Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,769
Mapema mwaka huu Raisi Putin wa Russia alitamba kwamba sasa Urusi ina silaha (missile) ambayo inaweza kupiga sehemu yeyote duniani. Ukweli ni kwamba wakati Putin akifanya majigambo haya, silaha hiyo ilikuwa bado inatengenezwa na mainjinia wa Urusi.
Silaha hiyo imetengenezwa kwa namna ambayo inapopigwa inaanza kuendeshwa kwa kutumia mafuta ya petroli, na baadaye inaendeshwa kwa nguvu za nyuklia.
Wanasiasa wa Kremlin wa Urusi walilazimisha mainjinia waanze kufanya majaribio ya siala hiyo ili kuonyesha ulimwengu nguvu za kijeshi za Urusi. Japo mainjinia walisema walihitaji muda zaidi ili kuikamilisha silaha hiyo, waliambiwa lazima wafanye majaribio sasa. Walipofanya majaribio silaha hiyo ilifeli kwa kuwa ilifanikiwa kwenda kilometa 35 tu kabla ya kulipuka na kuanguka chini. Mara nyingine ilienda kama kilomita 8 na kufeli.
Hili limekuwa jambo la kufedhehesha kwa Urusi.
Sasa wanamazingira wanakuja juu kuuliza ikiwa silaha hizo zilifeli na kulipuka sehemu ambazo hazikuwa zimepangwa kulipuka, ni nini athari za mionzi ya nyuklia sehemu zilipoangukia?
Source: MSN
Putin claimed a new nuclear missile had unlimited range – but it flew only 22 miles in its most successful test yet