Sikukosea kuihama CCM na kujiunga CHADEMA,

David Djumbe

Member
Oct 14, 2013
42
36
Katika kipindi hiki ambapo tumeshuhudia mvutano mkubwa ndani ya CHADEMA, kutokana na baadhi ya viongozi waandamizi kuvuliwa madaraka kwa tuhuma mbalimbali na kamati kuu, nimejikuta nikiwa katika wakati mgumu wa kujaribu kuelewa kwa undani na kupata ukweli na usahihi juu ya haya yanayosemwa.
kutokana na ushabiki, watu wengi huwa wanakuwa na mapenzi ya upofu ambayo huwafanya kushindwa kutafakari na kujirudisha kwenye neutral pale panapotokea mvutano wa pande mbili, ni hatari zaidi kukurupuka na kuanza kufafanua jambo ambalo hukulifanya wewe, na badala yake ukawa muongeaji kuliko hata mhusika mwenyewe.
Hii ni sawa na kuingilia ugomvi wa mke na mume ambao huisha na matokeo yake wewe ulieuingilia ukabaki na aibu.

Katika kipindi cha miaka 2 ambayo nimekuwa CHADEMA, nimejifunza na kujiridhisha kwamba niko kwenye chama sahihi ambacho kinathubutu kuchukua hatua pale kinapoona kuna kitu hakiendi sawa, haina maana kwamba kila hatua inayochukuliwa ni sahihi kwa 100%, la, lakini kitendo cha kuhisi kuna tatizo na kulifanyia kazi bila kujali nani kahusika ni msingi mzuri wa utawala wa kitaasisi.

Nilikuwa CCM tangu 1994 na kukitumikia kwa nguvu zote hadi mwaka 2005 nilipoanza kukosa nguvu za kuendelea kutokana na jinsi mfumo wao ulivyo wa kimaslahi zaidi,(kama wewe una uchungu sana na jamii, unatengwa na badala yake wale wenye kupenda kujipendekeza na wajanja wa janja wa mjini ndio wanaopewa nafasi zaidi)
niliamua kukaa nje ya siasa kwa miaka zaidi ya 5 nikiangalia namna siasa za nchi hii zinavyokwenda na baadae nkaamua kujiunga na CHADEMA.

kinachoendelea sasa ndani ya CHADEMA ni matayarisho ya chama kujiandaa kuongoza nchi>>> mimi nitamshangaa kila mtu kama atafikiri chama chenye nguvu ambacho ni tishio kwa chama Dola kitakuwa kimetulia kama maji mtungini katika kipindi kama hiki ambacho ni karibu kabisa na uchaguzi mkuu.... hizi ni changamoto na sio tatizo kupitia hapa!!! tatizo ni kushindwa kuzikabili changamoto hizi zilizopo mbele yetu.
kama wote kweli nia yetu ni kuiondosha CCM madarakani 2015, naamini katika kipindi hiki kila mmoja atatumia busara zaidi kukabiliana na haya yanayotokea na sio hasira wala jazba...

Natoa rai kwa wana CHADEMA wote, viongozi na wanachama wa kawaida, kutambua kwamba hii sio vita dhidi ya Zitto na Mbowe, hii ni vita ya ukombozi dhidi ya CCM, na hivyo silaha zetu zote ni lazima zielekezwe huko na sio kugeukiana wenyewe, tukubali pale tunapokosea na tuanze hatua nyingine pamoja.

haya ni maoni yangu kama mwanachama na yasihusishwe na nafasi yeyote niliyo nayo kama kiongozi.
 
At least hoja hii ina mashiko kuliko yule anayetangaza assasination kwenye jukwaa kule......eti zitto hatarini kuuwawa!!!
 
wimbi la viongozi chadema kujiuzulu liachwe wanawajibika kupigania wanachokiamini wakiwa ndani maana wakitoka hawatakuwa na haki ya hiyo.Hiki ni chama kwa watanzania mliopohuko mhakikishe kinaendeshwa kukidhi matakwa ya watanzania.
 
David Djumbe

Mwambie Maxence Melo akuwekee 'Verified User'. Au amesahau kuwa ulikuwa rais wake pale DIT?

Djumbe alikuwa presidaa pale DIT, Max Melo atakuwa anamkumbuka huyu. Eng Djumbe alikuwa mwanaharakat tangu akiwa pale DIT.Alifahamika kwa misimamo thabiti kutetea wanafunzi, hasa wakati ule mfumo uitwao education cost sharing, mtangulizi wake yaani Eng Ojendo na baadae Eng Lukombe King'ombe walipinga sana hii kitu iitwayo cost sharing, wakati ule mimi sikuelewa kwa nini walipinga kumbe baadae ndo ikazaliwa hii iitwayo Loan Board, ndipo nikagundua kwa nini wenye maono ya mbali walipings
 
All in all inapaswa kuheshimiana na kukubali kukosolewa.hakuna aliejuu ya sheria. Chadema mnapaswa kuwa mfano kama mlivyoahidi. Makosa mnayofanya yanawavunja nguvu wafuasi wenu kumbukeni muda unayoyoma. Kweli adui yenu anafanikiwa sasa! !
 
Nafarijika kuona kuna watu waelewa na hata upeo wao wanaona mbali, hata J.K.Nyerere alipingwa na baadhi ya watanzania kumwondoa mkolon, so CDM Tusipate taabu kulumbana na wapinga ukombozi. 2015 si mbali
 
Ahsante kwa uchambuzi mzuri. Nafahamu harakati zako na jinsi unavyosimamia hoja zako. Zaidi nakumbuka ulivyoanzisha umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu TAHLISO na kuwa rais wao wa kwanza. Mungu akubariki
 
David Djumbe alitumia muda mwingi akiwa chuoni kufanya harakati za mabadiliko vyuo vikuu kuliko muda wa darasani hadi wakataka kumfukuza pale DIT likini wakashindwa, akaanzisha Umoja wa Wanafunzi Vyuo Vikuu nchini TAHLISO na kuwa mwenyekiti wa kwanza wa umoja huo... ni mtu anayejua namna ya kukabiliana na migogoro na ndio maana nilikuwa nashangaa sana kuona yuko kimya kwenye siasa za nchi hii...BIG UP sana Presdaa wetu..
 
Back
Top Bottom