Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

Naamini viongozi wa CDM.. Ni watu makini, wenye upeo kusoma alama za nyakati na upepo wa kisiasa. .. Naunga mkono maamuzi magumu waliochukua. Poleni sana ccm, mlilia sana lowassa asihame kwa sababu mnajua ni mtu hatari kwenu kwa sababu anajua mbinu zenu zote hata zile za goli la mkono.. Mnahofia kuumbuka, mwaka huu hilo goli la mkono hakuna tena.. Yupo golikipa wa kudaka. Dead ccm..
 
Zero torelance ya rushwa kwa CHADEMA ambayo ni mshirika mkuu wa UKAWA inamkataa Lowassa kujiunga na CHADEMA na UKAWA kwa ujumla wake. Akihutubia katika mkutano wa siasa pale mwembe yanga, mwaka 2007, Dr. Slaa huku akisaidiana na Tundu Lissu, waliwataja mafisadi 11 katika nchi yetu. Orodha ya Dr. Slaa ya mafisadi ilijumuisha jina la Lowassa. Katika mkutano wa MwenbeYanga, CHADEMA ilitangaza zero tolerance kwa rushwa na ufisadi.

Tangu wakati huo, vita ya kupambana na ufisadi imekuwa sera kuu ya CHADEMA. Hata katika chaguzi za ndani za CHADEMA, rushwa haikubaliki kabisa na ni kigezo cha disqualification kwa wagombea. Sera hiyo kwa kiwango kikubwa imeifamya CHADEMA ipendwe na wanchinwengi na hivyo kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Hakuna hata siku moja ambapo CHADEMA imetangaza kuachana na sera yake ya kupambana na rushwa na ufisadi. Jaribio lolote na kumwingiza Lowassa CHADEMA kama mgombea ubunge au urais lina maana moja tu kwamba CHADEMA inasitisha rasmi vita dhidi ya ufisadi. Hivyo faida ya kisiasa ambayo CHADEMA na UKAWA ilikuwa nayo kupitia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi itakuwa imefikia tamati. Hakuna mantiki yoyote ya CHADEMA na UKAWA kupigana dhidi ya rushwa na ufisadi kama vile wizi wa ESCROW, mikataba ya kifisadi ya Gas na madini na nk. huku wakimkumbatia Lowassa katika chama cha CHADEMA na UKAWA. Kwa ufupi, mantiki ya vita dhidi ya ufisadi inakufa na hivyo CHADEMA na UKAWA hawatakuwa na tofauti yoyote ya kisera na hivyo CHADEMA NA UKAWA watafanana na CCM.

Huu ni ukweli mchungu ambayo CHADEMA na UKAWA inabidi wauone. Kuna hatari ya CHADEMA na UKAWA kukosa kuungwa mkono na wanchi kama watafanya kosa la kumfanya Lowassa kuwa mgombea ubunge au urais kupitia CHADEMA au UKAWA. Kiukweli wataua visibility ya vipaji vya wanasiasa waliochipukia kama vile Mnyika, Tundu Lissu, Halima Mdee, Wenje, Msigwa, Vincent Nyerere, n.k. Hakuna hata siku moja ambapo CHADEMA wamewahi kumwondoa Lowassa kwenye List of shame. Hawajawahi kumsafisha, na dhana hii ya kusafishana kwa dodoki, imepingwa sana na CHADEMA na UKAWA yake. Kuna vyama viko kama mafisi, vinasubiri CHADEMA na UKAWA wafanye kosa la kumkumbatia Lowassa. Vyama hivyo ambavyo ni kama mafisi wanaosubiri mkono wa binadamu udondoke ili waule vinajumuisha chama kile cha wasaliti waliotoka CHADEMA, yaani assosiation of cowards and traitors (ACT).

Umelipwa sh ngapi
 
hata slaa alikuwa ccm alipokatwa akaenda cdm

Aisee,inamaana ni kichaka cha wapigaji

Lazima tukubali asiekubali kushindwa si msindhani na ukiona anapapatika ujue kuna maslahi fulani kimtandao.

