Sikutegemea kama nitakuja kumpiga mke wangu hata siku moja, lakini jana nimelazimika kufanya hivyo

kyanyangwe

Member
Oct 31, 2018
77
150
Habari watu wa humu,

Ebwana ndugu zangu katika haya maisha mtu unaweza ukawa umejiwekea principles zako zitakazokuwa kama mwongozo wa maisha yako but ikatokea siku moja ukaenda kinyume na matarajio.

Binafsi nilishajiwekea katika maisha yangu sitokaa nimpige mke wangu hata kofi, lakini kwa hali iliyotokea jana nimejikuta namkung'uta ipasavyo.

Nimetoka kwenye mizunguko yangu nimechoka, nikamkuta kajilaza kwenye kochi huku anachat na simu yake tu.

Nimeingia na mizigo ndani hata kunipokea hakuna, kilichoniudhi zaidi nikamuuliza chakula kiko wapi akanionyeshea kwa kutumia mguu eti kile pale nijipakulie mwenyewe.

Jamani nikapandwa na hasira za ghafla, maana nilitafsiri ile kama dharau. Nikamshika nikamtandika makofi mawili kwanza, nikaona bado analeta kimdomo mdomo asee nilimpiga hatari.

Nikaona kakimbilia kwa jirani, baadae usiku jirani kamleta kutusuluhisha, yakaisha. Asubuhi kumekucha hakuna anayemsemesha mwenzie. Ila muda huu ameni-text kuniomba msamaha kwa yaliyotokea jana na amekiri makosa yake na hatarudia tena.

Sasa hapa natafakari, ni shetani gani alimuingia jana mpaka akaamua kuniletea dharau kiasi kile.
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,021
2,000
Ilimradi amejirudi na kuomba msamaha, basi msamehe na ujifanye kama hayo ni mapito. Ila muweke tu wazi kua aliofanya jana kwako yalikukwaza na ukayapokea kama dharau (ili ajue yalikukwaza sana).

Halafu weka maneno ya akiba, hauwezijua pengine na wewe utamkosea huko mbeleni na utahitaji msamaha wake pia.

Katika ndoa au wapendanao ugomvi hua kaukwepeki, hua upo tu.
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,241
2,000
Sasa huyo ni Mke wako au house girl wako? Akupokee na kukupa chakula kwani wewe ni mtoto wake?Huyo Mwanamke unataka alee watoto wangapi sasa kama na wewe ni mtoto pia?
Mimi nafikiri kuna baadhi ya Wanaume hata maana ya Ndoa hawaielewi, wanakurupuka tu.
 

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
16,520
2,000
I hate violence....

I always stay far away from the violence...

Better be alone but peacefully rather with partner but grieving...

Its better to have nothing and hold peace of mind rather than own names and things with majeraha....

Growing Old Peacefully, Silently.

Granny Matata.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom