Sikubaliani na Pinda kuhusu Dowans

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Kauli ya waziri mkuu Pinda aliyoitoa jana kupitia Star Tv kwamba serikali itafuata msingi wa utawala wa sheria wa dhana ya utawala bora kuilipa dowans sikubaliani nayo. Kwanza nampinga Pinda kwa kuangalia utawala bora katika ngazi ya juu tu kuhusu kesi inayoamuliwa na taasisi ya kimataifa ya biashara kati ya Dowans na Tanesco. Pili nampinga Pinda kwa mtazamo wake kuwa anayetarajiwa kulipa ufisadi wa Dowans siyo serikali bali ni sisi wananchi- raia wa Tanzania. Tatu, Pinda anakwepa ukweli kwamba rushwa si mojawapo ya misingi ya utawala bora.

Pinda amepotoka kwa sababu haiwezekani auone utawala wa sheria katika taasisi ya kimataifa inayoamua kesi wakati huohuo anakwepa ukweli kwamba kimsingi mkataba kati ya Dowans na Tanesco au wananchi wa Tanzania si halali kisheria- ni wa kifisadi. Dowans ilirithishwa mkataba feki na kampuni hewa ya Richmond. Utawala bora wa sheria unatoka wapi katika hali hii? Pinda pia anatundanganya watanzania eti serikali ndiyo inayotarajiwa kulipa ufisadi wa Dowans hali akijua pesa za serikali zinakamuliwa kutoka kwetu wananchi, hatutaki ufisadi huu. Mwisho, Pinda hawezi kuzungumzia utawala bora katika mkataba anaojua fika kuwa ni wa rushwa. Rushwa ni kipimo cha kukosekana kwa utawala bora. Lowasa, Msabaha na karamagi walijiuzuru baada ya bunge kubaini rushwa ilitumika katika kuipa Richmond kazi ya kuzalisha umeme. Pinda anajua kuwa Richmond haipo katika mafaili ya kampuni zilizowahi kusajiliwa na Brela hapa Tanzania. Uhalali wa kisheria na utawala bora katika mkataba wa Dowans unatoka wapi mzee Pinda?

Pinda asitufanya wananchi hatuelewi. Anataka kuhalalisha ufisadi wa Dowans na kutubebesha wananchi madeni ya kifisadi kwa manufaa ya kuwalinda mafisadi wa serikali ya CCM katika mkataba wa Richmond na Dowans. CCM ikihalalisha mzigo huu kwa wananchi itaendelea kukabiliana na hasira kali za wananchi, wananchi tumechoka kunyonywa na kunyanyaswa na CCM.
 
Pinda hana lolote ni wale wale bonge la mwizi, watetezi watakuja na kusema ni mtoto wa mkulima lakini yeye ndiye anawalinda wezi wa pesa za walipa kodi na sasa hivi wamemtuma aje kusema serikali italipa WEZI. Maajabu haya. Ndio serikali ya kwanza duniani kuwalipa Wezi.
 
mnashangaa nini? Kipi kipya?
Au mmesahau juzi alikataa ndinga akidai la beimbaya na hakusema lirudishwe kwa vendor wala walionunua wachukuliwe hatua gani?
Unamshangaa pinda aliyeishia kutoa machozi bungeni wakati watu walikuwa wanaendelea kuuawa hadi yule dada/mama wa BBC akawajua wauaji lakini system ilikuwa haijawajua?
Endeleeni kumshangaa Pinda!
 
Mafisadi wana kila sababu ya kusherhekea ushindi walioupata. Kwa kukubali kulipa ni kuitambua Dowans au Richmond ambayo kimsingi haipo au ina mawakala wa kifisadi. Ufisadi si tu kupokea pesa tu bali ni pamoja na kubariki ufisadi. Katika kushiriki ama kutoshiriki, viongozi tunawapambanua kwa kauri zao.
 
Aliporudishwa Pinda uwazir mkuu, nilitapika. Lile li jamaa halina kipya. Ni mwizi tu kama wengine. Sionagi tofauti kati ya mwizi na mlinda mwizi
 
Aliporudishwa Pinda uwazir mkuu, nilitapika. Lile li jamaa halina kipya. Ni mwizi tu kama wengine. Sionagi tofauti kati ya mwizi na mlinda mwizi
Hahahahahahaaaaaa
Pole ndugu kwa kutapika!
Vumilia tu tutafika!
 
