Uchaguzi 2020 Sikubaliani na imani hii potofu ya kisiasa hasa wakati wa Uchaguzi kama huu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,218
25,629
Kila unapofika wakati wa Uchaguzi kama huu, yanasemwa na kufanywa mengi. Moja kati ya maneno yanayosemwa sana ni kugawana/kugawa kura kwenye Uchaguzi. Kauli hii ndiyo imekuwa hoja hata ya kuwataka wapinzani waungane.

Pamoja na kukiri kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, kwenye Uchaguzi wa hapa nchini jambo hilo halipo. Kwenye Urais, Ubunge na Udiwani wananchi humchagua mtu wamtakaye kuliko chama chake. Huchagua kipenzi chao na wanayemwamini kuwafanyia kazi za Urais, Ubunge na Udiwani.

Kuna mifano na shahidi mbalimbali kuwa wingi au uchache wa wagombea haumzuii atakiwaye kushinda. Ushahidi wa haraka na wa karibu zaidi ni kilichotokea kwenye Kura za Maoni ndani ya CCM na CHADEMA. Waliotakiwa, bila kujali wingi wa wagombea, wameshinda kwa kishindo.

Kwangu mimi, msamiati wa kugawana au kugawa kura siuamini wala siukubali. Mgombea anajiuza mwenyewe kwa sifa, sera na kukubalika kwake. Hata wagombea wakiwa mamia, atakiwaye ataibuka mshindi kwa kishindo na kila mgombea atapata asilimia za kura anazostahili.

Kama kuungana mkono kwenye uchaguzi kwa vyama vya siasa kuwe ni kwa sababu nyingine. Si hii ya kugawana au kugawa kura. Humuhumu duniani, kuna chaguzi zilizokuwa na makumi ya wagombea na washindi wakavuka asilimia sitini za kura(ushindi wa Hayati Mkapa na Mzee Kikwete). Yaani, jumla ya kura za wengine zote hazifiki asilimia hamsini.

Kukubalika kwa mgombea hakutegemei kuungana kwa vyama. Matendo na maneno yake yatambeba na kumtetea uchaguzini.
 
Walishaungana wakashindwa.
Kung'ang'ania kuungana ni kukiri kwamba hakuna chama chenye uwezo wa kupambana na CCM chenyewe.
 
Back
Top Bottom