Sikubaliani kamwe na hili la "Bado tunakopesheka"

NAOMBA NIKOSOE KWA WELEDI
Mkopo una pande mbili hasi na chanya.... Mkopo hasi ni ule unaotumika mambo yanaposhindikana kabisa... Mkopo chanya ni ule mkopo unaokopa kufanyia jambo la maendeleo.. Lakini vyovyote iwavyo mkopo ni utumwa
Jambo lingine kwenye mkopo ni hili.... Unakopa wapi, unamkopa nani, kwa masharti yapi, kwa muda gani na kwa riba kiasi gani... Kuna mikopo ina masharti magumu na riba kubwa.
Kwenye mikopo pia kuna makubaliano, je familia inajua? Je mmeshauriana na kukubaliana? Hiki ni kigezo muhimu pia... Zaidi usipende kujifananisha na wengine , ati kwakuwa tu mimi nimekopa tena mkopo mrefu basi na wewe uniige... Hujui nguvu yangu ya kulipa ikoje...
Kama nchi naweza kusema tumekengeuka kwenye hili la mikopo na hii misaada, kwakuwa tumekuwa wakurupukaji mno na hatutendi kwa weledi.... Ni kweli kabisa wenzetu wana mikopo mirefu lakini ina faida kubwa na riba yao pengine ni ndogo sana... Halafu WAMESHAURIANA NA KUKUBALIANA.... Nimeshtushwa na kusononeka moyoni kwamba barabara ya uhuru ilijengwa kwa mkopo na tumechukua zaidi ya miaka 40 kuumaliza kulipia.... Hapa mkopeshaji Kala riba ma faida ya kufuru....
Mchina alijikongoja kwa miguu yake mpaka akasimama... Leo ndio mkopeshaji mkubwa wa mataifa mengi akiwamo mmarekani.. Kwahiyo si kweli kwamba usipokopa hutaendelea
Mimi nasema (I stand to be correct) tuondokane na haya mawazo ya kukopakopa.... Hatutafika popote... Tuwe na mawazo mapya ya kuja kuwa taifa linalokopesha kuliko hii ideology ya kusema bado tunakopesheka...!!! TUJIFUNZE KUJITEGEMEA na kama ni kukopa tukope kidogo sana tena kwa makubaliano halafu tukope kwenye taasisi zenye masharti nafuu na riba ndogo
Tusimuige Mjapani hatujui mikopo yake masharti yake yakoje... Lakini tuangalie Mjep yuko wapi.. Tusijilinganishe kabisa na yeye kwakuwa pamoja na kukopa sana almost alisimia 200 ya pato lake la taifa... Lakini ni mmojawapo wa nchi zinazoongoza kutoa misaada Tanzania na mikopo ya masharti nafuu.... Tuwe na tafakuri kwenye hili... Wenzetu wametuzidi sana... Isije kuwa wanakopa kwa riba ndogo sana halafu mkopo huohuo wanatukopesha sisi kwa riba ya juu halafu anakula commission... Mjapani sio mpumbavu atoe chakula chake ampe mgeni
Tusimuige mmarekani, huyo ndio kabisaaa sio level yetu... Hivi tunajua federal reserve kwenye dhahabu ni kiasi gani? Ukipata takwimu zake utatamani ujinyonge... Mmarekani hagusi vyake kabisa... Angalia mafuta anayo lakini hachimbi kila siku anahangaika na mafuta ya waarabu
a16c7de8e74b1adba03a131cf6f46f22.jpg

Mmarekani anakopa kwa akili, angalia mauzo yake ya silaha kwa mwaka duniani... Anakopa BILIONI kumi .. Anatengeza silaha anaziuza kwa BILIONI 20... Huyo sio mwenzako.. USIJIFANANISHE NAYE KABISA...
Tusidumazwe na hizi akili za kukopakopa na misemo ya kujifariji kwamba usipodaiwa huaminiki... Huheshimiki.. Uchumi wetu unajikongoja.. Tusiongeze matatizo ya madeni ya mikopo tena hii ya kukopa mia tano riba mia nne....

