Sikukuu za kidini ndio ziwe siku za kutoa msamaha kwa wafungwa badala ya siku ya uhuru

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Huu ndio ushauri wangu kwasababu dini zote zinatambua na kuhuburi msamaha kwa wakosaji.

Kwa msingi huo, kiongozi mwenye imani ya kidini, atakuwa sahihi zaidu kutoa msamaha kwa wafungwa katika sikukuu za kidini.

Na jatika hili, sidhani kama kuna sheria inatamka kuwa misamaha hiyo itolewe kwenye siku za kusherehekea uhuru wa nchi yetu tu zaidi ya kufuata utamaduni wa mtu mweupe(Wakoloni).

Tusherekee sikukuu hizi kwa kufanya kwa vitendo yale yaliyohubiriwa na Manabii na Mitume tunaowaamini..

Siku tukipata kiongozi mpagani, basi atatumia siki ya uhuru kutoa msamaha kwa wafungwa.

Najua kuna watu watasema serikali haina dini, ila swali ni je, inasamehe wafungwa kwa misingi gani kama sio kuzingatia ubinadamu unaotajwa katika vitabu vya dini?

Tuanze sasa.
 
Nchi haina dini!
Unakotupeleka siko! Vipi kama msamaha utafuate misingi ya majina ya hao wafungwa??
 
Nchi haina dini!
Unakotupeleka siko! Vipi kama msamaha utafuate misingi ya majina ya hao wafungwa??
Hakuna dini inayohuru ubaguzi wa aina hiyo. Kiongozi mwenye hofu ya Mungu, hawezi kutenda uyasemayo na atakuwa Kiongozi wa ajabu sana.

Yaani wewe kiongozi wa nchi, unajua kabisa kuna wafungwa kutokana na hali zao, wanahitaji msamaha, badala
yake, unawapelekea mchele na mafuta wakale sikukuu wakiwa gerezani halafu unasubiri siku ya uhuru, ndio utoe msamaha? Does it make sense au tunaishi kwa mazoea tu?
 
Dini zipo nyingi, ukitaka iwe hivyo unamuweka katika Mazingira gani Rais asiye wa dini hiyo? Je, na sikukuu za kidini za wahindi nazo zitajumuishwa?

Sikukuu za utaifa ni sawa kwa sababu wote tunaunganishwa na utaifa
 
Wafungwa wanaostahili msamaha, orodha yao huandaliwa na watendaji husika kwa kuangalia wanaostahili kisha Raisi huidhinisha waachiwe huru. Sasa hapo ugumu unatoka wapi? Kwani hivyo orodha huandaliwa kwa kuangalia mfungwa ni wa din ganii au wahusika huzingaria vigezo vilivyowekwa?
 
Kabisa Rais mkristo au muislamu atoe msamaha siku ya sikukuu za wahindi? Tuache masihara ,hiyo ni dhihaka kwa Mungu wa mbinguni
 
Hakuna dini inayohuru ubaguzi wa aina hiyo. Kiongozi mwenye hofu ya Mungu, hawezi kutenda uyasemayo na atakuwa Kiongozi wa ajabu sana.

Yaani wewe kiongozi wa nchi, unajua kabisa kuna wafungwa kutokana na hali zao, wanahitaji msamaha, badala
yake, unawapelekea mchele na mafuta wakale sikukuu wakiwa gerezani halafu unasubiri siku ya uhuru, ndio utoe msamaha? Does it make sense au tunaishi kwa mazoea tu?
Wafungwa wengi ni wahalifu! Waendelee tu kukaa huko kwa ajili ya Usalama wao
 
Nadhani hilo litaupima U secular wa Serikali yetu nadhani ni bora misamaha iwe inatolewa kwenye sikukuu za kitaifa.
 
Nahisi waliamua kufanya hivyo ili kuiepusha serikali kuonekana ina uhusiano wa kidini, hata kama watu wake wana dini.
 
Back
Top Bottom