Sikuruhusiwa kukagua Daftari la Maslahi na Rasilimali la Paul Makonda

Mkuu mdogo wangu Abdul Nondo, kwanza habari za siku?.
Pili bila kuingilia, your right to information, taarifa ya mali za viongozi, inalindwa na haki za the right to privacy, hivyo ili mwananchi uruhusiwe kukagua mali za kiongozi yoyote, maombi yako yaliza yaambatane na the the motive behind ya wewe kuzitaka taarifa confidential za mtu.
Ili kuwa fare kwa Makonda, you should have shown unazitafuta taarifa hizo in good faith just for the quest for info, tena ungepaswa, kuonyesha charity begins at home, kwa kukagua kwanza mali za viongozi wako wa chama, kisha uende kwa viongozi wa kitaifa, national level, ndipo uje regional level.

Kitendo cha kutaka kumchunguza Makonda tuu, sio kumtendea haki.
Sasa kwa kukusaidia wewe na wengine ambao hamjui source ya utajiri wa Makonda, karibu mitaa hii HAPA!.

Kama hoja yangu hiyo ya source ya utajiri wa Makonda ni bonafide genuine, nakushauri, achana na Makonda na yasiyokuhusu, fuatilia viongozi wako.
Ni ushauri tuu!.
P
Sheria na kanuni ya Maadili ya viongozi wa Umma , inataja kiongozi wa Umma na Raia yeyote ana jukumu la kukagua mali ya kiongozi huyo wa umma .

Zitto au viongozi wa chama sio viongozi wa Umma kulingana na sheria za nchi . Ila Zitto Kabwe akiwa Mbunge aliwasilisha tamko la mali zake na wewe ni Shahid kwani kuna thread yake humu.

Kwa mujibu wa kanuni za maadili ya viongozi wa umma za Na.168 kifungu cha 6 na 7 kinanipa hayo mamlaka pamoja na masharti yake,mimi kama raia kukagua daftari la rasilimali na madeni.

Kifungu cha 6 (1)(a) kinasema " mtu huyo awe amemplelekea Kamishna malalamika dhidi ya kiongozi wa umma" ,nilipeleka malalamiko yangu tarehe 17/Oktoba /2019 yakiwa na hoja za kueleweka na ushahidi.

Nchi zingine taarifa za mali za mtumishi wa umma sio siri na wala sio lazima uombe yaani unapata na nchi zingine taarifa zipo mtandaoni . Hayo mambo unayo tetea kaka Mayalla ni kuchochea Ufisadi na upigaji , Uwazi ndio kila kitu katika mapambano ya Rushwa na ufisadi na wala sio suala la faragha sijui confidentiality , Usiri sio kwa mali zinazomilikiwa na mtumishi wa ummma kama hutaki kuweka wazi acha kazi ya utumishi wa umma.
 
Nondo ana kichwa kizima sana.makala nzuri sana ila imepoteza hamasa kisiasa kwasab imekuja too late.Laiti NONDO angekuwa jasiri wa kuanika makala hii hadharan wakati ule, Nondo angepata fans wengi mno.
I wrote niliandika mbona sema ! Ndio kile kipindi mambo yalikuwa mengi chuo , kesi Mahakamani .
 
Haya ndio majitu ambayo yalikua yanajiita mazalendo kwa kujificha kwenye kichaka cha baba yao, sasa ndio rangi zao halisi zinaanza kuonekana , waacheni waumbuke ndio maana hata mama inamuwia vigumu kumpa hata ujumbe wa nyumba kunmi kumi kwa jinsi anavyonuka Rushwa .
 
