi kura zao zilichakachuliwa. Kwa wale wanaoijua historia ya Mh Silinde amemaliza katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka huu na daima aliishi maisha ya kuwapigania wanjonge na katika hili wasomi wa UDSM wanalitambua na mchango wake wanaukumbuka na utabaki kuwa historia kwani aliongoza mapambano dhidi ya mfumo mbovu na wa kibaguzi wa utoaji wa mikopo ya elimu ya juu. Hivyo basi Silinde aliamini kuwa mabadiliko yanawezekana kupitia vyama vya upinzani kwani ndio vyenye nia dhabiti ya kuwakomboa watanzania.
  Hivyo kwa tukio hili ni dhahiri kwamba si kweli na ni fikra zilizokufa kwa wasomi kuendelea kujipendekeza kwa chama tawala kwa ajili ya kuganga njaa na kuwa na matumaini ya kupata nafasi ya uongozi na ni rahisi na wala haiitaji nguvu ya kifedha kupata uongozi kupitia vyama vya upinzani kwani mchakato wa kura za maoni huwa ni wenye uwazi mkubwa na wananchi wenyewe huamua nani mwenye uwezo binafsi wa kiuongozi.
  Watanzania wa leo wameamka na wako tayari kujitoa kwa kadri ya uwezo wao kufanikisha mabadiliko, Mfano wasomi hawa waliojitosa kupitia vyama vya upinzani walichangiwa na wananchi shilingi 100/=, 200/=, 300/= wengine walipewa magari,mafuta nk, kuwawezesha kumudu gharama za kampeni. Kigezo cha kuwa tajiri au kuwa CCM kwa sasa hakina nafasi miongoni mwa watanzania. Ushindi walioupata kina Silinde David, Felix Mkosamali, Boniface Jacob-Diwani Ubungo Chadema, Adam Chagulani-Diwani Igoma Chadema nk, uwe ni funzo kwa wasomi waganga njaa na wenye matarajio ya kupata nafasi za uongozi kupitia CCM, kwani dalili za awali zinaonesha hata ndani ya baadhi vyama vya wanafunzi vyuoni kuna viongozi ambao wameingia kwa ajili ya kuibeba serikali na wapo walioingia kwa kushawishiwa kwa lengo la kuzima harakati za kutafuta haki na kukandamiza matakwa ya wengi,hili halina nafasi kwani itafika siku wasomi wakichoka hawategemea tene uongozi watasimama na kupaza sauti zao wakidai haki zao.,matatizo kama ya mikopo kwa wanafunzi, vyumba vya malazi(hostel) yamenzakushika hatamu na kuonyesha dalili mbaya huku viongozi wa hizo serikali za wanafunzi wapo kimya.
  Pia tukio la hivi majuzi la wanaojiita wasomi wa CCM kutoka vyuo vikuu vya Dodoma kugeuka kuwa wasemaji wa CCM na kutoa tamko la kulaani kitendo cha kidemokrasia kilichofanywa na wabunge wa Chadema cha kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati Rais Kikwete akihutubia, hili linatuonyesha aina ileile ya wasomi uchwara ambao kwao kujikomba ndani ya CCM ni kama mtaji wa kisiasa bila ya kujali maslahi ya umma. Haiingii akilini kwa mtu anayejiita ya msomi asiweze kuelewa msingi wa madai ya Chadema juu ya katiba inayokibeba chama tawala. Ukifuatilia kwa makini hili utagundua kuwa hawa ni wasomi walewale uchwara ambao baadaye huja kukumbwa na kimbunga cha kisiasa. Wasomi wa namna hii hawana nafasi kwa sasa katika jamii na daima watapata aibu kubwa pindi wakinyemelea nafasi yeyote ya uwakilishi.Wasomi wa ina hii ambao wamegeuka kuwa wasemaji wa CCM daima husimama kidete na mstari wa mbele kuminya haki za wengine vyuoni na kwamwe hawako tayari kukosoa serikali na kupigania haki za wanyonge.
  Vitendo vya usaliti miongoni mwa wasomi kwa matarajio ya manufaa hasa kutoka kwa watawala havina nafasi kwa sasa.
  Tusubiri tuone tuendako.
  Mwandishi wa makala hii ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anasoma Shahada ya Sayansi ya Komputa.
  jjarache@yahoo.com
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,839
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Umenena
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ni kwali kabisa mkuu!
   
 4. n

  ngoko JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ilitia mashaka makubwa kuona watu wanatoa tamko kwa niaba ya wasomi wa vyuo vikuu ya Dodoma. baadaye nikakumbuka walikuwa wahusika wa kutembeza form za mgombea wa sisiem. Mbali na hilo sikuona tamko la kupingana na hao vijana , most likely lilikuwa tamko hilo lilikuwa mtazamo halisi wa wasomi wetu wa Dodoma.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ndefu sana lakini safi
   
 6. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Nampongeza sana SILINDE kwa kuwa mpiganaji wa kweli toka alipokuwa pale UDSM alikua ni mtu mwenye msimamo wa kutetea maamuzi yake hadi dakika ya mwisho licha ya vikwazo vya mafisadi hukuwa mtu mwenye kubadilisha msimamo wake.

  Pole yake Julius Mtatilo aliyeingia CHOO CHA KIKE (CUF) atakuwa anamuaangalia mwenzie (SILINDE) kwenye luninga tu na kubakia kusema tulisoma naye huyu.
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Heko vijana
   
 8. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ukitaka kumficha mtanzania kitu kizuri, basi kiweke kwenye maandishi.
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo ndo jamaa kaamua kuandika article ndefu hivyo?
   
 10. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  I salute you guys..
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  hahahah

  mwandishi kasahau kuweka aya... ndo maana imekuwa ndefu... ila iko poa..
   
 12. LivingBody

  LivingBody Senior Member

  #12
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hakika Watanzania ni wazembe wa kujisomea,, jamaa kajitahiti kuelezea ila watu mnasema ndefu.
  kweli ukitaka kumficha Mtanzania kitu, weka kwenye maandishi. hahaha:teeth:
   
 13. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru wote kwa mawazo yenu...!
  Ni ndefu kweli inaweza kuwachosha ....lakini naamini ujumbe umefika....!
   
 14. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  gud article, kama kweli we unauchungu na nchi hii unapofanya siasa unapaswa ujiangalie unaendesha harakati zako ukiwa wapi? yaani unatetea wanyonge eti uko chama kimoja na R.A, A.C na E.L, wasomi jiangalieni.
   
 15. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Iko poa sana.
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Unajua kuchanganua hoja. Ahsante.
   
 17. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Silinde kweli ni mpiganaji wa ukweli maana amewahi kufukuzwa hata chuo
   
 18. A

  ANDREW MBEGETE New Member

  #18
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu we kiboko,yote ni kweli kabisaaaaaaa
   
 19. Cassava

  Cassava JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 282
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  Font size inatisha, siku nyingine mumbuke mwalimu wako wa mwandiko hata kama ujumbe wako umefika.
   
Loading...