Sikubaliani na suala la TANESCO kukata Rufaa kesi ESCROW

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Habari wana JF

Nianze kwa kuonesha msimamo wangu juu ya mchakato wa TANESCO kutaka kukata rufaa hukumu iliyotolewa ICSID. Mimi siungi mkono ukatwaji wa rufaa hiyo kwa sababu zifuatazo:

Sioni TANESCO kukata rufaa wanatafuta nini! Je, wanamtetea Harbinder Singh Seth ambaye amekwapua pesa ambazo si za kwake? Singasinga huyu aliishaihakikishia serikali kuwa hakuna mtu mwingine atakayekuja kudai ile pesa iliyokuwa kwenye akaunti kuwa ni yake. Sasa mwenye nayo kapatikana na kwa hukumu ya ICSID ndiye anastahili kulipwa ile pesa. Sasa kwanini huyo Singasinga mwizi asirudishe pesa yetu na aadhibiwe kwa mujibu wa sheria za nchi yetu? Kwa nini tuendelee kupoteza pesa kwa jambo ambalo linaeleweka hatima yake?

IPTL wasitulaghai kuwa wanaunga mkono TANESCO kukata rufaa hata kidogo. Lazima wao watake iwe hivyo kwa sababu ile hukumu ni mwiba kwao. Kwanza wanatakiwa kurudisha pesa waliojizidishia ambayo wanaendelea kutunyonya Watanzania hadi leo. Pili hiyo mitambo inastahili kutaifishwa baada ya kumning'iniza Harbinder Seth mahakamani kwa makosa mbalimbali.

Mheshimiwa Rais tunahitaji hatua madhubuti zichukuliwe mara moja dhidi Harbinder Seth na mnyororo mzima wa watu waliomsaidia kukwapua pesa za ESCROW hasa awajibike kuilipa benki ya Standard chartered ya Hongkong. Kukata rufaa ni kuendelea kupoteza pesa za Watanzania.
 
Anko
mpinga ufisadi mbona umevaa miwani , huoni hili

Ha ha ha siasa bana,kimyaaaa..Ila enzi zile za majukwaani mikwara mingi
 
Serikali ikubali kwamba ilibugi kwenye kumlipa singasinga zile hela za escrow. Hizi rufaa wanazokata na kushindwa kila saa...riba inazidi kuongezeka tu
 
Habari wana JF

Nianze kwa kuonesha msimamo wangu juu ya mchakato wa TANESCO kutaka kukata rufaa hukumu iliyotolewa ICSID. Mimi siungi mkono ukatwaji wa rufaa hiyo kwa sababu zifuatazo:

Sioni TANESCO kukata rufaa wanatafuta nini! Je, wanamtetea Harbinder Singh Seth ambaye amekwapua pesa ambazo si za kwake? Singasinga huyu aliishaihakikishia serikali kuwa hakuna mtu mwingine atakayekuja kudai ile pesa iliyokuwa kwenye akaunti kuwa ni yake. Sasa mwenye nayo kapatikana na kwa hukumu ya ICSID ndiye anastahili kulipwa ile pesa. Sasa kwanini huyo Singasinga mwizi asirudishe pesa yetu na aadhibiwe kwa mujibu wa sheria za nchi yetu? Kwa nini tuendelee kupoteza pesa kwa jambo ambalo linaeleweka hatima yake?

IPTL wasitulaghai kuwa wanaunga mkono TANESCO kukata rufaa hata kidogo. Lazima wao watake iwe hivyo kwa sababu ile hukumu ni mwiba kwao. Kwanza wanatakiwa kurudisha pesa waliojizidishia ambayo wanaendelea kutunyonya Watanzania hadi leo. Pili hiyo mitambo inastahili kutaifishwa baada ya kumning'iniza Harbinder Seth mahakamani kwa makosa mbalimbali.

Mheshimiwa Rais tunahitaji hatua madhubuti zichukuliwe mara moja dhidi Harbinder Seth na mnyororo mzima wa watu waliomsaidia kukwapua pesa za ESCROW hasa awajibike kuilipa benki ya Standard chartered ya Hongkong. Kukata rufaa ni kuendelea kupoteza pesa za Watanzania.

Kuna wahusika waliopiga pesa wanataka kutupoteza na wengine wako serikalini na bungeni. Rais wetu JPM chukua ile orodha yao uwashughulikie kwanza ili upate pesa za kuwalipa hao Stan Chart Bank. Usiache jiwe juu ya jiwe na tuko nyuma yako.
 
Nahisi ugumu unaanzia kwenye bajeti ya kampeni maana sidhani kama mfalme aliiepuka hii minoti wakati akipigania kuingia mjengoni.
 
Hili deni litalipwa na watanzania. Huyo singasinga ni sura tu, ila hiyo hela imechukuliwa na watanzania wenzetu na imesaidia kwenye kampeni.
Hakuna atakayemgusa Singasinga.
 
Hii rufaa ni figisu tu, wanajua wanachokifanya. Zili push ups majukwaani aliyekuwa wanapigiwa ni wapinzani na siyo mafisadi. Masikini Tanzania, i wish hayati JKN angekuwepo, pamoja na kwamba alistaafu lakini bado alkuwa na ubavu wa kuyapigia kelele maovu. Nchi imeshikwa na genge la waovu wachache kwa manufaa yao, UJINGA ni jipu baya sana.
 
Habari wana JF

Nianze kwa kuonesha msimamo wangu juu ya mchakato wa TANESCO kutaka kukata rufaa hukumu iliyotolewa ICSID. Mimi siungi mkono ukatwaji wa rufaa hiyo kwa sababu zifuatazo:

Sioni TANESCO kukata rufaa wanatafuta nini! Je, wanamtetea Harbinder Singh Seth ambaye amekwapua pesa ambazo si za kwake? Singasinga huyu aliishaihakikishia serikali kuwa hakuna mtu mwingine atakayekuja kudai ile pesa iliyokuwa kwenye akaunti kuwa ni yake. Sasa mwenye nayo kapatikana na kwa hukumu ya ICSID ndiye anastahili kulipwa ile pesa. Sasa kwanini huyo Singasinga mwizi asirudishe pesa yetu na aadhibiwe kwa mujibu wa sheria za nchi yetu? Kwa nini tuendelee kupoteza pesa kwa jambo ambalo linaeleweka hatima yake?

IPTL wasitulaghai kuwa wanaunga mkono TANESCO kukata rufaa hata kidogo. Lazima wao watake iwe hivyo kwa sababu ile hukumu ni mwiba kwao. Kwanza wanatakiwa kurudisha pesa waliojizidishia ambayo wanaendelea kutunyonya Watanzania hadi leo. Pili hiyo mitambo inastahili kutaifishwa baada ya kumning'iniza Harbinder Seth mahakamani kwa makosa mbalimbali.

Mheshimiwa Rais tunahitaji hatua madhubuti zichukuliwe mara moja dhidi Harbinder Seth na mnyororo mzima wa watu waliomsaidia kukwapua pesa za ESCROW hasa awajibike kuilipa benki ya Standard chartered ya Hongkong. Kukata rufaa ni kuendelea kupoteza pesa za Watanzania.
There is something beyond singasinga mbona kila kitu kipo wazi....pushup hzo n shidaaaa
 
Umenena vizuri. Kwa kuongezea serikali isiendelee kumlipa Singh daily capacity charge kuanzia sasa au tuilipe kwenye escrow nyingine.
 
Back
Top Bottom