Sikuamini siku nilipoona Mwanaume akilia na kujisabishia kifo kwa ajili ya Mapenzi. Wanaume ndio wanaumizwa sana kwenye mapenzi

Narudia tena kwa msisitizo kuwa sitasahau siku nilipoona "Mwanaume"akilia kwa sababu ya Mapenzi.Sikuwahi kufikiria kama kitu kama hiki kinaweza kutokea.

Kijana mmoja biashara yake ilikuwa ya duka.Alitokea kumpenda mdada mmoja wa chuo alikuwa anasomea nursing. Alimtongoza yule dada akiwa form 6 yule dada sijui ni jini maimuna lilimjia akakubali Ila alikuwa akisita sita mwanzoni kisha akaingia box.

Walianza mazoea kama kiutani Ila mwishowe wafall in love. Yule mdada alipokwenda shule umbali haukuwa kikwazo kwao kwani simu na mitandao ilitumika kwa wao kuwasiliana.

Kila yule dada alipohitaji "hela"wao wanaita "pocket money"kijana aliingia mfukoni bila choyo na kumtumia huko aliko.

Mahitaji hayakuishia hapo zile mara sina ka dress kazuri Kama wenzagu hazikuisha kila siku.Kijana aliendela kuvumilia akijua palipo na upendo ni kuvumiliana.

Baada ya kumaliza Chuo na kuhitimu Nursing.Alirudi nyumbani na waliendelea kukutana na penzi likanoga,hakuna aliyetia mashaka penzi.

Ila jinamizi likaingilia Penzi lao yule dada mara tu alipopata kazi katika hospitali ya Mkoa. Mazoea yakapungua kabisa kwasababu baadae alihamishwa sehemu ya kazi.Alichomuahidi ni kwamba sitakusahau ntarudi unioe

Siku iliyomliza yule kijana ni Pale aliposhuhudia sherehe kubwa ya ndoa iliyokuwa ikifanyika mtaani kwao ya Familia moja ya Kitajiri hapo mtaani.

Yule kijana alikuwa mtaalamu wa kufunga mastage katika kumbi za sherehe basi hiyo siku haikuwa nzuri kwake aliitwa kufunga stage katika kumbi hizo.

Baada ya sherehe kuanza alipomuona Bibi Harusi alistuka moyo na kujiuliza "mbona Kama namfahamu"alikuwa akiitwa Angel Racy basi baada ya jina la bibi harusi kutajwa nguvu zilimuishia kabisa akakosa furaha na kutoka nje ya ukumbi.

Hapo ndipo nilimshuhudia akilia nje ya ukumbi na kujilaumu"kwanini aliniaminisha ananipenda wakati leo ameolewa na msomi na mtoto wa kitajiri ameniacha mimi maskini".

Kwa ghadhabu aliyonayo aliwasha pikipiki yake na kuelekea kwa spidi kali nyumbani.Lakini kwasababu ya machozi yaliyokuwa yakiririka alishindwa Kuona mbele vizuri ndipo Gari moja kubwa lililokuwa limebeba mahindi lilimpitia na kumsambaratisha.

Hii ni moja ya visa vya kuumiza sana Ila wanaume wanaumizwa kwa njia mbalimbali kwenye mapenzi.Hata kuliko wan awake maumivu ya mwanume aliyeumizwa ni Makali zaidi ya mwanamke
Kujuiua kwa ajili ya mapenzi ni udhaifu wa mtu binafsi. Haujali jinsia bali kiwango fulani cha ukichaa wa muda (temporal insanity) wa mhusika.
 
Yani mimi lamba mwiko niache ugali dagaa,wali na nyama nijiue kisa mapenzi!!!! Mapenzi yakinikosea haimaanishi maini,juisi kola,makande,mchicha n.k navyo ati vimenikosea hivyo niviache tu!..
 
Narudia tena kwa msisitizo kuwa sitasahau siku nilipoona "Mwanaume"akilia kwa sababu ya Mapenzi.Sikuwahi kufikiria kama kitu kama hiki kinaweza kutokea.

Kijana mmoja biashara yake ilikuwa ya duka.Alitokea kumpenda mdada mmoja wa chuo alikuwa anasomea nursing. Alimtongoza yule dada akiwa form 6 yule dada sijui ni jini maimuna lilimjia akakubali Ila alikuwa akisita sita mwanzoni kisha akaingia box.

Walianza mazoea kama kiutani Ila mwishowe wafall in love. Yule mdada alipokwenda shule umbali haukuwa kikwazo kwao kwani simu na mitandao ilitumika kwa wao kuwasiliana.

Kila yule dada alipohitaji "hela"wao wanaita "pocket money"kijana aliingia mfukoni bila choyo na kumtumia huko aliko.

Mahitaji hayakuishia hapo zile mara sina ka dress kazuri Kama wenzagu hazikuisha kila siku.Kijana aliendela kuvumilia akijua palipo na upendo ni kuvumiliana.

Baada ya kumaliza Chuo na kuhitimu Nursing.Alirudi nyumbani na waliendelea kukutana na penzi likanoga,hakuna aliyetia mashaka penzi.

Ila jinamizi likaingilia Penzi lao yule dada mara tu alipopata kazi katika hospitali ya Mkoa. Mazoea yakapungua kabisa kwasababu baadae alihamishwa sehemu ya kazi.Alichomuahidi ni kwamba sitakusahau ntarudi unioe

Siku iliyomliza yule kijana ni Pale aliposhuhudia sherehe kubwa ya ndoa iliyokuwa ikifanyika mtaani kwao ya Familia moja ya Kitajiri hapo mtaani.