Tuwe na tafakuri
Vielimu vyenu duni kuhusu uchumi msitake kujihalalidhia upinzani wenu dhidi ya Serikali na kuubatiza ushauri. Wapo wengi serikalini wenye uelewa wa kutosha juu ya hayo mnayodai na kazi yao ni kuweigh faida na hasara ya maamuzi hayo.
Huwezi kudoubt kwa Rais anayekopa fedha kwa ajili ya miundombinu labda tu kwa kuwa uchumi unakuwa umekupita kushoto.
Miaka michache hasa kuanzia 2020, tunatarajia kuwa na fedha nyingi zinazotokana na tozo za mafuta ya Uganda ambayo kwa mapipa yapatayo 216,000 kila siku, huku kila pipa lokilipiwa dola 12, tunatarajia kuwa tunapata wastani wa tilioni 2 (2,000,000,000,000).
Licha ya LNG kuchelewa kujengwa kutokana na mporomoko mkubwa wa mafuta na gesi mwaka 2014, kutengemaa huko kunatarajia kuboost speed ya mchakato wa kuchimba gesi baharini, ambako jumla ya gesi tuliyonayo ni futi tilioni 57 (57,000,000,000,000 cf). Hapa wenyewe mnajua mapato yake.
Ni lazima SGR pia italeta mapinduzi makubwa ya mapato kwa bidhaa kutoka nchi jirani.
 
Deni La Marekani ni sh ngapi. Ok tuache hayo. Unakosoa kwa nia gani ya kama kawaida yako kumpinga Rais. Unataka kutuambia Rais kama JPM na Sio Taasisi imekopa. Je umeangalia nia ya mkopo. Huwa ajenda zenu mkianza kuandika mnakuwa kwanza na chuki zile za Sisi kina mama au unakuwa na nia tu ya kusubiri kukosoa tena JF ili wanabavicha mpate uwanja Wa kutoa prejudices zenu. Lini umesifia. Katika Nchi za africa zenye wezi wengi jitahidini kupima nia ya viongozi wenu .mnakaa hapa mnasahau historia mpo tu na ajenda zenu zenye majibu kwanza. Eti mnajadili hapa hamjadili mnapiga Majungu. Mana mna majibu yenu. So sad so stupid so disheartening.
Akiota mapembe unamuongezea.. Na mkia.. Hii taarabu inafaa kuitengenezea bit... Kisha nitakupeleka studio kwa gharama zangu ukatoe singo yako hii.... Kuna mada ukiziona ni maji ya shingo kwako ni vema kukaa kimya ili kuficha upumbuvu wako... Unalinganisha deni la marekani, mtu anayekusaidia kila siku... Your upstairs should be examined
 
Mungu akutie nguvu kwa hili. Pia waandishi wa habari wasio woga ni watu muhimu sana ktk kufikisha ujumbe. Nikupe mfano. Kipindi cha vita ya wahujumu uchumi (chini ya Hayati Sokoine)kati ya 1982-1983 kuna swali aliulizwa Mwl. Nyerere kwenye interview likapelekea kusitisha operation ile. Kama sijakosea aliulizwa swali moja la kimantiki na mwandishi mmoja maarufu aliitwa Peter Enahoro wa gazeti la Afrca Now. Maswali "Je,mnapokamata pesa na mali za wafanyabiashara na kuzitaifisha ni halali?" Mwl akauliza kwa nini unaniuliza vile? Akamjibu,ni vyema wakatendewa haki! AkamuulizaMwl,hivi katika mfumo wako wa siasa ya ujamaa,ni kiasi gani cha pesa kisheria mfanyabiashara anatakiwa kukimiliki ili asiitwe mhujumu uchumi? Akaendelea,je kama nchi huru,hamuoni ni kosa, kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hamjaliwekea sheria yoyote? Kiujumla maswali hayo,yalimfanya Mwl abadili uelekeo na akamjibu yule mwandishi "I wish you could be a good critic by starting there, and I agree with you that we made a mistake"

Sent from my H8501 using JamiiForums mobile app
That was the man with brains upstairs... Rip
 
Deni La Marekani ni sh ngapi. Ok tuache hayo. Unakosoa kwa nia gani ya kama kawaida yako kumpinga Rais. Unataka kutuambia Rais kama JPM na Sio Taasisi imekopa. Je umeangalia nia ya mkopo. Huwa ajenda zenu mkianza kuandika mnakuwa kwanza na chuki zile za Sisi kina mama au unakuwa na nia tu ya kusubiri kukosoa tena JF ili wanabavicha mpate uwanja Wa kutoa prejudices zenu. Lini umesifia. Katika Nchi za africa zenye wezi wengi jitahidini kupima nia ya viongozi wenu .mnakaa hapa mnasahau historia mpo tu na ajenda zenu zenye majibu kwanza. Eti mnajadili hapa hamjadili mnapiga Majungu. Mana mna majibu yenu. So sad so stupid so disheartening.
We Jamaa ni bure kabisa!
Sasa maswala ya vyama hapa yameingiaje?

