Sikukuu na salamu za mchele na mbuzi kutoka kwa rais

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,683
8,829
Nimesikia kwa miaka mingi sasa maraisi wetu wakitoa msaada na salamu za mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia kwa wenzetu wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Jamani, hivi nyama ya mbuzi na wali mbona naona kama vinakinaisha? Pia Waswahili tunapenda wali kuku, je kwanini maraisi wetu wasiwe wanatoa makuku badala ya mbuzi?
Bado niko Mafia napunga upepo, nimewamiss sana.
Idd Mubaraq

Ni Aibu kubwa sana kwa mkuu kwa Nchi kutoa vimbuzi na vimchele halafu anatangaza kwenye vyombo vya habari kwani huko ni kuwanyanyapaa watoto waishio ktk mazingira hatarishi - ITIFAKI IMEZINGATIWA:deadhorse:

• Thanks
Reactions: Ame

kwenye red mkuu, nahisi umevaa msuli kitu kinapata upepo wa baharini!!!!

Ni Aibu kubwa sana kwa mkuu kwa Nchi kutoa vimbuzi na vimchele halafu anatangaza kwenye vyombo vya habari kwani huko ni kuwanyanyapaa watoto waishio ktk mazingira hatarishi - ITIFAKI IMEZINGATIWA

umeona ehhhh

vyo
Ni Aibu kubwa sana kwa mkuu kwa Nchi kutoa vimbuzi na vimchele halafu anatangaza kwenye vyombo vya habari kwani huko ni kuwanyanyapaa watoto waishio ktk mazingira hatarishi - ITIFAKI IMEZINGATIWA:deadhorse:

Katika mambo yote yanayonihuzunisha hili ni mojawapo wa viongozi wa taiafa kutoa zawadi za wali na mbuzi; jamani ni haki kwa yatima na wasiojiwea kupewa social services na serikali yao na katika hilo hiyo package ya wali na mbuzi wakati wa sikukuu ni haki yao na wala si zawadi. Vipi wakuu wa nchi kuwapa watoto zawadi za kifamilia badala ya za kisera kama kuandaa policies nzuri zinazoweza ku cater for these needs? Ingekuwa kila ikifika hizo siku serikali inaboresha sera kwa kadiri uchumi unavyokuwa (kama wanavyotuambia uchumi wetu unakuwa) hiyo ingekuwa ni zawadi bora lakini mambo ya mbuzi na mchele kweli ni uzalilishaji wa hali ya juu kwa hawa minor citizen wa Tanzania.

Hata enzi za mababu zetu kulikuwa na sera nzuri tu za kuwatunza yatima na wajane kwa kuamuru mf. kaka mkubwa kurithi mke ama mtoto; ninyi mtasema eti ni mila potofu lakini kumbuka hakukuwa na watoto wa mitaani. Wenzetu walipo endelea waliboresha hizo sera na kutafuta mbadala lakini sisi tukawakabidhi mitaa kuwalea hao watoto wetu bora huku tukibugia pesa zao kibao wanazopewa na hao ambao angalau wanaoheshimu thamani ya mwandamu kwa kisingizio cha kuondoa mila potofu kumbe ni kujaza matumbo yetu yasiyojaa.

mwenzio kapelekwa huko na bwana jambajamba koromakoroma

hahahahahahhahahahahahahahahaha.....
Kha! Bujibuji tuonee huruma na mabvu zetu lol! yaani nimecheka hadi kwikwi imenishika kweli Eid imewadia

yaani katika vitu jk ananikasirisha kiukweli ni hawa mbuzi
kwanini kama anaupendo wa kweli asijitolee kuwasomesha hawa watoto japo elimu ya msingi
hawa mbuzi sana sana labda wanakuwa ni faida ya wenye vituo
au wanawala halaf chooni mchezo umekwisha au mzee alimpa hayo masharti?
basi atoe mbuzi watoto wale kisha atoe elimu manake vyote wanavihitaji