Na ndio maana hata baadhi ya wapiga dili weengi sana waliumia Lowasa kuachwa,na baadhi yao walitegemea Uwaziri ndio hao atakaosepa nao.
Aisee madaraka matam kweli,sasa hivi mtu anae force uongozi huyo kweli kiongozi bora?
 
Mheshimiwa EDO NGOYAI LOWASA mzee wa maamuzi magumu, nakupa BIG UP MZEEEE WE JEMBE MZEEEEE INGIA UKAWA NA sisi wote tunatia TIMU hukohuko na SASA ni safari YA UHAKIKA NA SI MATUMAINI TENA ....MWALIMU ALISEMA TUSIPOPATA DIRA YA KWELI NDANI YA CCM TUTAITAFUTA NJE YA CCM na AKAONGEZA CCM SIYO BABA WALA MAMA YAKE mwacheni mzee wetu TIMU EDO OYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
Umeandika vizuri lakini kuna jambo moja unasahau. Kwa Mungu hakuna mdahambi asiyesamehewa. Pitia kwa kina the list of shame. Haikuwa orodha ya majina tu, kila aliyetajwa jina ilielezwa ni kwa nini allitwa sababu. Ukiangalia katika ile list ufisadi wa Lowasa ulitajwa kuwa unahiska na kampuni ya City Water, iliyopewa tenda ya kusambaza maji katika mkoa wa Dar es Salaam. Wakati huo Lowasa alikuwa waziri wa fedha. Kama unakumbuka ni Lowasa aliyevunja ule mkataba, na kama utakumbuka vyema City Water iliishtaki serikali mahakamani, tena nje ya nchi. Serrikali ilishinda kesi na kukwepa kulipa mamilioni ya fidia. Lowasa alijichomoa automatically kwenye list oa shame. Mpaka leo CDM wamekaa kimya kabisa na huu ni udhaifu, walitakiwa wakiri wakati ule kuwa Lowasa amejisafisha kwa kuvunja mkataba na CITY water.

Come Richmond saga, hii halikuibuliwa na CDM hata siku moja. Hii ilikuwa ni vita ya wanamtandao waliokosana katika safari, wakaanza kuparurana. CDM kama ilivyo kwa watanzania wote walikuwa ni washabiki tu wa vita ya maccm wenyewe. Loawasa akapigwa mweleka, akajiuzulu, mbiu ikapigwa nchi nzima kuwa ni fisadi, waliopiga mbiu hii ni akina Sendeka, Kilango, Sitta, Mwakyembe, Nape na wakaunda umoja kabisa kuhakikisha kuwa wanamzika kisiasa. Hapa Lowasa alikuwa anajipigania mwenyewe kujisafisha huku akiogopa kwani kujisafisha kwake na Richmiond ni kumpaka mtu mwingine matope. Lowasa amekuwa na busara sana asimguse mwenye Richmond.

Hakuna pengine popote unapoweza kusema kwa hakika kuwa Lowasa ni fisadi kando ya hizi scenario mbili. Huoni kwamba ni rahisi kusafishika. Makosa mengine ni yale aliyoyafanya dhidi ya wapinzani kama mwana ccm hayo anaweza akasamehe.

Jambo la muhimu la kuangalia hapa ni kuwa shida nchi yetu ni mfumo na si kingine chochote. Kama nia ya UKAWA ni kuingia na kutawala tu basi ni bora tuendelee hivi hivi tu. Mfumo huu unatakiwa ufumuliwe na tuanze upya. The system is so corrupt. Kama Lowasa kuingia UKAWA kutarahisisha hilo la kuiondoa CCM na kuanza kuunda taifa upya mimi naunga mkono na aje haraka sana.

Mungu ibaraiki Tanzania
Nikiri kuwa umeandika vizuri sana na umechambua inavyotakiwa hasa unaposema msingi wa Lowassa kuwepo kwenye lisrt of shame. Katika uziwangu nimesema hakuna wakati wowote CHADEMA na Dr. Slaa wamewahi kuwatangazia wananchi kuwa wametupilia mbali list of shame. Sanasana list inaongezeka ikijumuisha majina ya zamani. Kama CHADEMA na Dr. Slaa pamoja na Tundu Lissu hawajawahi kuikana list of shame iweje leo ghafla bin vuu, Lowassa asafishwe? Kama waliridhika kuwa Lowassa ni msafi kwa nini hawakumpatia haki yake mapema ya kumsafisha mpaka wasubiri wakati huu wa uchaguzi ambao CCM imemkata? Ni lini list of shame ime-shrink kuwa na orodha ya watu 10 badala ya 11. CHADEMA na UKAWA wata-live consequences za uamuzi wao. Watakuwa salama kama watamsimamisha mgombea ambaye siyo Lowassa. Kwa wengine mantiki inakataa kabisa, list of shame bado haijakuwa revised kwa kupunguzwa.
 