Anachobore pinda ni kutokua jasiri.personally he is a good person bt he can not stand for what he believes in.in short pinda ni kunguru and he does not qualify 2 be the pm.nway serikali ya kifisadi ya jk inamuona wa maana coz haingilii maswala yao,anabaki kulia tu kama zuzu.in reality pinda stinks jst like the rest of them
 
Atakuwaje jasiri wakati kupewa uPM kwake ni ngekewa? Lazima awe 'yes man' vinginevyo tajiri yake atampiga chini.
 
Kwa mtu mwenye akili anaona wazi kwambe maudhui mazima ya mkutano wa Pinda na wahariri wa magezeti, ilikuwa ni kujenga mazingira muafaka ya ulipaji wa hizo fedha halamu. Mengine yote aliyoyazungumza hayakuwa na maana yeyote. Chukua ili suala la katiba; inawezekanaje waziri mkuu mzima ukaitisha mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia mawazo yako. Yeye kama mtendaji mkuu wa serikali tulitegemea angelitoa msimamo wa serikali juu ya jambo hilo; badala yake akatoa mawazo yake binafsi ambayo alisema atayawasilisha kwa rais kwa uamuzi. Kama hivyo ndivyo, kwanini basi hasingelisubiri akapata muafaka wa rais. Baya zaidi hata hakuwa na uhakika ni mawazo yapi apeleke kwa rais. Kama itakavyokumbukwa, bado hakuwa na uhakika kama marekebisho ya katiba yanayohitajika ni ya kuandika katiba mpya au kurekebisha vifungu fulani fulani kwa katiba iliyopo. Hivyo Pinda anapashwa aambiwe wazi kwamba kwa mujibu wa "penal code" muarifu na yule aliyemsaidia huyo muarifu kufanisha dhuluma yake, mbele ya sheria wote ni waarifu kwa kiwango kile kile.
 
Kama hali ndiyo hiyo bunge liunde kamati ya kuchunguza sababu za nchi kuingia hasara ya kulipa Dowans bilioni 185. Matakeo yake lazima Lowasa asafishwe. Hapo mpo?
 
NILIAHA MSHUHA SIKU NYINGI, Washajua udhaifu wake sasawanamtumia kama MUHURI.

HIVI AKIWA RAISI ITAKUWAJE? JAMAA WANAWEZA KUMPIGIA DEBE AKAWA RAISI MAANA YEYE SI MZEE WA KIMYA NA KULIA TU!
 
Dah, wakati mwingine humu jamvini hunifanya nicheke peke yangu, mfano huyo nyau hapo na 8 ndo anafanyaje? Good stuff. Ni ngumu sana Pinda kufanya chochote pale alipo, jamaa wakuwabana JK ndo mshikaji sasa unaanzia wapi. Hafu ukizingatia PM mwenyewe ni mtoto wa maskini ambaye siyo jeuri.
 
Hapa ndo nitaona ujasiri wa Samuel Sitta. Je atajiuzulu toka Serikali inayotenda kinyume na ushauri wake?
 
Pinda amechemsha,alitakiwa aseme hatua walizoishachukuliwa waliotuingiza ktk huo mkataba. Maazimio ya bunge haikuwa kuvunja mkataba pekee.
 
Kauli ya waziri mkuu Pinda aliyoitoa jana kupitia Star Tv kwamba serikali itafuata msingi wa utawala wa sheria wa dhana ya utawala bora kuilipa dowans sikubaliani nayo. Kwanza nampinga Pinda kwa kuangalia utawala bora katika ngazi ya juu tu kuhusu kesi inayoamuliwa na taasisi ya kimataifa ya biashara kati ya Dowans na Tanesco. Pili nampinga Pinda kwa mtazamo wake kuwa anayetarajiwa kulipa ufisadi wa Dowans siyo serikali bali ni sisi wananchi- raia wa Tanzania. Tatu, Pinda anakwepa ukweli kwamba rushwa si mojawapo ya misingi ya utawala bora.