vyo

Katika mambo yote yanayonihuzunisha hili ni mojawapo wa viongozi wa taiafa kutoa zawadi za wali na mbuzi; jamani ni haki kwa yatima na wasiojiwea kupewa social services na serikali yao na katika hilo hiyo package ya wali na mbuzi wakati wa sikukuu ni haki yao na wala si zawadi. Vipi wakuu wa nchi kuwapa watoto zawadi za kifamilia badala ya za kisera kama kuandaa policies nzuri zinazoweza ku cater for these needs? Ingekuwa kila ikifika hizo siku serikali inaboresha sera kwa kadiri uchumi unavyokuwa (kama wanavyotuambia uchumi wetu unakuwa) hiyo ingekuwa ni zawadi bora lakini mambo ya mbuzi na mchele kweli ni uzalilishaji wa hali ya juu kwa hawa minor citizen wa Tanzania.

Hata enzi za mababu zetu kulikuwa na sera nzuri tu za kuwatunza yatima na wajane kwa kuamuru mf. kaka mkubwa kurithi mke ama mtoto; ninyi mtasema eti ni mila potofu lakini kumbuka hakukuwa na watoto wa mitaani. Wenzetu walipo endelea waliboresha hizo sera na kutafuta mbadala lakini sisi tukawakabidhi mitaa kuwalea hao watoto wetu bora huku tukibugia pesa zao kibao wanazopewa na hao ambao angalau wanaoheshimu thamani ya mwandamu kwa kisingizio cha kuondoa mila potofu kumbe ni kujaza matumbo yetu yasiyojaa.

Wapi wali mbuzi....... Hahahhhahahahahahahahf
Jakaya wali mbuzi....dunia ya Tanzania haiishi vimbwanga.

ndicho anachojuwa kuchezea pesa zetu..kwanini asiwanunulie hata hiace ambayo watapata mlo wa kila siku ikipiga daladala?

dah kumbe uko holiday ndio maana husikikii. injoyi yua olideyi NJ

hao mbuzi na mchele wala sio hela inayotoka mfukoni mwake ni zile hela zinazotengwa kwaajili ya dharura huko ikulu na pia anachukua hela zile za majanga ndio anatoa zawadi na inawezekana hata hajui ni vituo vingapi vimepewa hao mbuzi na mchele yeye anapelekewa riport baadae na ufisadi unafanywa pia kupitia kwa hao hao wanaojifanya kutoa msaada kwa niaba ya m...kwe....re, hapo hakuna lolote ni kodi zetu ndio hizo wanazojifanya kutoa msaada. NASEMA HIVI watoto hawataki mbuzi na mchele kwani huo mda wa mwaka mzima wanakula nini? wanahaitaji elimu bora, waboreshewe makazi yao, nguo mpya,vitabu na kukuza vipaji vyao sio mbuzi. unafiki tu huuuuuuuuu.

• Thanks
Reactions: Ame
Nimesikia kwa miaka mingi sasa maraisi wetu wakitoa msaada na salamu za mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia kwa wenzetu wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Jamani, hivi nyama ya mbuzi na wali mbona naona kama vinakinaisha? Pia Waswahili tunapenda wali kuku, je kwanini maraisi wetu wasiwe wanatoa makuku badala ya mbuzi?
Bado niko Mafia napunga upepo, nimewamiss sana.
Idd Mubaraq

Inabidi Ikulu waangalie na kubadilisha hii kitu. Kwanza ni makosa kuita zawadi ni makosa vilevile kuita msaada kwani kupata mlo ni haki ya Kikatiba ya kila mtanzania sio yatima tuu na haki hiyo inatakiwa itolewe toka tarehe moja Januari mpaka tarehe 31 disemba.

Ibara ya 14 ya katiba ni pana sana ingawa ina mstari mmoja:

Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

Kama watanzania tutakuwa imara kudai haki zetu huenda wakala kuku kila siku badala ya wali mbuzi siku za sikukuu.

• Thanks
Reactions: Ame
Ame umenena vyema!

Nahofia nikoongeza nitaharibu! We don't need favors, ahadi and the like! We need better policies, system and stratergies; kwani it is our kodi and we need to allow accountable uses of them! I hope sijaharibu sana!

donti ageni raiti hard ingrysh

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom