Sikubali kuulizwa mjumbe wangu wa nyumba kumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikubali kuulizwa mjumbe wangu wa nyumba kumi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakati, May 13, 2009.

 1. Kakati

  Kakati Senior Member

  #1
  May 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nafasi ya mjumbe wa nyumba kumi katika Tanzania:

  Leo naona niwarudishe watanzania wenzangu katika jambo ambalo limekuwa likinisumbua kwa muda mrefu, nalo ni juu ya nafasi ya mjumbe wa nyumba kumi katika utawala na uongozi wa nchi yetu.

  Ninavyofahamu wakati wa chama kimoja tulikuwa na mfumo ambao kiongozi wa CCM wa eneo alikuwa pia ndiye kiongozi wa serikali katika eneo hilo. Katika ngazi ya Kijiji, kiongozi wa CCM alikuwa Mwenyekiti wa Tawi. Alikuwa ndiye mwenye majukumu ya kuendesha chama na serikali. Katika ngazi ya chini kabisa ilikuwa kiongozi alikuwa Balozi wa nyumba kumi ambaye katika maeneo mengine aliitwa Mjumbe wa nyumba kumi.

  Kiongozi huyu alikuwa na mamlaka ya chama na serikali. Hakuwa na malipo isipokuwa kuheshimiwa na alikuwa akichaguliwa na watu katika eneo husika kuwa kiongozi wao.

  Hali hii kisheria ilabadilika baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa. Sasa Mwenyekiti wa kijiji huchaguliwa na wananchi naye hutumikia watu bila kujali vyama vyao. Katika utaratibu wa miundo ya serikali za mitaa sehemu zingine kiongozi wa chini ni Mwenyekiti wa Kijiji/Mtaa na katika eneo jingine ni Mwenyekiti wa Kitongoji. Hakuna tena katika utawala na uongozi ngazi ya Balozi au mjube wa nyumba kumi.

  Kinachonifanya niandike haya ni hali halisi ilivyo kwa sasa kiutawala na utendaji wa ofisi nyingi zinazohusiana na jamii kama huduma za hospitali, vituo vya polisi na kadhalika. Ukitoa taarifa polisi utaulizwa jina la mjumbe wako! Sasa mjumbe gani? Katika CCM wanao viongozi wao ambao bado wanawaita wajumbe na kwa ujumla hawa wameendelea kuwa walewale waliokuwepo kabla ya utaratibu wa vyama vingi. Kumbe polisi anakuwa anauliza mjumbe wako sawa na kukuuliza kiongozi wako wa CCM ni nani. Hii sio sawa kwani hakuna tena nafasi ya mjumbe katika utawala wa nchi yetu na wala mtu hahitajiki kumjua mjumbe wa CCM wala wa CHADEMA, CUF au chama chochote kingine.

  Ninapoandika hili nina ushahidi wa hivi karibuni kuhusiana na ugawaji wa chakula cha msaada (Home The Guardian, 13th May 2009). Habari hiyo inamtaja Mkuu
  wa Wilaya kuwa alitegemea watu watambuliwe na mjumbe wao. Sehemu yake inasema "According to the DC, the victims were supposed to be identified by known ten cell leaders after
  taking the list of families to ward officers for food distribution." Sasa hao wajumbe 'known' nani anawajua na anawajuaje? Mamlaka yao yanatoka wapi au yanatokana na sheria gani? Kama ni wa CCM, je kama kila chama kikiwa na wajumbe watajulikana wangapi?

  Huyo mkuu wa wilaya anatafuta urahisi wa kushughulika na watu, tena hayuko peke yake. Lakini kwa kweli yeye na wenzake wanakwenda kinyume na mfumo wa uongozi na utawala wa nchi yetu. Natambua umuhimu wa watu kutambuana a kutambuliwa, ni muhimu sana, tena zaidi katika nchi ambayo watu hawana vitambulisho rasmi. Hata hivyo naona ni muhimu ama tuanzishe upya nafasi ya hao wajumbe watakaokuwa hawahusiani na chama chochote au basi wakati wa kutoa huduma tusiwaulize watu wajumbe wao na tusitumie wajumbe wa CCM au wa chama chochote kwa shughuli za Serikali zinazohusu raia bila kujali itikadi zao.
   
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ki ukweli mimi nitajuaje kama wewe uliishapata msaada na unataka tena na tena. Kuna wazee wa EAC wameibiwa sana hela zao kwa sababu mtu anaenda anasema mimi ni Salum Moses, atakuja na vyeti vya ndoa, hati ya nyumba na vitu kama hivyo ambavyo vinatengenezeka Salamander,na karani mlipaji hana njia ya kuthibitisha. Njia mbadala ni kuwa na national id card, hapa ndiyo umuhimu wa kadi hiyo unapojulikana.
   
 3. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu hoja yako ni njito na yamhimu sanaaa. Mi nadhani hawawajumbe wanyumba kumi hawatakiwi kuwa na chama kama ilivyo jeshi la police au JWTZ. Hawa wachaguliwe na wananchi wote bila kujali itikadi kwani wanafanya kazi kama polisi bila kujali chama. Hivyo ni vyema wahusika wakabadilisha utaratibu huo wasiwe kama watumishi wa CCM bali wananchi kwa ujumla na wasiwe na wasifungamane na chama chochote.
   
 4. Kakati

  Kakati Senior Member

  #4
  May 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi naona ni sawa wachaguliwe na wanchi wote kama unavyosema lakini wanaweza kutoka katika vyama sio lazima wasiwe na chama kama polisi au JWTZ. Muhimu ni kwamba wasifanye kazi kwa kutumwa na CCM au chama chochote huku wakitegemewa kufanya kazi kwa ajili ya watu wote.

  Kubwa naona tunakubaliana kwamba utawala wa nchi usiishie katika Mtaa/kijiji. Kuwe na ngazi ya chini yake inayotambuliwa kiserikali.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nani alikudanganya kuwa hawana vyama? nani alisema kuwa polisi na Jwtz hawana vyama???????????????????????????
  Kama nasema uongo muulize Tibaigana kampeni anazofanya za chama cha mafisadi kadi alipata lini??????????????
  Waulize wanajeshi kibao walio mujengo kadi walipata lini????????? au nini kiliwafurahisha kujiunga na mafisadi?????????????
   
 6. Kakati

  Kakati Senior Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Suala hili naona lisisahaulike wakati wa kujadili katiba mpya ya Tanzania
   
Loading...