Sikukuu ya uhuru Tanzania: Una kitu gani cha kumweleza Julius K Nyerere?

Natalia

JF-Expert Member
Jul 3, 2011
4,324
1,892
I say thank you to Julius k Nyerere kwa kweli nikiona nchi zingine hazina Amani nasema " God may Nyerere soul rest in peace .Pia thank you " Alexander Nyirenda .Wako mbinguni
 
Naomba kueleweshwa, ni uhuru wa Tanzania au TANGANYIKA??

Kama Mwalimu wangu Historia alikuwa sahihi tar 9 disemba ni uhuru wa Tanganyika. Ni ulimbukeni wa hali ya juu sana wa Baba Mwanaasha kujaribu kufunika historia ambayo itakuja kumhukumu siku moja. Mwaka 1961 hakukuwa na nchi inayoitwa Tanzania Bara, ukweli huu hauwezi kupingika.

Sisi Tanganyika hatuhitaji kuanzisha vikundi vya kihuni kama UAMSHO kudai Tanganyika, lakini watawala jaribuni kuonyesha heshima kwa Tanganyika maana kuna kila dalili kwa inakaribia kurudi
 
Hivi Tanzania ilitawaliwa lini na nani mpaka ipate uhuru? Tangu Tanzania izaliwe imekuwa chini ya MAGAMBA mpaka leo so kwangu naona Tanzania bado ipo chini ya koloni la MAGAMBA so hilo wazo lako la kuwepo kwa siku ya uhuru wa Tanzania ni mpaka pale chama cha upinzani kitakapochukua nchi.

Unless uwe unamaanisha maazimisho ya miaka 51 ya uhuru wa TANGANYIKA/TANZANIA BARA hapo tutaelewana.
 
...Kwamba nchi inazidi kudidimia miaka nenda miaka rudi pamoja na rasilimali kubwa sana zilizogunduliwa miaka ya karibuni. Nchi imeingiliwa na manyang'au wameiteka nyara Serikali na kufanya ufisadi wa hali ya juu kila mwaka na amani iliyopo miaka ya nyuma nchini taratibu inaanza kupotea.
 
Namuuliza Nyerere, ni mwafrika mkombozi wa wenzake wengi, kwanini aliacha jina la utumwa na mji wa Daressalaam? au hajui ilianzaje? ni ubwete bwete wa kupata watumwa kwenda zanzibar wakauzwe.
 
Namuuliza Nyerere, ni mwafrika mkombozi wa wenzake wengi, kwanini aliacha jina la utumwa na mji wa Daressalaam? au hajui ilianzaje? ni ubwete bwete wa kupata watumwa kwenda zanzibar wakauzwe.
Sikuelewi
 
I say thank you to Julius k Nyerere kwa kweli nikiona nchi zingine hazina Amani nasema " God may Nyerere soul rest in peace .Pia thank you " Alexander Nyirenda .Wako mbinguni
hakuna nchi inaitwa tanzania ilipata uhuru tarehe 09.12....Nitamwambia naitaka tanganyika yetu
 
Back
Top Bottom