Sikubaliani na utumbuaji unaoendelea

seckymose

Member
Dec 29, 2016
87
47
Kheri ya mwaka mpya wakuu,

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu utumbuaji unaoendelea haswa huu wa karibuni ambao tumeshuhudia Bosi wa TANESCO Ndugu Felichesmi Mramba akitumbuliwa kwa kile kinachosemekana kupandisha bei ya umeme bila ridhaa ya waziri(mhongo---muongo).

Hivi hakuna njia ya kumrekebisha mtumishi wa umma isipokuwa kumtumbua tu? katika mmchakato wa kupandisha bei ya umeme kuna taasisi ngapi zinahusika? mbona hizo taasisi nyingine ambazo zimeratify swala hilo wameachwa tu?
 
Hapana kaka, hakuna jinsi, makosa lazima yaadhibiwe vikali kukomesha tabia ya "Biashara kama kawaida" ili kutekeleza azma yetu ya kuwalinda "wananchi wanyonge, walioumbwa kwa mfano wa Mungu", hakuna namna, majipu yanayojilipa bonus kubwa hivyo wakati shirika halina ufanisi wowote lazima yatumbuliwe kikatili tu; Duterte style, period.
 
Tanesco imekuwa ni Biashara badala ya kuwa huduma.wananchi wanaumia ati
 
Tunataka MTU atakaye zalisha umeme kwa gesi yeye anajua kutumia maji tu so hatumhitaji kwa sasa.
 
Katika hili Mramba kaonewa. Sidhani kama alikurupuka mwenyewe na kupandisha bei. Lazima kuna tasisi nyinine zilihusika. Kwanini iwe yeye tu ndo kawajibishwa? Au ndio mbuzi wa kafara?
 
Bado sawala la kupandisha hovyo bei ya petrol na mafuta mengi wasiposhirikisha serikali idara husika ni ktumbua tu
 
Nafikiri hata Mhongo anapaswa kutumbuliwa tena wa kwanza, kwani upandishaji wa gharama lazima ukubaliwe na yeye. Lakini nafikiri kuna watu wanatafutwa ili waondoke ukipatiwa kasababu unatoka bila kujali haki. Kukurupuka kumezidi awamu hii.
 
Back
Top Bottom