Watanzania wanataka mabadilikoo mambo ya kubebana sahv yameshakwishaa people are thinking beyond
 
Siasa mchezo sio.
Baada ya uchaguzi ndio kila mtu atajua alichopanda.

Halafu UKAWA wanaamini saana kwamba yeye ndio atawabeba,sasa tujiulize hivi kweli hiki chama au NGO.

Yaani kwenye Chama choote hakuna mwenye Kiki zaidi ya Lowasa?
UKAWA kuna mitego wanaingia ya CCM bila wao kujijua,wasitegemee kwamba kuna makubwa ambayo wananchi wanategemea kwa hilo la LOWASA,sana sana ni kuwapa Kiki CCM tu.

Kama kuhama chama ni janga la pande zoote,Chadema kuna team itatimkia ACT kwa ZITTO na Machali,CUF kuna Team inatimkia ADC kwa Hamad Rashid,balaa tupu kote kote.
Na ndio maana hata CCM hii habari haiwaumizi kichwa kabisaaa

Angalia watu wako walisema nini baada ya Magufuli kuteuliwa '' sasa basi afadhari huyu jamaa atatunusuru''
Angalia yaliyotokea Kenya na wala usiende mbali MKUU. Watu hawataki huu mfumo wa kiimpunity!!!!!!
 
Mkuu kama huna uhakika na ulichoandika heri kukaa kimya, kama unataka kujijua we ni mwongo rejea uzi wa @ mwanakijiji wa 2007 na nadhani utaomba mod aufute uzi huu, loh hadi aibu kwa ulivyo mwongo.
 
Hakili yangu ngoja nifikiri kwanza maana hakili yangu imechoka mno sijui tumwombe mungu
 
Sidhani kama Bw.Lowasa yuko sawa sawa kabisa! Inawezekana hayuko mzima kama tunavyodhania. Ninaposema mzima nazungumzia uzima wa psyche inawezekana kabisa hayuko hapa Duniani na amepoteza kabisa uwezo wa kutambua uhalisia!

Hili siyo jambo geni sema hapa kwetu nyumbani halieleweki sana kwa sababu bado hatujafikia huwo uwezo wa kuwa na wataalamu wa haya mambo kwetu sisi tunatambua ugonjwa pale tu mtu anapoumwa tumbo, kichwa, homa, kukohowa n.k lkn kuna magonjwa mengine yanayohusisha psyche ambayo yanasababishwa na mambo mengi kama Umri, ambapo mgonjwa huwa anapoteza hali ya kutambua uhalisia na anakuwa kwenye Dunia yake tu, hivyo anafanya mambo ambayo anayaona yeye kwenye Dunia yake, rejea ushambuilizi wa kisu kwenye daladala yule mtu alikuwa na mgonjwa na alipoteza uhalisia ktk Dunia yake alikuwa anaona kuna mtu anamshambulia na hivyo akaamua kumshambulia kama kujitetea...

Niliposikia ya kwamba Mke wa Bw.Lowasa kamsihi sana Mume wake asitoke CCM na kuhamia CHADEMA na yeye kukaidi nikatambua ya kwamba kuna kitu kinamsumbua Bw.Lowasa, ni kwamba yuko Dunia nyingine na sasa akina Slaa, Mbowe &Co. siajabu wameshajua hilo na wanachofanya ni kumtumia tu kwani kama kweli yuko sawa psyche ni ngumu sana kufanya maamuzi aliyofanya huku akijua fika yatakayo mkuta!



