Sikutegemea kama ingetokea siku na mimi nijihisi nimeambukizwa UKIMWI... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikutegemea kama ingetokea siku na mimi nijihisi nimeambukizwa UKIMWI...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by queenkami, May 25, 2012.

 1. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hello Wapendwa.

  Kuna mahala fulani huwa ninasafiri kwenda mara kwa mara kufuatilia mambo ya kibiashara.Huko mahala ninaposafiri huwa kuna mama yangu mkubwa anaishi huko lakini siku zote huwa nashukia hotelini.Kila nikifika huwa nampigia simu mama mkubwa na pia najitahidi kwenda nyumbani kwake kumsalimia lakini mama mkubwa analalamika kuwa ni vizuri siku nikiwa huko japo siku moja moja nilale nyumbani kwake.

  Mama yangu mkubwa nimuathirika wa UKIMWI,sio kwa kumuhisi bali kwa kinywa chake alimweleza mama yangu,pia hataki kutumia hizi dawa za kurefusha maisha hivyo amekonda sana na ana mapele na vidonda na majipu vinamtokea kila mara.

  Siku moja nikiwa huko nikaamua kwenda kulala nyumbani kwa mama mkubwa wangu japo ana chumba kimoja,nilipofika nikakuta kidole chake kimoja cha mkononi kimeoza kwa kidonda chenye usaha,mwenyewe akanambia eti kuna mdudu akiingia kwenye kucha kidole ndo kinakua hivyo.

  Tulikula kisha tukapiga story hadi usiku mwingi kisha sababu alikua ana magodoro mawili nikamwomba anitandikie godoro mim nilale chini.

  Wakati anatandika shuka kwenye hilo godoro kwa bahati mbaya kile kidole chake chenye kidonda kikanichoma mguuni hadi pakakatika hadi damu ikanitoka halafu ule usaha wake ukabakia juu ya hapo aliponikata na kucha yake.Niliogopa sana,cha ajabu yeye hata hakuonesha mshituko,ila mimi niliogopa hadi sikuweza hata kupata usingizi.Kesho yangu nikarudi hotelini kwangu nikiwa na mawazo ya kuwa labda virusi vimenipata.Nilimaliza shughuli zangu huko nikasafiri kurudi nilipotoka lakini wiki mbili tokea aliponikata na kucha nilikuwa na mawazo sana lakini baadae nikasahau.

  Kwa kawaida mimi ni mtu mwenye kinga imara,ni kwa miaka mingi sijawahi kuumwa kitu chochote zaidi ya mafua,tena hata mafua yenyewe sio mara kwa mara.Kama baada ya mwezi na nusu hivi tokea nilipokatwa na kucha nikapata mafua makali yaliyoambatana na homa kali na maumivu ya kichwa,nikaanza tena kukumbuka lile tukio,nikaanza kuhisi labda nimeshaathirika,wakati mwingine najipa moyo kuwa ni mafua ya kawaida maana hata kama kuathirika inaweza kuchukua hata miaka mingi bila kuona dalili.

  Miezi michache baadae nikasafiri kwenda Ulaya,wiki moja tu tokea nifike nikaanza kupiga chafya mfululizo halafu pua ilikua inawasha ajabu hadi ikawa nyekundu na jicho moja likawa linatoa machozi hasa nikiwa nje natembea,mawazo tena ya kukatwa na kucha yakarudi kwa kasi,safari hii nikawa sina uhakika kabisa kuwa mimi ni muathirika au la maana tokea nizaliwe sijawahi kupatwa na hali kama hii,baada ya kupiga chafya kila dakika kwa wiki nzima mfululizo nikaamua kwenda hospitali,nikaambiwa nina allergy ya polen,daktari akasema kwa vile kilikua kipindi cha summer hewa imechafuka kwa polen inayotokana na maua yaliyopo kila mahala,ila nikashangaa maana home kwangu nina maua ya kila aina na sijawahi kupata hiyo hali,rohoni nikazidi kuogopa kuwa huenda nimeathirika kwa kukatwa na kucha.

  Siku nyingine tena ghafla nikaanza kuwashwa na kuvimba mwili,yaani bila kujua sababu nilikuwa nawashwa kuanzia utosini hadi kwenye unyayo halafu nikiamka ngozi imevimba na kuwa nyekundu,kwenda hospitali nikambiwa eti kuna matunda nilikula ambayo nina allergy nayo,kweli kuna vitunda fulani nilikula,lakini nilizidi kuogopa kuwa haya mauza uza labda yanatokana na kukatwa na lile kucha.

  Siku nyingine tena nikala viazi na samaki halafu usiku nikaamka tumbo likawa linaniuma sana kisha nikaanza kuendesha,kila dakila nikawa naenda chooni kwa siku mbili kisha likapoa.

  Nikaona kukata mzizi wa fitina acha nikapime,kabla ya kukatwa na kucha nilikua nina uhakika kuwa sina ukimwi,niliamini kama mtu hujawahi kusex,wala kuongezewa damu,sindano nilichomwa nikiwa mtoto,wala sishirikiani na mtu vitu vya kukata hivyo chance ya kuwa na UKIMWI ni ndogo.

  Kabla ya kwenda kupima nilisali nikamuomba Mungu kuwa kama kuna kirusi chochote kilichojipenyeza mwilini mwangu siku ile nilipokatwa na kucha la muathirika kife kwa jina lake lenye nguvu kupita majina yote.
  Majibu yangu yakaja kuwa mim sio muathirika.

