Silaha za Masafa Marefu Zinazomilikiwa na JWTZ

unachotafuta utakipata muda si mrefu
Nin wasiwasi sana na silaha za masafa marefu tulizo nazo ndani ya majeshi yetu ya ulinzi. Miaka ya 2000 kuna zile zilizokuwa zinalipuka zenyewe kule Mbagala. Na ninavyokumbuka Tanzania tuliwahi kununua vifaru vingi na Gun Howitzers nyingi sana wakati wa utawala wa Nyerere kutokea Urusi. Silaha zile ndizo kwa kiasi kikubwa sana zinazotumika sasa hivi vitani huko Ukraine.

Urusi inazitumia na Ukraine pia inazitumia. Jambo linalojitokeza ni kuwa mizinga inayotumika katika Howitzers na vifaru hivyo haipatikani tena. Urusi haizitengenezi tena, na Ukraine imekusanya mizinga karibu yote iliyokuwa kwenye nchi za Warsaw pact na haitoshi kwani mizinga mingine imekuwa hailipuki; hiyo imetokea kwenye pande zote mbili za magogoro huo.

Sijaona Tanzania ikitupa vifaru vya zamani na kuleta vipya, na sijui kama Tanzania itapata tena mzinga ya kutumia kwenye vifaru hivyo kama siyo vya shoo tu. Vifaru kama hivyo leo hii vimekuwa scrap zilizosambaa kwenye ardhi ya ukraine.

Ninajua kuwa zamani shirika la Mzinga liliundwa ili kuwa linatengeza mizinga hiyo, ila sasa baada ya kutokuwa na matumizi ya mizinga hiyo kwa muda mrefu sijui tuko wapi. Ila vita hii ya Ukraine tuichukulie kama funzo kuwa utegemezi wa silaha za urusi siyo jawabu la usalama na ulinzi wetu tena. Urusi imeshapitwa na wakati sana kwenye teknolojia ya vita.

View attachment 2219644View attachment 2219645View attachment 2219646
Unachokitafuta utakipata muda si mrefu
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom