Sikubaliani na Sababu za kusitisha Muswada! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikubaliani na Sababu za kusitisha Muswada!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hmaster, Apr 16, 2011.

 1. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hi Wanajf! Ninakubaliana kabisa na kuondolewa hati ya dhalula iliyoambatanishwa na muswada wa mabadiliko ya katiba ili watu wengi zaidi wapate fulsa ya kuuchangia. Jambo ambalo bado sijalidhika nalo na maelezo ya spika wa bunge ni pale alipoorodhesha masuala ya kuzingatiwa HUO ni:
  1. Kuweka utangulizi mzuri ili kila mtu aelewe nia ya muswada
  2. Kuandikwa kwa kiswahili
  3. Kuchapishwa ktk magazeti
  4. Kutoa fulsa kwa watu wengi kuchangia.
  Hapo kwenye red, je muswada utakaoendelea kujadilwa ni uleule ila ukiwa kwa kiswahili na mabolesho ya utangulizi au unaandikwa muswada mwingine? Nawaomba mnijuze huenda bado ni mchanga ktk taaluma ya miswada. KARIBUNI!:behindsofa:
   
 2. m

  mapambio Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hukumwelewa vzuri!...Utaletwa mwingine..unadhani hawaogopi kuhaibika?
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Leo ktk taarifa ya habari wameonyesha sehemu ya hotuba ya Nape akisema kuwa CCM ndiyo iliyoishauri serikali kwenda kuandika upya muswada wa katiba. Nape watanzania tunakuheshimu kwani umewahi kuwa msema ukweli. Sasa nakuomba wewe ama hapa JF au sehemu nyingine, uthibitishe kuwa uliyosema ni kweli. Hivi wana JF, ni kwel kuwa ccm ndio waliishauri serikali iuondoe muswada bungeni? Hivi ni halali kwa akina nape kuzunguka nchini wakijigamba kuwa ndio wamefanikiwa kuishauri serikali iuondoe muswada bungeni?
   
 4. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ukiwa ndani ya ccm unawehuka!
   
 5. Pawaga

  Pawaga JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 1,246
  Likes Received: 684
  Trophy Points: 280
  CCM wanaelekea kaburini 2waache waende salama maana wanaweweseka kama vichaa
   
 6. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Kweli nimeamini hata nyoka akijivua gamba bado sumu ni ileile,Nape 120 ileile Kama Makamba
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hivi hizo ndizo kazi za mkuu wa wilaya .... au ndiyo misuse of government revenues
   
 8. L

  Lusambara Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape amesema kuwa wao ndio walioishauri serikali iondoe mswada wa katiba ambao ulikuwa umepelekwa kwa hati ya dharula.

  Kama kweli CCM ndiyo imeshauri serikali iuondoe, nina maswali ambayo inabidi tujiulize

  1 - Mswada huo umetungwa na nani au na serikali ya chama gani? kiasi cha chama tawala CCM kuona una makosa ambayo yamefanywa na serikali ya chama hicho kilichotunga na hivyo ccm ikashauri utolewe?

  2 - Mswada huo kabla ya kusomwa ulijadiliwa na BARAZA LA MAWAZIRI, Ina maana hata mawaziri nao ambao waliujadili hawakuona makosa mpaka akina Nape walipoona na kutoa ushauri?

  3 - Kama Nape na wenzake wameona utolewe? Wameshafanya hivyo mara ngapi tangu uhuru na miswada mingapi ilisomwa kwa lugha ya kiswahili ( Miaka hamsini sasa)?

  4 - Ni mbunge yupi wa CCM ambaye kwa uwazi kabisa ameonyesha kuukataa mswada huo bila kujificha?

  UKWELI NI KWAMBA VYAMA VYA UPINZANI VIMEWEZESHA MSWADA HUU KUONDOLEWA NA WALA SI CHAMA TAWALA AMBACHO SERIKALI YAKE NDIYO ILIYOLETA MSWADA HUO.
   
 9. Shidende

  Shidende Member

  #9
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  ukishapewa tu cheo ccm ni lazima uwe mropokaji!ndicho anacho prove Nape...!
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  nape ni amekurupuka sana, anadhani kuongea sana ndiko kuna ipa credit ccm. hili alilozungumza hata mtu wa kawaida anatambua kuwa si kweli. ccm na serikali yake ndio waliopeleka muswaada ule mbovu kupindukia. kwa style hii c kwamba anakiokoa/kukijenga chama chake bali kubomoa zaidi
   
 11. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hilo sio la kubishania tena, Nape yupo kwenye mchakato wa kujimaliza tu... tatizo la ccm ni sikio la kufa, wameamua kufia kwenye siasa zao za PROPAGANDA kwa kila kitu hata wakati maisha ya Taifa yanapokuwa hatiani, kisa??? kushiba madaraka!! Nape atueleze kilichosababisha Prince Bagenda ashindwe kumaliza "hoja" zake kwenye kongamano la katiba kule UDSM? Pia atuambie kilichomkuta Tambwe Hizza pale Karimjee? Na je hao wawili walikuwa wanawakilisha mawazo yao binfsi au ya chama?? Masikini CCM....
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu Nape si ndio alipewa ukuu wa Wilaya hivi karibuni?. Na kwa sheria iliyopitishwa na Bunge leo hii Dodoma, Nape, kama mkuu wa Wilaya atachunguza 'mis-conducts' katika uendeshaji wa shughuli za kimahakama!

  Sasa kama Nape anakuwa hodari wa propaganda hata kwenye mambo ya wazi kabisa kama hili la katiba atawezaje kusimamia utendaji wa kazi za kimahakama?

  Kuna vitu vichache tu Nape na wenzake wanatakiwa wazingatie
  1. Katiba mpya haipo kwenye MANIFESTO YA CCM 2010-2015. Haipo!

  2. Chadema katika manifesto yake 2010-2015 na hata kwenye kampeni zake walisema wazi wazi mara elfu lela ulela kuwa watahakikisha kuwa MCHAKATO wa kupata katiba mpya unaanza ndani ya siku 100. (Nasisitiza MCHAKATO wa kupata katiba mpya na sio huu upotoshwaji kuwa chadema walisema watatengeneza katiba mpya ndani ya siku 100)

  3. Wakati Chadema wanaanza kupaza sauti ya kutaka katiba mpya baada ya uchaguzi Mh. Celina Kombani na Mwanasheria mkuu kwa nyakati tofauti walisema 'hakuna haja'ya kuwa na katiba mpya ila marekebisho yanaweza kufanyika!

  4. Yote tisa, kumi muswada umeletwa bungeni kwa hati ya 'dharura' huku ukiwa umeandikwa kwa lugha ya kiingereza.

  5. Chadema na wadau wengine (sio CCM-Bara) wameukosoa vilivyo na hatimae kwa nguvu ya kujivua gamba muswada umerudishwa kwa ajili ya maboresho.

  Kwa mtitiriko huu ni wapi hasa Nape anaweza kutoa credit kwa CCM? Kama hii timu mpya uliyoundwa itawekeza kwenye hizi strategies za kizamani badala ya kuwa factual then Chadema wakae mkao wa kula maana Tafrija yaja. Dot.com generation will not be swayed with S.L.P strategies. wrong move!
   
Loading...