View attachment 271495 View attachment 271496View attachment 271497

Iawezekana pia wadeni Wake (waliomchangia billion) ndiyo waliomtuma. Kwani kama Mh. Magufuli alikataa kuungana naye inaonekana wadeni walimuambia wamuue au arudishe hela zao. Hivyo bora aoneshe juhudi kama wale wajumbe wa nec waliokuwa wamekula mil5 waliimba kuonesha juhudi.
 
Let assume hayuko mzima
viongozi wengi walioweka historia duniani hawakuwa wazima kichwani
walikuwa crazy enough to dare
Kina Hitler na Iddi Amin na Stalin na kina Mrema na Mtikila wote sio wazima but historia inawatambua

mbona Nyerere hukumuweka kwenye hiyo list wakati ana vigezo vyote?
 
Kumbuka hata Marekani ilimtumia gaidi Osama Bin Laden kuisambaratisha Urusi. Si mbaya kwa sasa CDM wakimtumia Lowasa kuusambaratisha mfumo mfu wa CCM. Siasa ni strategy na hii ni fursa nzuri ya kuisambaratisha CCM hata kama ni kwa mbinu chafu!
Hapana, hakuna justification ya kutumia mbinu chafu kufikia lengo zuri. Kumbuka jinsi UKAWA walivyokataa mchakato wa katiba kwa sababu CCM walitumia mbinu chafu. Kama CHADEMA na UKAWA wanatumia mbinu chafu kuiondoa CCM madarakani watutangazie wananchi. Ninavyofahamu ni kuwa CHADEMA inapenda siasa za kistaarabu. Njia chafu zitaishia kuwa na mwisho mbaya. Unadani Lowassa atakubali kutumika tu kama toilet paper kuiingiza madarakani UKAWA? Nani aliyesema bila Lowassa UKAWA haiwezi kuchukua nchi. Nimesema wazi hapo juu, hii strategy siyo nzuri. Inawafanya UKAWA kama watu ambao hawakuwa na political leaders wa kuongoza nchi wakati siyo kweli. Ina-dilute kwa kiasi kikubwa strengths ambazo CHADEMA na UKAWA kwa ujumla wanazo bila ya ujio wa Lowassa. Kwamba the end justifies the means, hii ni disastrous strategy.
 
Mheshimiwa EDO NGOYAI LOWASA mzee wa maamuzi magumu, nakupa BIG UP MZEEEE WE JEMBE MZEEEEE INGIA UKAWA NA sisi wote tunatia TIMU hukohuko na SASA ni safari YA UHAKIKA NA SI MATUMAINI TENA ....MWALIMU ALISEMA TUSIPOPATA DIRA YA KWELI NDANI YA CCM TUTAITAFUTA NJE YA CCM na AKAONGEZA CCM SIYO BABA WALA MAMA YAKE mwacheni mzee wetu TIMU EDO OYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.......Mzee Lowasa ni mwanasiasa aliyekomaa na ameprove katika jamii kuwa yeye ni JEMBE...kama ni kuchafuliwa huyu mzee kachafuliwa sana na mpaka leo Serekali hii haijawahi kumshitaki kama fisadi au matumizi mabaya ya offisi , jambo ambalo sisi kama watanzania inatufanya tuamini kuwa kumbe EDO ni msafi na hizo zilikuwa chuki na fitina za kisiasa....EDO twenzetu UKAWA safari hii sasa kama mafuriko waliyazuia kwa mkono basi wazuie sunami sasa
 
Angalia watu wako walisema nini baada ya Magufuli kuteuliwa '' sasa basi afadhari huyu jamaa atatunusuru''
Angalia yaliyotokea Kenya na wala usiende mbali MKUU. Watu hawataki huu mfumo wa kiimpunity!!!!!!

Usilinganishe kenya na Bongo. Bongo sisi tuna unafuu mkubwa sana. Angalau tuna accountability. Magufuli ni mtu safi sana. Ila apewe tu wabunge wengi wa upinzani ili wasaidie kuibana serikali, kwani Kwa Magufuli kutekeleza maamuzi kwake siyo shida. Na hana kundi la kulipa fadhila. Na magufuli hana kujuana, alishawahi kuacha mdogo Wake akaenda jela Kwa sababu ya ubazilifu.
 
Back
Top Bottom