Sikujua kama UKIMWI umeshakuwa wa kawaida kiasi hiki

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
2,827
3,569
Ni leo mchana nilikuwa napata lunch kwenye kijiwe kimoja O'bay, ni katurubali flani tunakopatia msosi wa bei poa. Nikakuta wadada watatu nao wanasubiria order yao kwenye meza ya mbele yangu. Mazungumzo yao sasa, loh! Yaani ukimwi wanauzumgumza kama vile ni kahoma flani tu!

Ilikuwa kama hivi:

Mdada 1: Mwenzangu umejiachia! Ufanyage mazoezi shoga, unene pia sio mzuri
Mdada 2: Najitahidi lakini loh! Hivi clinic wewe unaendaga wapi?
Mdada 1: Sisi clinic yetu ya kistaarabu, ya kisomi hasa. Mwenyewe naingiaga saa nane. Hata usiku wanahudumia, unaweka tu appointment na dr wako. Yani wako safi sana.
Mdada 2: Hongera, uko kwa vigogo!
Mdada 1: Yaani ni wa ukweli. Ila wananiudhi kitu kimoja wanachelewesha majibu ya viral load (Nikaanza kustuka, viral load si ni ngoma jamani?)
Mdada 3: Wapi huko hampimwi viral load?
Mdada 1: Kupima wanapima sema majibu ndio wanachelewesha sana. Na mi nataka nione matokeo ya juhudi zangu maana sijawahi kukosa kidonge tangu nimeanza
Mdada 2: Ingekuwa amri yangu ningetaka nipimwe viral load kila mwezi
Mdada 3: We Z*n*a umeanza lini dawa kwani unataka kupimwapimwa hovyo
Mdada 2: Si hovyo jamani hivi unajua kila mwenye HIV angefanya kama sisi ukimwi ungebaki historia (Nikawakodoloea mimacho tena, ni wadada wazuri acha!)
Mdada 1: Yule baba tunakutanaga clinic (akaelekeza kwa jibaba flani limeshibashiba, linaangaza angaza macho kutafuta pa kukaa. Akanyoosha mkono kumwashiria aje. Akasogea karibu. Jamaa anaonekana smart sana)
Jibaba: Hey vipi wewe
Mdada 1: Niko poa, niambie.
Jibaba: Unafikaga huku?
Mdada 1: Huku mbona ndio maeneo yetu? Ofisi yetu ile pale (akaonyesha jengo la ghorofa upande wa pili wa barabara). Tuko third floor.
Jibaba: Napajua sana kumbe uko pale
Mdada 1: Eeeh. Na hawa tuko nao (akatambulisha wale wenzie wawili)
Jibaba akaaga akaenda kukaa na wenzie wengine, inaonekana kama alikuwa anawasubiri. Wadada wakaendelea na mazungumzo, wanaongelea wenzao wanaokutana nao huko clinic, mara fulani kajifungua, mara fulani anaolewa nk.

Nikamaliza kula nikaondoka mdogomdogo na mawazo, huku mazungumzo yao yakibakia kichwani mwangu kama mwangwi hivi! Nilivyonasa hiyo script (bila tape recorder) ni ushahidi wa jinsi mazungumzo ya hao wadada yalivyonikamata!

Hivi jamani mnajua kuna tofauti sana kati ya kusikia matangazo ya ARV redioni na kuwasikiliza wanaosema wanazitumia? Pia kuna tofauti sana kati ya kusikia kuhusu takwimu za ukimwi na kukutana live na wenye ujasiri wa kusema 'tuna VVU'!
Niseme ukweli, sikuamini kuwa tumefikia hatua ya kuwa ukimwi unaonekana wa kawaida kiasi hiki!
 
Yaani sura za wale wadada bado zimeniganda. Nimewaangalia sikuwamaliza! Na yule jibaba pia!
Pia nimeelewa jinsi unyanyapaa unavyokuja. Neno la unyanyapaa nimelisikia sana, lakini sikujua kama hata mimi naweza kunyanyapaa bila kujielewa!
Pole, japo sijaona kama umewanyanyapaa Ila ni vile tulizoea wenye HIV zamani walikua wanaisha miili na kuteseka sana hali ambavyo ni tofauti mnoo na sasa watu huwezi wadhania..eh Mungu aepushie mbali.
 
Tatizo siku hizi kuna maradhi mabaya zaidi ya Ukimwi, Ukimwi ukiipata ukazingatia masharti mbona unaish na mipango Yako unaifanya Kama kawaida Ila kuna maradhi ukiyapata hata mipango Yako hayaendi Ndio maana sikuhiz watu wanaudharau Ukimwi. Mfano maradhi ya kansa, Ni hatari zaidi ya Ukimwi
 
Ulifaa uwe mwandishi shushushu ama tape recoder umewanukuu vizuri ila kwenye mambo ya msingi kama ile asilimia 65 ya watz wana ngoma nilistukaga sana kumbe yule mwandishi alikuwa poyoyo
 
Tatizo siku hizi kuna maradhi mabaya zaidi ya Ukimwi, Ukimwi ukiipata ukazingatia masharti mbona unaish na mipango Yako unaifanya Kama kawaida Ila kuna maradhi ukiyapata hata mipango Yako hayaendi Ndio maana sikuhiz watu wanaudharau Ukimwi. Mfano maradhi ya kansa, Ni hatari zaidi ya Ukimwi
Umesahau kisukari,na presha
 
Ulifaa uwe mwandishi shushushu ama tape recoder umewanukuu vizuri ila kwenye mambo ya msingi kama ile asilimia 65 ya watz wana ngoma nilistukaga sana kumbe yule mwandishi alikuwa poyoyo
Akiwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi tutampoteza tu
 
Back
Top Bottom