Nondo mdogo wetu, wewe ni mwanasiasa..ukitaka kuwin political fans wa kibongo achana na kushambulia 'dead snake'. PIGA 'nyoka' hai aliyepo kwny usukani kwan huyo ndio competitor wako! Okotaokota huko udhaifu serikalini weka kweupee kama ulivyofanya leo.kigogo, zitto au mange they grew famous kwa kuanika mambo live!
Hii ya leo ni marudio tuu , l wrote and l did kipindi Magufuli akiwa Rais na Kipindi Makonda akiwa Mkuu wa Mkoa na Gazeti likaandika front page ,
 
Makonda alikuwa juu ya sheria.... Alivamia Clouds lakini Waziri Nape ndio akapoteza kazi; hakuna jambo angefanywa wakati Jiwe yupo, swali ni je, bado anahiyo political cover? Au kaachwa aliwe na fisi?
Alishawahi kupitisha barabara kwenye shamba la bwana mallya huko kigamboni ati anawatetea wananchi ili achukue kupanda.
 
Kumbe P ni mbonge la Rapper
JF imekumbatia vipaji vya Watu sana.
Kiukweli sii wengi wananifahamu, kabla sijawa mtangazaji, nilikuwa DJ on the radio, na nilikuwa rapper.
moja ya versi zangu ni hii
"Do you wanna dance, you to turn on" X 3
If you wanna dance, you need to turn on, the EXTS of RTD, and this is P of RTD, rapping on a mic in a special way, when you wanna dance and feel alone, you just need to turn on the EXTS of RTD cause we are on the air.
P
 
17, Oktoba ,2019 niliandika Barua Sekretariati ya Maadili chini ya Kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Marehemu Jaji Mstaafu Harold R. Nsekela nikiomba kukagua Daftari la Maslahi , Rasilimali na madeni pamoja na matamko ya zawadi ya Makonda kama ambavyo kanuni za maadili ya viongozi wa umma za 1996 Na. 168 kifungu cha 6 na 7 kinavyoniruhusu mimi kama Raia kuomba kukagua Daftari hilo.

Barua yangu ilijibiwa tar 15 ,Novemba 2019 ,wakikataa kunipa ushirikiano kukagua Daftari la Makonda nilijua tuu ni kwasababu ya hofu iliyokuwepo na namna Makonda alivyokuwa anaogopwa . Ila suala la kukagua Daftari la mtumishi wa umma katika ofisi ya Sekretariati ya maadili haipaswi kuwa suala la kuomba au la siri, kiongozi akishakuwa mtumishi wa umma tuu kila kitu kuhusu utumishi wake kinapaswa kiwe wazi na umma ujue.

Sheria ya Takukuru Namba 11 ya mwaka 2007 ,kifungu cha 27 kinasema " Ni kosa mtumishi wa umma kuwa na mali ambazo mwenye nazo hana maelezo ya kuridhisha kuhusu alivyozipata au kuwa na mali au pesa nyingi kuliko kipato chake halali " .

Kwangu mimi binafsi nilikuwa na wasiwasi na fedha na mali za Makonda, alikuwa na nafasi ya Mkuu wa mkoa tuu.Ila hakuna aliyewahi jua wapi kwingine alikuwa anapata fedha kwa namna alivyokuwa anagawa na kutumia.

Msukuma tar 7/Feb 2019 alitoa tuhuma Bungeni kwamba Makonda ana miliki mali nyingi tofauti na kipato chake akataja Gari Lexus ya Mil.400,magorofa Mwanza, ana miliki magari Toyota V 8 ,alikarabati ofisi yake kwa milion 400 bila kufuata utaratibu wa manunuzi (Chanzo Gazeti la mwananchi tar 8 Feb 2017,J.tano.).

Mh.Joseph Selasini Bungeni tar 11 , Feb 2017 kwamba Makonda ana miliki Apartment Viva Towers lenye thamani ya milion 600 (Chanzo Gazeti la Mwananchi February 11,2017).

Blog ya Sauti Kubwa,tar 30 Agosti 2018 aliandika na kuambatanisha na nyaraka mbalimbali za umiliki wa viwanja kwamba Makonda ana miliki Ardhi Dodoma eneo la Iyumbu new Town Center viwanja sita jumla mita za mraba 92,341 .

Pia Kugawa gawa fedha.

