Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi?

HABaRI,
"witnessj,
Miaka mitatu unaanza kuvuna muda unavyozidi kwenda na mavuno yanaongezeka ni miche ya kubebeshwa ya muda mfupi,Hiyo ni fursa kama uko vizuri wahi,Soko lake wamesema Kuna watu wanazifata shambani zinakwenda Ulaya na america kwani kipindi cha msimu huko sehemu nyingine Duniani zinazozalisha Avocador msimu unakuwa umukwisha au bado.
Mashamba eka moja kununua ni kuanzia laki 1-2,Nilimuliza mtaalamu mmoja toka SUA (chuo cha kilimo cha sokoine-morogoro)Akaniambia kwa heka moja unaweza kupanda mpaka miti 100.

LUMUMBA
Mkuu nashawishika sana...wewe umeshaanza michakato?
 
Mkuu nashawishika sana...wewe umeshaanza michakato?

HABARI,
"witnessj,
Mimi nategemea kuanza mwaka huu Nimempa mtu kazi ya kutafuta shamba Kilolo,Mufindi,Makete na Njombe Nitaangalia wapi pa kupata shamba kubwa,Ninahitaji zaidi ya heka 50-100,Kwakuwa utaalamu wa kubebesha ninao kwenye miembe,mikorosho najua kwa Avocado ni sawa sawa.
Nasubiri majibu ya eneo kwanza.

Kwa ujumla soko ni kubwa sana kwa nchi za ulaya kama Denmark, Ufaransa, Uholanzi, Norway, Hispania na Uingereza,Kuna kampuni inaitwa Africado ndio ya kwanza tanzania kuanza kupeleka maparachichi ulaya.

LUMUMBA
 
Lakini makete haijabarikiwa wilaya ya kikuda sana just take it from me

Naungana nawe kabisaa makete sio sehemu salama na hapajabarikiwa kwa lingine zaidi ya Baridi kaliii na udongo usio na rutuba
 
HABARI,
"witnessj,
Mimi nategemea kuanza mwaka huu Nimempa mtu kazi ya kutafuta shamba Kilolo,Mufindi,Makete na Njombe Nitaangalia wapi pa kupata shamba kubwa,Ninahitaji zaidi ya heka 50-100,Kwakuwa utaalamu wa kubebesha ninao kwenye miembe,mikorosho najua kwa Avocado ni sawa sawa.
Nasubiri majibu ya eneo kwanza.

Kwa ujumla soko ni kubwa sana kwa nchi za ulaya kama Denmark, Ufaransa, Uholanzi, Norway, Hispania na Uingereza,Kuna kampuni inaitwa Africado ndio ya kwanza tanzania kuanza kupeleka maparachichi ulaya.

LUMUMBA
Nimekupm mkuu
 
Katika mizunguko yangu ya kazi nilitoka Morogoro nikaenda Mbeya kufanya shughuli zangu za kilimo hasa umwagiliaji, basi nikiwa Mbeya pale kwa kuwa mimi ni mdadisi nitampigia jamaa yangu mmoja ambae ni mwenyeji wa Mbeya pia ni Mkulima, duh jamaa mcheshi sana na ni mshikaji sana japokuwa ni msomi mkubwa na mfanyabiashara

Basi akanambia njoo huku Njombe,jioni ile nikapanda gari kuelekea huko, nilipofika nikakutana na jamaa ang mmoja niliesoma nae chuo akanipokea na akawa mwenyeji wangu.
Nilipompigia jamaa angu huyu Mkulima akanambia bado hajafika mjini ndio anatoka shamba, kumbuka hapo ni saa nne usiku.

Kesho yapo ikawa asubh , baridi ilikuwa kiasi japokuwa mwenyeji wangu alinambia ni wakati wa joto kwa sasa haaa haaaa Njombe kama ulaya vile

Kama saa moja hivi jamaa angu alikuja akanichukua , tukampitia na mshikaji wake mmoja , na safari ikaanza ya kuelekea nisikokujua kwenye nchi ya maziwa na Asali kama Mwendo wa 80km tukaanza kukwepana na milima ya Lupembe na baada ya muda mshikaji wangu akanambia hapa ndio tunaingia shamba, kwa kuwa lilikuwa shamba jipya lenye milima na milima , na lilikuwa Shamba kubwa kiasi , haaa haaa sio kubwa kama unavyofikiria ww ila ni zaidi ya hekari 400+ Virgin land , hapo hapo nikaanza udadisi wangu na kuanza kukumbuka nilivyokuwa nafundishwa na Maprofesa wangu enzi hizo nasoma pale SUA ,

Nilichoshangaa ni nn?
Katika udadisi wangu niligundua kuwa ile Ardhi haikuwahi kulimwa , mimea iliyoota maeneo Yale iliashiria rutuba ya ajabu iliyoko katika udongo ule , hali ya hewa na baadhi ya vitu vilionyesha kuwa eneo lile linapata mvua kubwa sana kwa mwaka tatribani 2300mm per yr
f8e30fe5a8f17a71a09ce3f3cca203a6.jpg