Unauliza ni lini mshana amemsifia jpm!!!
Amsifie ili iweje?
Kwa kuongeza deni la taifa kwa 17% kwa miaka miwili tu?

Yaani ni sawa unataka baba amnunulie nguo mwanae halafu halafu upite na matarumbeta mtaani kumsifu kama baba ameifanyia familia yake mambo makubwa!
Huo ni wajibu wake!!
 
Vielimu vyenu duni kuhusu uchumi msitake kujihalalidhia upinzani wenu dhidi ya Serikali na kuubatiza ushauri. Wapo wengi serikalini wenye uelewa wa kutosha juu ya hayo mnayodai na kazi yao ni kuweigh faida na hasara ya maamuzi hayo.
Huwezi kudoubt kwa Rais anayekopa fedha kwa ajili ya miundombinu labda tu kwa kuwa uchumi unakuwa umekupita kushoto.
Miaka michache hasa kuanzia 2020, tunatarajia kuwa na fedha nyingi zinazotokana na tozo za mafuta ya Uganda ambayo kwa mapipa yapatayo 216,000 kila siku, huku kila pipa lokilipiwa dola 12, tunatarajia kuwa tunapata wastani wa tilioni 2 (2,000,000,000,000).
Licha ya LNG kuchelewa kujengwa kutokana na mporomoko mkubwa wa mafuta na gesi mwaka 2014, kutengemaa huko kunatarajia kuboost speed ya mchakato wa kuchimba gesi baharini, ambako jumla ya gesi tuliyonayo ni futi tilioni 57 (57,000,000,000,000 cf). Hapa wenyewe mnajua mapato yake.
Ni lazima SGR pia italeta mapinduzi makubwa ya mapato kwa bidhaa kutoka nchi jirani.
Siangalii mipasho uliyoandika kwakuwa hapa sio kwenye band ya taarabu mtaani... Ninachoshangaa ni kule kudhani wewe unajua zaidi kuliko wengine na takwimu zako za kufikirika kuelekea 2020
 
We Jamaa ni bure kabisa!
Sasa maswala ya vyama hapa yameingiaje?

Unauliza ni lini mshana amemsifia jpm!!!
Amsifie ili iweje?
Kwa kuongeza deni la taifa kwa 17% kwa miaka miwili tu?

Yaani ni sawa unataka baba amnunulie nguo mwanae halafu halafu upite na matarumbeta mtaani kumsifu kama baba ameifanyia familia yake mambo makubwa!
Huo ni wajibu wake!!
Hao ndio tunaita short sighted minds
 
Sizonje ameshasema sisi ni matajiri ndio maana tunaaminika kupewa mikopo!
Tatizo watu wetu hawajui kuwa kwenye international Credit Ratings za kina Moody's and the like sisi tuko kwenye JUNK STATUS!!!

Hii JUNK STATUS inatuweka kwenye kundi la nchi ambazo ni Risk kuzikopesha. Yaani wanaotukopesha wanatake chances tu .......... No wonder interest rate tunawekewa juu. Unakopa 500 unalipa 900 kwa miaka mitano!!

Sasa sijui kwa nini hata akina Zitto huwa hawamention hii kitu!!
 
