Sikubaliani mfumo wa kuwa winner wa majority votes wins the election | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikubaliani mfumo wa kuwa winner wa majority votes wins the election

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pax, Aug 22, 2010.

 1. P

  Pax JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ndugu wana JF nimejaribu kuuangalia mfumo tunaotumia wa kuchagua viongozi na hakika nikakataa kuukubali kwa vigezo kadhaa. Mfumo huu wa kupiga kura na anayepata kura nyingi kuwa ndiye mshindi sio mzuri. No offense, lakini nafikiri kuifanya kura ya Professor kama Issa Shivji kuwa sawa na ya mtu asiyejua ku analyze na ku evaluate issues ni kukosa umakini na mbinu inayotumiwa na vyama vikongwe barani africa kuendelea kukaa madarakani. Nafikiri weighted votes kutoka kwenye mikoa husika ndio ingekuwa kigezo kizuri. Kungewekwa criteria kwa mfano idadi ya watu, kiwango cha elimu mfano proportion ya watu wenye elimu ya msingi, sekondari,chuo kikuu n.k, idadi ya vyuo na vyuo vikuu, pato la mkoa, etc,etc hivi vigezo vingetoa idadi ya kura ambayo mkoa husika inatoa, mgombea yeyote anayepata majority votes za watu wa mkoa huu anachukua kura zote za huu mkoa. Maana yake ni kwamba ubora au quality ya kura itabalance idadi ya watu. Vyama ambavyo vimezoea kutumia ignorance ya wananchi kushinda vitapotea maana tabia ya kuwapa watu pesa, nguo n.k haitaweza kuwaingiza Ikulu.

  Hii itavifanya vyama kuwa makini zaidi maana vitajua kuwa idadi ya wanachama au idadi ya watu sio kigezo cha kushinda kura za mikoa. Itamaanisha pia kuwa kuwa na watu wengi wanaokuja kwenye kampeni na kuvaa fulana za vyama na kuimba majukwaani mapambio ya kila namna sio kigezo cha wao kuingia ikulu.

  Wasomi wengi hawaendi kwenye kampeni maana wanajua karaha zilizopo huko, hamna la maana wanaloongea wagombea. No offense lakini kampeni zinajazwa na makundi ya watu wasioweza kuchambua sera, wanaopiga makofi hata pale mgombea napoongea porojo na kujisifu kwa mafanikio yasiyoonekana. Hawa ndio wanaotuchagulia viongozi kila kukicha, hii nchi itakuja kuongozwa na mwendawazimu siku moja kwa kufuata huu mfumo wa kura mojamoja. Marekani, South Africa etc ndio mfumo wanaotumia. Kura nyingi za mtu mmojammoja hazikupi ushindi, Weighted votes kutoka kwenye mikoa au provices ndio kigezo, maana hizi ni quality votes.

  Natumai nimeeleweka katika hili, nimechoka kuona watu wanakodishwa kwenda kwenye kampeni ili mikutano ijae au watu kupiga kura kutokana na mapenzi tu ya chama bila kuangalia umakini wa mgombea.
   
Loading...