Organic matter layer ya Ardhi ile ni zaidi 40cm,
Nilichoshangaa zaidi ni pale nilipoenda ndani ya Shamba zaidi na kuona kuwa kuna chanzo kizuri cha maji , nilitamani niende kwetu Rombo niwachukue wale wazee niwalete pale kwa sababu kule sijawahi kuona kitu kama kile .
Bhasi nikaendelea na utafiti wangu nikagundua vitu vingi zaidi katika Ardhi ile na baada ya kukaa na kuangalia milima ikishangaa ujio wetu na muda ulikuwa umeenda , tukafanya baadhi ya kazi pale na kuanza kurudi

Ninachotaka kusema ni kwamba
Don't limit your mind to think
Seed and not diamond will make Africa great
Wekeza vzr kwenye kilimo
Uzi utakao fuata nitawaeleza katika hyo Ardhi ni nini kimepandwa na kinawezaje kumlipa Mkulima tena bila stress , najua utafikiri ni miti ya mbao lakini sio kweli ....stay tuned
Jumapili njema wana jamvi
inapendeza saana mkuu naomba muongozo wako wa kilimo cha mpunga na mboga mboga
 
Umeishia kujipiga picha wewe badala ya fursa za hapo NJOMBE. Mibongo sisi tumirogwa na nani?
 
Umeishia kujipiga picha wewe badala ya fursa za hapo NJOMBE. Mibongo sisi tumirogwa na nani?

HABARI,
"andreakalima,
Comrade hayo maneno uliyoandika sio ustarabu kabisa yeye amepiga picha kuonyesha uhalisia wa eneo unajuaje kama tayari ameshafanya uwekezaji hapo,Ni vema ukamuuliza badala ya kutoa maneno ya kejeli.

LUMUMBA
 
Katika mizunguko yangu ya kazi nilitoka Morogoro nikaenda Mbeya kufanya shughuli zangu za kilimo hasa umwagiliaji, basi nikiwa Mbeya pale kwa kuwa mimi ni mdadisi nitampigia jamaa yangu mmoja ambae ni mwenyeji wa Mbeya pia ni Mkulima, duh jamaa mcheshi sana na ni mshikaji sana japokuwa ni msomi mkubwa na mfanyabiashara

Basi akanambia njoo huku Njombe,jioni ile nikapanda gari kuelekea huko, nilipofika nikakutana na jamaa ang mmoja niliesoma nae chuo akanipokea na akawa mwenyeji wangu.
Nilipompigia jamaa angu huyu Mkulima akanambia bado hajafika mjini ndio anatoka shamba, kumbuka hapo ni saa nne usiku.

Kesho yapo ikawa asubh , baridi ilikuwa kiasi japokuwa mwenyeji wangu alinambia ni wakati wa joto kwa sasa haaa haaaa Njombe kama ulaya vile

Kama saa moja hivi jamaa angu alikuja akanichukua , tukampitia na mshikaji wake mmoja , na safari ikaanza ya kuelekea nisikokujua kwenye nchi ya maziwa na Asali kama Mwendo wa 80km tukaanza kukwepana na milima ya Lupembe na baada ya muda mshikaji wangu akanambia hapa ndio tunaingia shamba, kwa kuwa lilikuwa shamba jipya lenye milima na milima , na lilikuwa Shamba kubwa kiasi , haaa haaa sio kubwa kama unavyofikiria ww ila ni zaidi ya hekari 400+ Virgin land , hapo hapo nikaanza udadisi wangu na kuanza kukumbuka nilivyokuwa nafundishwa na Maprofesa wangu enzi hizo nasoma pale SUA ,

Nilichoshangaa ni nn?
Katika udadisi wangu niligundua kuwa ile Ardhi haikuwahi kulimwa , mimea iliyoota maeneo Yale iliashiria rutuba ya ajabu iliyoko katika udongo ule , hali ya hewa na baadhi ya vitu vilionyesha kuwa eneo lile linapata mvua kubwa sana kwa mwaka tatribani 2300mm per yr
f8e30fe5a8f17a71a09ce3f3cca203a6.jpg

Organic matter layer ya Ardhi ile ni zaidi 40cm,
Nilichoshangaa zaidi ni pale nilipoenda ndani ya Shamba zaidi na kuona kuwa kuna chanzo kizuri cha maji , nilitamani niende kwetu Rombo niwachukue wale wazee niwalete pale kwa sababu kule sijawahi kuona kitu kama kile .
Bhasi nikaendelea na utafiti wangu nikagundua vitu vingi zaidi katika Ardhi ile na baada ya kukaa na kuangalia milima ikishangaa ujio wetu na muda ulikuwa umeenda , tukafanya baadhi ya kazi pale na kuanza kurudi

Ninachotaka kusema ni kwamba
Don't limit your mind to think
Seed and not diamond will make Africa great
Wekeza vzr kwenye kilimo
Uzi utakao fuata nitawaeleza katika hyo Ardhi ni nini kimepandwa na kinawezaje kumlipa Mkulima tena bila stress , najua utafikiri ni miti ya mbao lakini sio kweli ....stay tuned
Jumapili njema wana jamvi

NIMEAMUA KURUDI TENA NJOMBE KUENDELEA NA UCHUNGUZI WANGU
Salama wana jamvi tar 26 mwezi wa nne mwaka jana(2017) niliandika uzi mmoja kuhusu siku yangu ya kwanza kufika katika mji wa njombe na nikaeleza uzuri ulio katika mji ule pamoja na vijiji vyake , pia nikaeleza fursa nilizoziona kule

Sasa leo naomba niwaeleze kidogo, baada ya kuona uzuri wa nchi ile ya njombe na vijiji vyake vilivyojaa utajiri juu ya milima na mabonde nilimaliza kazi iliyonipeleka na nikarudi zangu Morogoro kuendelea na shughuli zangu za ufundi huku akili yangu ikiwaza ni kwa namna gani nitaweza kurudi tena katika ardhi ile ili nifanye upembuzi zaidi na lengo langu ni kugundua vitu flani katika eneo lile kwa ajili ya uwekezaji

Basi mwanzoni mwa mwezi April mwaka huu nilipokea tena ujumbe kutoka kwa mwekezaji mmoja tena maeneo yale na alikuwa anahitaji huduma yangu lakini hii ilikuwa tofauti na ile ya kipindi kile na ilikuwa kubwa kidogo , basi nikamjibu ba kumwambia ya kuwa ningeenda tena njombe katikati ya mwezi wa nne kwa ajili ya kazi yake hiyo , uzuri ni kwamba huyu mwekezaji ananiani na anajua siwezi kumwangusha kwenye kazi yake na hua tunawasiliana na ananishauri mambo mbali mbali kwa sababu yeye ni mhenga kidogo kuliko mimi.

Siku zikazidi kwenda na ndani ya mwezi ule nikasafiri gafla kwenda nje ya nchi kwa shughuli za biashara kwani ilinilazimu kufanya hivyo na nikamuahidi mteja wangu kuwa soon nikirudi ningeenda Njombe kwa ajili ya kazi yake na akakubali kwa kuwa ni mwelewa sana.

Nikafanikiwa kurudi mapema na ilipofika tar 29 april mwaka huu nilianza tena safari ya kuelekea Njombe kwa ajili ya kazi huku nikiwa na shauku kubwa ya kuendelea kuyasoma mazingira ya njombe vyema hasa kwenye vijiji vyake na maeneo ya mbali kidogo na mji. Nilipokelewa Vyema na mwenyeji wangu ambae tulisoma wote Chuo kikuu pale SUA miaka hiyo kwa sababu aliniomba tuonana nilipompa taarifa ya kwamba nitafika Njombe

Baridi ilikuwa kali sana kwangu kwa sababu nilikuwa sijabeba sweta lakini mwenyeji wangu aliniambia kuwa kipindi cha baridi bado hakijaanza ( Jiografia ya Njombe ni kwamba iko kwenye mwinuko upatao zaidi ya 1700m kutoka usawa wa bahari na annual mean temperature ni 22 degrees of Celsius na wakati mwinginie joto huwa chini sana mpka kufikia nyuzi joto 5-8 kipindi cha baridi kali) wakati naingia Njombe joto lilikuwa nyuzi joto 18 tu. hali hii ya hewa ilinifanya niendelee kuwaza zaidi kuhusu eneo hili

Kesho yake Tuliamka vzr na kuanza kazi au Ziara ya kuzunguka kwenye vijiji nje kidogo ya mji na mgeni wangu alinikutanisha na kichwa mmoja hapa JF ambae amewekeza sana kwa upande wa Njombe na Makete nilifurahi sana kukutana na huyu jamaa kwa sababu ni mtu makini sana na mwenye akili ya kuwaza tofauti

Tulitembea kwenye maeneo ya Matebwe, Lupembe, Mfriga, madeke, Ikondo na tuliweza kumaliza kazi salama na kurudi mjini

Next thread nitaelezea sasa upembuzi wangu mfano nitaeleza namna Ardhi wa maeneo haya ilivyo na udongo wenye rutuba na wa aina yake kuliko maeneo mengi ambayo tumekuwa tukifanya kazi kwa sababu tuliuchua udongo wa maeneo hayo na kuupima kwa kina kweli kweli huku tukifanya comparison na maeneo mengine ya nchi hii kwa kuwa kampuni yetu ina database kubwa ya udongo wa nchi hii kutokana na huduma zetu za soil test

nitaeleza fursa kubwa ya kilimo cha parachichi na pia nitaeleza vzr kuhusu namna zao la chai linavyozidi kumuumiza na kumpa mkulima deni la maisha pia nitaeleza nilipokutana na mbunge wa Njombe, Lupembe na Makete
my-drive

1UnSZTxnOJdr9xzrAxwBigHTXzu0NsmBe
 
74 Reactions
Reply
Back
Top Bottom