Sikubaliani na migomo ya wanafunzi Tumaini na SAUT juu ya ada!

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,062
79,089
kwa kuangalia harakaharaka migomo ya wanafunzi Tumaini na SAUT inaweza kuwa na maana lakini tukiangalia gharama za uendeshaji sidhani kama kutoa ada ya milioni 2.5 ni kubwa namna hiyo kama hawa wakuu wanavyotaka kutusadikisha! Hivi vyuo ni vya taasisi binafsi zenye malengo ya kutoa elimu bora wakati huo huo kuboresha huduma na kupanua uwezo wao! Na ninaamini kila centi inayoongezwa kwenye ada zao ina mipango maalum katika bajeti ya hivi vyuo ikiwemo kuajiri waalimu wapya (CAG anaweza kuhakikisha hilo)! Ikumbukwe bado kuna uhaba mkubwa wa waalimu kwenye hivi vyuo!

Sasa ningewashauri hawa wanafunzi waelekeze maandamano yao kwa serikali ya JK kwa kuwa ndiyo sababu a kupanda kwa gharama za uendeshaji kuanzia umeme, chakula hata mafuta ambavyo vinaadhiri uendeshaji na hata kiasi anachopata mwalimu ambaye naye mwishowe anadai mshahara upande. Vilevile hizi taasisi za vyuo wana mipango yao yaani kuboresha na kuongeza uwezo wa kufundisha na sidhani kama itakuwa ustaarabu kushusha tu kwa vile watu fulani wanataka kusoma dezo je wadogo zenu wanaofuata hawana haki ya kukuta hizo huduma hapo? na je hawana haki ya kupata nafasi zaidi katika hivyo vyuo?

Tutumie busara kwenye hili millioni 2.5 si kiasi cha kulalamika namna hiyo mpaka migomo ukizingatia zinalenga katika kuboresha huduma katika hivyo vyuo!
 
Huko mijini mambo mazuri naona. Huku kijijini hilo pesa la kuongezea wanetu hatuna. mambo magumu. elefu ishirini ya ada ya sekondari twaomba mjini kwa ndugu na jamaa!
 
Jambo ambalo hujaelewa ni kwamba:-
Tumaini na SAUT walipeleka Bodi ya mikopo kuwa ada yao ni shs 2.5mil. Mikataba wanafunzi na Bodi inaonyesha watalipiwa kiasi hicho. Walisahau kuweka asilimia ya ongezeko ili Bodi wa-budget. Sasa wanapoongeza waendelee na wale wanaoingia na sio wale walio tayari chuoni maana Bodi haitambui ongezeko na wazazi hawana cha kuongezea, kwa nini wasigome.
Kwa wale wapya wala Bodi haikukataa wanapewa kama chuo inavyowasilisha ada zao. Mzozo uko hapo.
Wawe waaangalifu na mikataba ndio chanzo cha mgongano.
 
kama bodi imesahau kuweka nyongeza tatizo la nani? si wewe uwapangie eti watoze kwa wanafunzi wapya na si wa zamani! hamna mkataba unaosema hivyo katika nchi hii yenye inflation ya overnight! hali halisi ya kupanda kwa gharama ndo inaamua otherwise kuna vyuo vya kata unaweza enda kama hujui nani ni wakumgomea!
 
Hawa wanafunzi wanahaki ya kuvigomea vyuo kwani kimsingi Bodi inatoa flat rate kwa vyuo sasa hawa wa vyuo binafsi huwa wanapandisha ada wakijua Bodi itatoa tu pesa, Ndugu milioni mbili kwa Tanzania n pesa kubwa sana, najua huwezi ona lakni kiukweli ni ada kubwa sana. maana kuna wale ambao bodi haiwapi pesa unategemea nini?
Mbeki alipoishauri serikali itenge mgodi mmoja kwa ajili ya kushughulikia elimu, barabara na afya serikali ilitia pamba maskio, sasa wawajibike kwa yanayotokea.
Serikali haikupima kujua unapopandisha gharama flan huathiri huduma nyingi.
 
