Sikubaliani na hiki alichofanyiwa huyu binti, Jeshi la Polisi lichukue hatua kwa waliohusika

Nov 19, 2017
815
1,021
Kumekua na Video inayozunguka katika Magroup ya Whatsapp na mitandao mbali mbali.

Video ikimuonesha binti anayetuhumiwa kwa wizi katika makanisa.

Viongozi/waumini wanaonekana katika video hii wakimpiga mtuhumiwa.

Jambo hili halikubaliki na niuvunjaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu.

Kama hawa ndo viongozi wa dini, basi tuna safari ndefu kama taifa.

Natumaini kuwa sheria itachukua mkondo wake.

Video yenyewe hii hapa.
 
Kama unampenda Sana na kumjali mchukue kaa naye kwako umuondolee aibu ya wizi....maana huyu itakuwa Hana MTU maalumu WA kumshughulikia matatizo yake.

Kuja kuandika hapa bandiko akati amekutwa MTU Kati aisaidii kitu.....wewe unajua sadaka zinavopatikana Kwa shida siku hizi jiongeze ......ukiona uwezi mwache ale kipigo chake cha mbwa mwitu watu wamalizane naye
 
Huyo binti ilibidi atolewe pepo la wizi na kumbadilisha kwa maombi awe raia mwema sio kumpiga.

Makanisa ya sasa hayana nguvu za Mungu yapo kibiashara zaidi ndio maana yanachukia kuibiwa badala ya kubariki na kuombea wanaowaudhi kama huyo mwizi.
Kwa kitendo hicho waliyochukua ni dhahiri hayo makanisa ni magenge tu ya kutafuta fedha tu

Ova
 
Kama unampenda Sana na kumjali mchukue kaa naye kwako umuondolee aibu ya wizi....maana huyu itakuwa Hana MTU maalumu WA kumshughulikia matatizo yake.......kuja kuandika hapa bandiko akati amekutwa MTU Kati aisaidii kitu.....wewe unajua sadaka zinavopatikana Kwa shida siku hizi.......jiongeze ......ukiona uwezi mwache ale kipigo chake cha mbwa mwitu watu wamalizane naye
Kwa hiyo hapo kanisani wangempiga hadi kuua siyo

Ova
 
Kanisani nao wanachukua sheria mkono

Ova
Mkuu, wezi wengi wanajua kwenye nyumba za ibada ndio sehemu salama za kuiba kwa maana huko hawachomwi moto kwa tairi za gari ndio maana wanaenda kuiba.

Hawawezi kufanya hivyi sehemu kama Tandika sokoni.
 
Kweli mkuu. Kumbuka Papa alimsamehe yule jamaa aliyempiga risasi.
Alhaji Mwinyi alimsamehe yule dogo aliyempiga kibao.

Hawa wa sasa ni WAJASIRIAMALI sio watumishi wa Mungu.
Papa alisamehe hawa wameibiwa sim na fedha naona wanataka kumtoa mtu uhai
Bora hata wale wa uhamiaji walimpa jamaa adhabu,hawa walokole wanapiga 😂😂

Ova
 
Kwani alikwambia Nani kanisani awezi kufa?? Si mwizi .....kwani treatment ya mwizi ni nini?? Kumfanyia massage? Kumgonga,,? Au Kula naye wali maharage.😂😂😂😂
Teh teh

Ova
 
Mnisamehe, hawa jamaa ni wapumbavu!

Wamama wanaoongoza kwa kudondoka kwa mapepo kwenye hayo makanisa, wakitoa machozi wakati wanasali, ndo huyo anayesisitiza mwanamke mwenzake apigwe, aongezwe n.k

Akipelekewa kesi ya uzinzi, anasema imeandikwa SAMEHE 7 X 70, mwenye kuhukumu ni Mungu, Yesu alifia dhambi msalabani n.k

Ila huyo dada, kapora kipato chao, yaani kwao amefanya uporaji kwa kutumia nguvu TOFAUTI na wao wanavyopora kwa kutumia IMANI.
 
Back
Top Bottom