Pinda amepotoka kwa sababu haiwezekani auone utawala wa sheria katika taasisi ya kimataifa inayoamua kesi wakati huohuo anakwepa ukweli kwamba kimsingi mkataba kati ya Dowans na Tanesco au wananchi wa Tanzania si halali kisheria- ni wa kifisadi. Dowans ilirithishwa mkataba feki na kampuni hewa ya Richmond. Utawala bora wa sheria unatoka wapi katika hali hii? Pinda pia anatundanganya watanzania eti serikali ndiyo inayotarajiwa kulipa ufisadi wa Dowans hali akijua pesa za serikali zinakamuliwa kutoka kwetu wananchi, hatutaki ufisadi huu. Mwisho, Pinda hawezi kuzungumzia utawala bora katika mkataba anaojua fika kuwa ni wa rushwa. Rushwa ni kipimo cha kukosekana kwa utawala bora. Lowasa, Msabaha na karamagi walijiuzuru baada ya bunge kubaini rushwa ilitumika katika kuipa Richmond kazi ya kuzalisha umeme. Pinda anajua kuwa Richmond haipo katika mafaili ya kampuni zilizowahi kusajiliwa na Brela hapa Tanzania. Uhalali wa kisheria na utawala bora katika mkataba wa Dowans unatoka wapi mzee Pinda?

Pinda asitufanya wananchi hatuelewi. Anataka kuhalalisha ufisadi wa Dowans na kutubebesha wananchi madeni ya kifisadi kwa manufaa ya kuwalinda mafisadi wa serikali ya CCM katika mkataba wa Richmond na Dowans. CCM ikihalalisha mzigo huu kwa wananchi itaendelea kukabiliana na hasira kali za wananchi, wananchi tumechoka kunyonywa na kunyanyaswa na CCM.

In a country where the freemasons are the rulers what do you expect.Tusubiri tu kuliwa nyama na kutolewa kafara!
 
Sijawahi kusikia hili la utawala bora wa kulipa deni la kampuni ambayo iliingia nchini kwa kuidanganya Serikali. Tukumbuke kwamba kampuni hii ilidanganya kwamba HQ yake iko Houston, Texas na ina utalaamu katika kufua umeme. Hii haikuwa kweli bali ilikuwa ni kamuuni ya ndani kifisadi ya ndani ya briefcase na haikuwa na utaalamu wowote ule katika kufua umeme.

Pamoja na kampuni hii kupewa mkataba ule wakati nchi ikiwa imegubikwa kwenye giza la kutisha haikuweza kufua hata tone moja la umeme kwa visingizio mbali mbali.

Sasa iweje kampuni ya kitapeli/kifisadi ambayo iliidangaya Serikali leo hii ivune shilingi 185 billioni na Waziri Mkuu ambaye anatakiwa asimame kuhakikisha pesa za walipa kodi haziguswi hata senti moja leo atoe kauli eti kwa kufuata utawala bora basi Serikali itawalipa Richmond/Dowans pesa ambazo hazistahili.

Utawala bora huu kama unafuatwa mbona wale Wazee wa jumuiya ya Afrika Mashariki bado wanazungushwa kwa zaidi ya miaka 30 katika kudai haki ya mafao yao toka EAC? Utawala bora kama kweli upo kwanini Serikali haitaki kuwalipa Wafanyakazi kima cha chini ambacho kimeombwa na Jumuiya ya Wafanyakazi kinachoendana na hali halisi ya ghrama za maisha? Au huu utawala bora unakuwa na umuhimu pale tu ambapo mafisadi kama Rostam wanapohusika ndiyo Serikali inaona umuhimu wa utawala bora? Hakuna utawala bora wowote kwa kuilipa kampuni iliyoingia nchini kifisadi na kupata mkataba kifisadi huu ni wizi wa mchana kweupe.

Pinda acha usanii! Tetea maslahi ya Watanzania badala ya kutetea maslahi ya Mafisadi. Hukupewa uPM ili kutetea maslahi ya mafisadi bali kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom