Sikubali kama uchumi wetu umeshuka bali Serikali inakwepa majukumu yake au kuna mlegezo uko mbioni

wakatanta

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
2,593
3,148
Nitakuwa wa mwisho kukubali maelezo ya Rais Samia suluhu Hassan ya kwamba uchumi wetu umeshuka kutoka kukua kwa 6.9% mpaka 4.6%.

Maelezo haya yametolewa mwezi mmoja na siku kadhaa mara baada ya Rais Magufuli kufariki dunia.

Akiwa hai na amiri jeshi mkuu Rais Magufuli, akisaidiwa na Samia ,Majaliwa na Mpango waliendelea kutuambia kwamba uchumi wetu umetulia ni kweli ingekuwa ngumu kupanda, hata hivyo tulicheza pele katika kudili na corona, hakukuwa na lockdown, Wananchi waliendelea kuzalisha watalii waliendelea kuja japo si kivile.

Magufuli alikuwa muwazi,alisema, uchumi umekuwa lakini tunakazi kubwa ya kujenga nchi ,siongezi mishahara ispokuwa tujenge nchi kwanza.

Nionavyo Mimi Waliobakia wanampango wa kusamehe kodi makampuni makubwa kwa kisingizio cha kubusti biashara ,kukwepa kuongeza mishahara, huku wakijiandaa kupokea misaada ikiambatana na mashariti ya Kijinga kabisa, kaeni kwa utulivu muone kama hiki kiunzi tutakiruka, waliobakia karibu wote ni waoga sana, jiandaeni kununua chanjo badala ya kujenga uchumi, msikilizeni foreign Minister yupo live ITV kipindi cha dakika 45, tunaenda kukopeshwa fedha za chanjo, huo ndio msimamo wa serikali kwa kigezo cha kwenda na dunia, unapewa misaada kiduchu halafu unakopeshwa deni kubwa la matrilion ya pesa kwa ajili ya tiba.
 
Assignment ambayo Bi Mkubwa kapewa na sponsaz wake --- kama uliwahi kufanya mathematics za inverse function, utanielewa vizuri. Mkono wake unawaelekeza raia kwamba tunaenda Mashariki, but mwendo halisi ni kuelekea Magharibi. Hii inaitwa ^Confuse and Control Rule^ ilibuniwa na ^Mjeremani^ Hitler mwaka elfu moja mia tisa arobaini na kumi.
 
We boya kweli! Nani alikuwa na koromeo la kumtishia maisha mwenzie awamu ya 5? Njaa inakuchapa hata huo muda wa kumvimbia mtu unaukosa,,, tumeheshimiana sana uraiani labda kama mwenzangu ulikuwa umeajiriwa kwa muhindi!

Thubutu, uhuni wote uliokuwa ukifanyika chini ya dhalimu tumeuona, watu wenye madaraka walikuwa na kiburi cha hali ya juu cha madaraka, na walikuwa wanaweza kukufanya lolote. Kwenye chaguzi tumeona unyama, ukatili na uhayawani wa wazi, tena kwa uratibu wa vyombo vya dola. Sijui ni heshima ipi unaongelea.
 
Thubutu, uhuni wote uliokuwa ukifanyika chini ya dhalimu tumeuona, watu wenye madaraka walikuwa na kiburi cha hali ya juu cha madaraka, na walikuwa wanaweza kukufanya lolote. Kwenye chaguzi tumeona unyama, ukatili na uhayawani wa wazi, tena kwa uratibu wa vyombo vya dola. Sijui ni heshima ipi unaongelea.
wapinzani kuporwa ubunge wao au ukatili gani unasema!!!
 
Back
Top Bottom