Vielimu vyenu duni kuhusu uchumi msitake kujihalalidhia upinzani wenu dhidi ya Serikali na kuubatiza ushauri. Wapo wengi serikalini wenye uelewa wa kutosha juu ya hayo mnayodai na kazi yao ni kuweigh faida na hasara ya maamuzi hayo.
Huwezi kudoubt kwa Rais anayekopa fedha kwa ajili ya miundombinu labda tu kwa kuwa uchumi unakuwa umekupita kushoto.
Miaka michache hasa kuanzia 2020, tunatarajia kuwa na fedha nyingi zinazotokana na tozo za mafuta ya Uganda ambayo kwa mapipa yapatayo 216,000 kila siku, huku kila pipa lokilipiwa dola 12, tunatarajia kuwa tunapata wastani wa tilioni 2 (2,000,000,000,000).
Licha ya LNG kuchelewa kujengwa kutokana na mporomoko mkubwa wa mafuta na gesi mwaka 2014, kutengemaa huko kunatarajia kuboost speed ya mchakato wa kuchimba gesi baharini, ambako jumla ya gesi tuliyonayo ni futi tilioni 57 (57,000,000,000,000 cf). Hapa wenyewe mnajua mapato yake.
Ni lazima SGR pia italeta mapinduzi makubwa ya mapato kwa bidhaa kutoka nchi jirani.

kumbe kuna watu wanadharau kiasi hiki halafu unaishi kwa ndoto?? ajabu sana hii!!!
 
Mkuu Ukijiheshimu utaheshimiwa jamaa hana lugha ya kuheshimu Watanzania wala wale ambao waliomtangulia kwanini aheshimiwe? Kuwemo ndani ya taasisi ya Urais hakumpi mtu sifa ya kuheshimiwa kama yeye mwenye hana heshima na wala hajui kutumia lugha yenye staha. Kuna Jizi kama yeye nchi hii? Nani alimwambia wastaafu wanawashwa?

23434832_1767224130240823_288060841442134065_n.jpg

Aliyeshauri tuchukue huu mkopo na bila hata kulishirikisha bunge sijui aliwaza nini... Na aliyekubali pia mkopo wa riba kama hii naamini hajushauriwa vema... Unajua wapiga dili wako kila mahali na kwenye kila viwango vya maisha... Nina wasiwasi huu mkopo uliingiliwa na madalali na inawezekana kabisa ndio walijenga hoja zenye ushawishi mkubwa mpaka ndugu zetu wakalainika na kukubali
 
NAOMBA NIKOSOE KWA WELEDI
Mkopo una pande mbili hasi na chanya.... Mkopo hasi ni ule unaotumika mambo yanaposhindikana kabisa.
....
Kama nchi naweza kusema tumekengeuka kwenye hili la mikopo na hii misaada, kwakuwa tumekuwa wakurupukaji mno na hatutendi kwa weledi.

Ni kweli kabisa wenzetu wana mikopo mirefu lakini ina faida kubwa na riba yao pengine ni ndogo sana.
...
Uchumi wetu unajikongoja. Tusiongeze matatizo ya madeni ya mikopo tena hii ya kukopa mia tano riba mia nne.

Tuwe na tafakuri

mshana jr, hoja yako ni nzito na inahitaji mjadala wenye takwimu sahihi. Kama unayo majibu ya maswali yafuatayo, utakuwa umetusaidia kujadiliana kwa tija.
1) Serikali iliyoko madarakani imekwisha kopa kiasi gani hadi sasa?

2) Imekopa kwa shughuli gani?

3) Kiasi hicho kimokopwa wapi?

4) Ni masharti gani ya mikopo hiyo?
 
Tatizo watu wetu hawajui kuwa kwenye international Credit Ratings za kina Moody's and the like sisi tuko kwenye JUNK STATUS!!!

Hii JUNK STATUS inatuweka kwenye kundi la nchi ambazo ni Risk kuzikopesha. Yaani wanaotukopesha wanatake chances tu .......... No wonder interest rate tunawekewa juu. Unakopa 500 unalipa 900 kwa miaka mitano!!

Sasa sijui kwa nini hata akina Zitto huwa hawamention hii kitu!!
Nimeokota kitu hapa JUNK STATUS RANKING
 
mshana jr, hoja yako ni nzito na inahitaji mjadala wenye takwimu sahihi. Kama unayo majibu ya maswali yafuatayo, utakuwa umetusaidia kujadiliana kwa tija.
1) Serikali iliyoko madarakani imekwisha kopa kiasi gani hadi sasa?

2) Imekopa kwa shughuli gani?

3) Kiasi hicho kimokopwa wapi?

4) Ni masharti gani ya mikopo hiyo?
Asante hili linahitaji muda ili kuweza kujibu kwa usahihi
 
Back
Top Bottom