  Nilichojifunza ni kuwa ukiruhusu ubongo wako uamini unaumwa kweli utakuletea vimagonjwa vya ajabu ajabu kusuport imani yako maana kipindi nilichokua naogopa nilipatwa hadi na vichomi ila nilipoambiwa sina UKIMWI hata sikujua vilipotelea wapi.
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  dahh pole sana my dear hakuna raha duniani kama kujua status yako....
  mimi siku niliyoamua kupima na kupata majibu yangu nilijiona kama nimezaliwa upyaaaa......sirudi tena dhambini
  stigma ya hiv ni mbaya unaweza kufa bureeeeeeeeee
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Dah queenkami pole sana ..
  Mie nakumbuka rafiki yangu alikuwa anaumwa sana ila hakunambia nini kinamsumbua ingawa siku zote alinihakikishia ana vidonda vya tumbo..
  Kwa sababu nilikuwa naamini ni rafiki yangu mpenzi na ni mtu niliyemwamini siku zote,..
  Nilikuwa namuuguza kila anapoumwa ..kuna kipindi alikuwa anafikia hali ya kutokuweza kuamka kitandani namuogesha na kumlisha..
  Nilipatwa Presha siku Dr aliponiuliza madame hivi huyu Best friend wako ukimuogesha huwa unatumia Gloves
  Nikamuuliza Why ndo akanifungia ofisini kwake na kunipa habari kamili..
  Mwili ulinyong'onyea
  Jasho lilianza kunitoka
  Na kuhisi kizunguzungu..
  Nilikuwa na hali ngumu sana....
  Ila mungu ni mwema siku zote..
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,221
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Duh. . .poleni sana Mama wa kwanza na QK. . .
  Watu wengine hua wakishaupata hawajali ikiwa wataambukiza wengine au la. Pengine mama mdogo wa QK alimkata kwa makusudi kabisa.
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  huu ugonjwa huu unaweza upata hvhv .... umekaa pabaya kwanza,just imagine una ndoa ,umetulia mwenzako je?
   
 6. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,849
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Acha uoga, hata kama ingekutwa nao sio mwisho wa maosha hivyo jifunze kuwa jasiri na acha imani potovu kuwa, mtu mwenye ukimwi ukiwa naye karibu atakuambukiza ukimwi.
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 41,972
  Likes Received: 9,820
  Trophy Points: 280
  pole sana! hongera kujua afya yako.
   
 8. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  hahaa Smile wee acha tu
  yaani ukiwa hujui status yako ukisikia watu wanaongelea UKIMWI unakua mnyongee.
  Sasa hivi najua maana ya ule msemo wa "unaringa umepima?" lol
  Kwa kweli ninafuraha kujua kuwa Mungu alinipigania sababu uwezakano wa kuambukizwa ulikuwepo.
  MUNGU NI MWEMA SANA.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Inatishaa. Unaweza kufa kwa BP
   
 10. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  FirstLady1 hakika Mungu ni mwema kweli.
  Ukisema hali ngumu nakuelewa maana nimepitia hapo mahala.
  Pole sana mama wa kwanza.
  Shoga yako hata kama hakutaka kukwambia angekuomba tu uvae gloves ila watu wengine hawajali wenzao mwaya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ndo hapo,ndo maana unaposikia mtu ana huu ugonjwa tusikimbilie kuona kuwa walikua m..laya ndo wakapata.
  Chukulia mfano wangu mimi na wa FirstLady1 si ndo kufa bila hatia huko.
  Mungu tusaidie hii inaweza mpata yeyote katika mazingira yeyote.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  mungu ni mwema always...tuzidi tu kuombeana bado safari ndefu my dear
   
 13. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni kweli woga sio mzuri ila ukweli ni kwamba niliogopa na nilishindwa kujizuia kutokua na hofu.
  Pili najua kula au kushikana na mtu mwenye ukimwi hakuleti maambukizi ila issue yangu ni zaidi ya kuwa karibu na mtu mwenye ukimwi.
  kama umesoma yote nadhani utanielewa.
  Pia kujifunza ujasiri wa kuishi na ukimwi sio lelemama ndio maana watu wanapewa ushauri nasaha,ukimwi unatisha ndugu yangu maisha yenyewe ndio kwanza tunayaanza.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  yaani Smile nilipopata jibu la Dr ilibidi kwanza nimwambie na baba watoto hali halisi
  Ila ndo maana nasema kweli mungu ashukuliwe siku zote
   
 15. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  Queenkami, hili ni somo zuri sana kwa jamii! ila rudia kupima kila miezi mitatu, ili kuwa na uhakika.
   
 16. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 5,394
  Likes Received: 4,875
  Trophy Points: 280
  Dah, ama kweli, UKIkuingia MWIlini unatisha...!!!
   
 17. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Asante Lizzy.
  umeongea kama mama yangu alivyoongea,
  nilijaribu sana kumshawishi kuwa ni bahati mbaya lakini haamini.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,134
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Hivi wanapimia wapi?

  Siwezi pima labda niko kwenye machela, na huu u-stiker wa Drogba?

  Pimeni tu nyie lol
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,382
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Lizzy asante sana
  sijui wanadamu tumeumbwa vip ...
   
 20. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  acheni tu wakuu,
  yaani baada ya majibu najiona kama bilionea jinsi nilivyo na furaha wakati yapo mengi yakuhofia pia kama cancer na mengine mengi.
   
Loading...