Yule kijana alikuwa mtaalamu wa kufunga mastage katika kumbi za sherehe basi hiyo siku haikuwa nzuri kwake aliitwa kufunga stage katika kumbi hizo.

Baada ya sherehe kuanza alipomuona Bibi Harusi alistuka moyo na kujiuliza "mbona Kama namfahamu"alikuwa akiitwa Angel Racy basi baada ya jina la bibi harusi kutajwa nguvu zilimuishia kabisa akakosa furaha na kutoka nje ya ukumbi.

Hapo ndipo nilimshuhudia akilia nje ya ukumbi na kujilaumu"kwanini aliniaminisha ananipenda wakati leo ameolewa na msomi na mtoto wa kitajiri ameniacha mimi maskini".

Kwa ghadhabu aliyonayo aliwasha pikipiki yake na kuelekea kwa spidi kali nyumbani.Lakini kwasababu ya machozi yaliyokuwa yakiririka alishindwa Kuona mbele vizuri ndipo Gari moja kubwa lililokuwa limebeba mahindi lilimpitia na kumsambaratisha.

Hii ni moja ya visa vya kuumiza sana Ila wanaume wanaumizwa kwa njia mbalimbali kwenye mapenzi.Hata kuliko wan awake maumivu ya mwanume aliyeumizwa ni Makali zaidi ya mwanamke
Hapa kilichomuua ni mazingira aliyomo alipogundua hizi habari mbaya. Kama ingekuwa ni nyumbani, amepigiwa simu na kupewa taarifa mbaya, kama ni kulia, angelia na kulala na akawa salama. Ila kulia huku unaendesha chombo barabarani, ajali ina nafasi kubwa kutokea.
 
Wanaume wapumbavu labda kama huyo wanaosomesha wanawake na kuwasubili,eti kupenda.

Mimi nimekuwa nikipendwa zaidi kuliko kupenda ila kipindi niliumiaga ni wakati Niko chuo kuna mdada ambae alinielewa na katika mazoea nikamuelewa yeye alikuwa mjanja na kanitoa out nyingi Sana hadi kulijua Jiji.

Nikajiaminisha tukawa kwenye love,akijikuta nimecheat wala alikuwa ha mind anauliza tuu afu anakaa kimya siku ya siku nikaja kujua kumbe ana mtu wake na ni wachumba akanipiga marufuku eti nisije haribu uchumba wao.

Kuanzia hapo Sikuwahi kuwaamini wanawake tena niliumia Sana ila sikulia ,kwa hiyo hadi leo hii sijawahi kupenda na kwa kweli siumiagi maana mahusiano yangu yoyote huwa Niko mguu ndani mguu nje Niko tayari kwa chochote hadi kwenye ndoa naishi hivyo hivyo na nimezoea

Kiufupi vijana ni wahanga wanatakiwa kupewa elimu ya saikolojia ya mapenzi na kutomwamini mwanamke maana ni mtu anabadilika,
 
Wenye hela kina bill gate ndo wameachwa mkuu....
Sawa sasa si unapesa ambazo ndio security yako ya uhakika kuliko mtu kwa mgongo wa mapenzi,sijui mnaopenda ila mm kupenda ni kugonga demu tena once namkinai natafuta mwingine,binafsi sirudiagi wanawake ukiacha mke ambae nafanya kama wajibu
 
Ndo tatizo la kuwa na kamupenzi kamoja tyuu!! what is a Nurse bana!! tena one year course!! unatafuta kifo tu km hivi!! kidume kamata videmu kumi vinavyo zidiana kwa Elimu na uzuri!!

mimi NIlikuwa na mupenzi mzuri wa kawaida akaleta nyodo sababu ya uzuri wake Lool!! nikabeba Dr akanionyesha mikogo ajili ya kijistethoscope chake nikasema subiri dawa.

nikaruka na Muhasibu shirika la Afya Duniani mpaka leo tuko ughaibuni. siwajui tena hao!! wanasaga soli Manzese huko! dawa imewaingia. me ni Gold bana.

eti nife ajili ya maku ya UMMA ?? Thubutu!! halafu kumbukeni kahirizi wanawake ni wachawi sana wa mapenzi akikuacha hakufungui!!! anataka uumie mnooo!! kosa alilofanya angempiga kimimba tu!!! akamkumbuke vizuri!!
This is big problem ila pengine ni ufinyu wa kipato ila baharia kama mm ni kufinya na kusepa.

Pia kuna watu yaani wamezaliwa kupenda,nina jamaa yangu ameachwa na wanawake mara tatu,,katika kumdadisi niligundua ni wale wanaume wanaopenda afu wanafanya makosa kwenye kutongoza yaani anatumia nguvu kubwa inakuwa kama anamlazimisha mwanamke sasa kwa staili hii na kuishi kwa kubembeleza lazima uachwe na ulie lie
 
Stori inafanana na yangu tofauti kusomesha na kufa tu
Hata mimi alikiwa Nesi, Hata mimi alipata kazi hospitali ya mkoa, hata mimi aliajiriwa mkoa mwingine

Tofauti ni kwamba alipozingua nilianza mimi kuoa mwingine, kama angeolewa kabla sijaoa labda ningedata na kufa pia
 
Back
Top Bottom