Nijuacho mimi kuna vyuo ada zao huwa zipo fixed (unaposign contract fee statement yako inaonesha kiasi utacholipa kuanzia 1st mpk final year).
pia kuna vyuo ambapo utakuta vimeandika "fees are subject to change".
SWALI: SAUT, Tumaini agreement inaonesha nini kati ya hivyo juu nilivyoweka?? ukishayajua haya ndio utajua mchawi ni nani chuo au mwanafunzi.
Note: chuo chochote makini ni lazima kispecify kati ya hayo mawili.
 
Nafikiri hivyo vyuo wako sahihi. Tukumbuke kwamba hivyo ni vyuo vya binafsi siyo taasisi za umma hivyo kujiendesha kwao ni kutokana na ada za wanachuo. Kama mtu huna uwezo wa kumpeleka mtoto wako huko hiyo itakuwa imekula kwako. Tusitake kuwalazimisha washushe ada eti walingane na vyuo vya umma wakati hawapati ruzuku yoyote katika kuendesha vyuo vyao. Kama wanatoa elimu bora hiyo yote ni kutokana na ada inayolipwa na wanafunzi.

Tuangalie tu mfano wa shule hizi zilizofumka sasa hivi al-maaruf English Medium ada zao ni balaa lakini tutafanyaje? Hatuna jinsi isipokuwa ni kukabiliana nao tu kwa wenzangu ambao hatuna uwezo ndo hao tunaishia kuwapeleka watoto wetu kwenye shule za serikali ambazo hali yake tunaifahamu wenyewe. Hivyo ni vyema tu wa-TZ tukakubali kuwa kama huna uwezo wa kukabiliana na hiyo ada ya hao jamaa usiende huko. Waachie wenye uwezo wao waende huko, tusitatake kulazimisha mambo ambayo hayana tija kwa vyuo hivyo. Hebu hao wanachuo wafikrie kama ukifika wakati uongozi ukaamua kuwafukuza nani atapoteza? Ni vyema tukawa tunaangalia hata upande mwingine wa shilingi siyo kushinikiza tu!! Those are private entities, we should value their contribution!!
 
Tumain na Saut ni wezi wa pesa za umma kwa kupandisha ada ili wachume zaidi kutoka serikalini..
 
Bwana we..maandamano ni maandamano tu na vilevile migomo haijalishi chuo kinaendeshwa na nani
 
Wabongo tunajua kutafutana uchawi wakati mchawi wetu tunamjua! CCM na serikali yake! halafu kuna kawaziri kamoja kalishawahi kuamuru ati bei zisushwe bila kuiamuru serikali yake ishushe ukali wa maisha pia! bado tumejawa na hulka ya ujamaa tunataka quality education at a free price!
 
Tumain na Saut ni wezi wa pesa za umma kwa kupandisha ada ili wachume zaidi kutoka serikalini..

mbona SAUT hatujagoma bana acheni kuwackiliza waandishi ambao hawajui maadili yao wanaandika bila kuwa na solid evidence....
 
Wewe mpuuzii kweli yaani unashangilia ada iwe kubwa? Kama umezaliwa familia tajiri ama ya kupata fedha kwa ufiosadi usidhani ni wote! Toa kichefuchefu chako hapa. Wazazi wanaumia wewe unaleta madudu yako hapa! Yaani ntafanya jitihada mpaka nikujue
 
Bajeti za Harusi zinazidi hata mara tatu ya hapo, kulipa ada mnaona shida!

sasa wewe bwana mkubwa inakuaje,kwani hyo budget ya harusi anatoa mtu mmoja kama ada,just be critical thinker and learn how to argue intelligently,otherwise shut up and zzzzz.
 
Back
Top Bottom