Sikutegemea kama nitakuja kumpiga mke wangu hata siku moja, lakini jana nimelazimika kufanya hivyo

Nadhan badala ya kumpiga, alipokuonesha chakula kwa mguu ungeeweka vifurushi vyako ukatoka ukaenda kula nje ukirudi unafanya shughuri zako au unalala huku ukiendelea na uchinguzi.
Kama walivyosema wadau hapo juu kuna mambo matatu
1 - hili ni lakawaida huwa wanamtindo wa kuwapima wanaume
2- ni tabia yake mbaya aliificha so now anaaza kuionesha
3- kuna mtu anampa jeuri( kikombe hiki kikuepuke) . katika uchunguzi wako anza na huko kwa jirani alikokimbilia. Angalia ni mtu wa kariba gani na familia yake ikoje na maisha kwa ujumla.
Bwana akupe subira na uvumilivu katika kipindi hiki
 
sijui nikagongee nyagi!
kaliwa huyo na mtu ambaye ni mtamu balaa kwake

Huyo anayechati naye ndio amekula mzigo, sasa hivi jamaa (mumewe) anamuona kama beberu . Jiandae kwa mengi zaidi wanawake ndivyo walivyo. Pole sana lakini, mie nakupongeza kwa hayo makofi.
Wanawake sijui wanashida gani, sijui inakuwa inatokana na vile wanaume tunaishi nao au kuna kitu sijakifahamu bado. Kuna mzee wangu( Baba yangu mkubwa) majuzi kati nilimpihia tukawa tunazungumza mawili matatu. Baadae akaanza kulalamikia mkewe kuwa kabadilika sana, inafika kipindi kupika pale nyumbani ni ile mpaka ajisikie. Na zaidi anapika mchana tu usiku hapiki na sio kwamba hakuna chakula au hela hakuna ila ni kiburi tu kimemiaa na hii imekuja baada ya mzee kupata mdororo kidogo kwenye miradi yake ambayo mwanzo ilikuwa inamlipa vizuri mpaka wakajenga nyumba mbili na akamfungulia na biashara huyo mama. Sasa biashara yake mama ndio inampa mpa vichenji vya mahitaji yake muhimu. Ndio hivyo mzee analalamika kinoma, mwanamke full kiburi na mengineyo.
So ikifika hapo yaani mimi suala la kuoa kabisa naliogopa maana hawa viumbe wanatuweka kwenye majaribu kuharibu mili yao kwa vipigo ambacho si kitu chema na salama.
 
kyanyangwe, Inamaana unajilaumu kwa ulichofanya!?

Huo ndiyo UANAUME sasa, wala hujakosea hata kidogo.

Nakuhakikishia, kama usingempiga ipo siku yangetokea zaidi ya hayo. Acha kuapa kabisa aisee!
Hapo umeokoa mambo mengi sana.

Hatua aliyokuwa amefika ni mbaya sana katika mahusiano ya mapenzi.
Mwanamke huanza tabia kwa process.

Mimi hata akiwa Girl Friend wangu tu, akifanya hivyo lazima achezee vitasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kyanyangwe,
Mkuu, kwanza bado uliyekosea ni wewe. Maana huwezi kujiwekea principle alafu ukasema unaivunja. Iko hivi, ukiona dharau ya namna hiyo usikimbilie kupiga. Jitafakari inatokana na nini. Angalia hasa mambo ya fedha kama huduma ziko vizuri, kitandani nk. Kama hujaangalia hayo, leo kaomba msamaha, kuna muda atarudia, ukimpiga anaenda kwa yule anayempatia huduma. Huwajui hawa!!
 
Sababu ndogo sana hizo, kukupokea mzigo sio issue kivile na haina mantiki yoyote zaidi ya ukoloni tu, umetoka na mzigo umbali mrefu umevumilia afu ukasirike kutokupokewa tu?? Kwani hujui mahali pa kuweka huo mzigo??, kosa la pili ndo la kijinga zaidi, Yani unauliza chakula kipo wapi nyumbani kwako!!! Hujui jiko au meza ilipo?? Be a gentleman Bro... Jifunze kujihudumia unapokua nyumbani, mana hata yeye siku akija na mzigo akukute unachati hutafanya kama unavyotaka akufanyie... Tusiwatumikishe kama watumwa wake zetu, kwa kisingizio cha majukumu yao. Sometimes our demands is full of shit
 
Back
Top Bottom