Tarehe 3/Juni/2019 alitoa fedha kwa wachezaji wa Simba mil.10 kwa Golikipa Manula,milion moja moja kwa kila mchezaji,mil. 2 kwa mchezaji wa kike,milion 3 kwa msemaji wa simba @hajismanara na septemba 9,2019 akatoa milion 10 kwa Juma Kaseja ,tar 5 Oktoba 2019 uwanja wa uhuru Dar alitoa Shiling Mil.100 kwa wajumbe wa shina wa CCM Mkoa wa Dar.(Chanzo Millard Ayo na EATV).

Tarehe 18/Septemba/2019 siku ya Jumaano kupitia Gazeti la Mwananchi iliandika kichwa cha habari "Makonda aeleza anakotoa fedha". Makonda kwa kauli yake ya mdomoni baada ya watu kuhoji wapi anapata fedha hizo zote za kugawa gawa ikiwa yeye ni mkuu wa mkoa tuu.

Katika taarifa hii alisema yeye anatumia watu wenye kipato kikubwa kuwaelezea shida na wao hutoa msaada akitolea mfano milion 10 alizompa Juma Kaseja , Makonda alijibu pia nchi hii ni tajiri na watu wake ni matajiri .Kama fedha alikuwa anapewa na wahisani au marafiki je sheria ya inasemaje mtumishi wa umma anapopokea zawadi ? .

Sheria ya maadili ya viongozi wa umma Na. 13 ya 1995 kama ilivyofanyiwa marekebisho kuanzia kifungu cha 12(2 na 3) inaeleza utaratibu wa mtumishi wa umma kupokea zawadi ya zaidi ya thamani ya laki mbili, alipaswa kutoa taarifa kwa muajiri wake lakini pia taarifa ya matamko ya zawadi alizopewa yanapaswa kuwepo katika ofisi ya Kamishna Sekretariati ya Maadili.

Hivyo lengo langu nilitaka kujua idadi ya mali alizo nazo na nilitaka kujua kama hizo zawadi anazipokea kama huwa anaziwasilisha kwa Boss wake kwa mujibu wa sheria ya maadili na kanuni zake ,ili ndio nipate facts za kupeleka malalamiko yangu TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria ya Takukuru Na.11 ya 2007 kifungu cha 39 kinachonipa mimi mamlaka kama mwananchi kutoa taarifa kwa TAKUKURU popote ninapoona kuna makisio ya uwepo wa Rushwa ,

Ili TAKUKURU ifanye kazi yake ya kuchunguza na kujiridhisha (Prove or disprove the allegations) ni kazi ya TAKUKURU kama ilivyoelezwa katika sheria ya TAKUKURU kifungu cha 7(e),(f),i,ii,iii, na cha 10 (1) a,b,c . Nadhani TAKUKURU bado wanasababu nyingi zaidi kufanya uchunguzi juu ya Allegations na nyingine nyingi dhidi ya Paul Makonda .


Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa-ACT Wazalendo.

13/Machi/2022.

Kigoma-Ujiji.View attachment 2148675
huyu mtu anatakiwa ashitakiwe kama alivyofanyiwa sabaya tu. tena inasemekana mwanzoni alikuwa anashida arusha ili kumsaidia sabaya alipoona pamoto akaufyata.
 
Kiukweli sii wengi wananifahamu, kabla sijawa mtangazaji, nilikuwa DJ on the radio, na nilikuwa rapper.
moja ya versi zangu ni hii
"Do you wanna dance, you to turn on" X 3
If you wanna dance, you need to turn on, the EXTS of RTD, and this is P of RTD, rapping on a mic in a special way, when you wanna dance and feel alone, you just need to turn on the EXTS of RTD cause we are on the air.
P
Hongera mkuu kumbe upo na kipaji nyuma ya Taaluma.

Kuna watangazaji wengi kwa sasa wanaimba, sema labda umri umeenda kidogo tungependa kukuona majukwaani licha ya kuwa mtangazaji.
 
Back
Top Bottom