Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi? | Page 7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Lasway.Jr, Oct 29, 2017.

 1. Lasway.Jr

  Lasway.Jr Senior Member

  #1
  Oct 29, 2017
  Joined: Jul 25, 2015
  Messages: 172
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 80
  Katika mizunguko yangu ya kazi nilitoka Morogoro nikaenda Mbeya kufanya shughuli zangu za kilimo hasa umwagiliaji, basi nikiwa Mbeya pale kwa kuwa mimi ni mdadisi nitampigia jamaa yangu mmoja ambae ni mwenyeji wa Mbeya pia ni Mkulima, duh jamaa mcheshi sana na ni mshikaji sana japokuwa ni msomi mkubwa na mfanyabiashara

  Basi akanambia njoo huku Njombe,jioni ile nikapanda gari kuelekea huko, nilipofika nikakutana na jamaa ang mmoja niliesoma nae chuo akanipokea na akawa mwenyeji wangu.
  Nilipompigia jamaa angu huyu Mkulima akanambia bado hajafika mjini ndio anatoka shamba, kumbuka hapo ni saa nne usiku.

  Kesho yapo ikawa asubh , baridi ilikuwa kiasi japokuwa mwenyeji wangu alinambia ni wakati wa joto kwa sasa haaa haaaa Njombe kama ulaya vile

  Kama saa moja hivi jamaa angu alikuja akanichukua , tukampitia na mshikaji wake mmoja , na safari ikaanza ya kuelekea nisikokujua kwenye nchi ya maziwa na Asali kama Mwendo wa 80km tukaanza kukwepana na milima ya Lupembe na baada ya muda mshikaji wangu akanambia hapa ndio tunaingia shamba, kwa kuwa lilikuwa shamba jipya lenye milima na milima , na lilikuwa Shamba kubwa kiasi , haaa haaa sio kubwa kama unavyofikiria ww ila ni zaidi ya hekari 400+ Virgin land , hapo hapo nikaanza udadisi wangu na kuanza kukumbuka nilivyokuwa nafundishwa na Maprofesa wangu enzi hizo nasoma pale SUA ,

  Nilichoshangaa ni nn?
  Katika udadisi wangu niligundua kuwa ile Ardhi haikuwahi kulimwa , mimea iliyoota maeneo Yale iliashiria rutuba ya ajabu iliyoko katika udongo ule , hali ya hewa na baadhi ya vitu vilionyesha kuwa eneo lile linapata mvua kubwa sana kwa mwaka tatribani 2300mm per yr
  [​IMG]

  Organic matter layer ya Ardhi ile ni zaidi 40cm,
  Nilichoshangaa zaidi ni pale nilipoenda ndani ya Shamba zaidi na kuona kuwa kuna chanzo kizuri cha maji , nilitamani niende kwetu Rombo niwachukue wale wazee niwalete pale kwa sababu kule sijawahi kuona kitu kama kile .
  Bhasi nikaendelea na utafiti wangu nikagundua vitu vingi zaidi katika Ardhi ile na baada ya kukaa na kuangalia milima ikishangaa ujio wetu na muda ulikuwa umeenda , tukafanya baadhi ya kazi pale na kuanza kurudi

  Ninachotaka kusema ni kwamba
  Don't limit your mind to think
  Seed and not diamond will make Africa great
  Wekeza vzr kwenye kilimo
  Uzi utakao fuata nitawaeleza katika hyo Ardhi ni nini kimepandwa na kinawezaje kumlipa Mkulima tena bila stress , najua utafikiri ni miti ya mbao lakini sio kweli ....stay tuned
  Jumapili njema wana jamvi
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #121
  Dec 29, 2017
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,483
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  Asante sana,
  Nimekuja, ila sikuwa nimeuona huu uzi ngoja niusome vizuri
   
 3. pemgtoonet.com

  pemgtoonet.com JF-Expert Member

  #122
  Jan 1, 2018
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 515
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 60
  Bei ya eka 1 inaanzia laki na nusu na kuendelea...
   
 4. said mgalla

  said mgalla Member

  #123
  Jan 4, 2018
  Joined: Jan 4, 2018
  Messages: 24
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  Chardams tubebane BC ndugu yangu kwenye hayo mashirika yako
   
 5. said mgalla

  said mgalla Member

  #124
  Jan 4, 2018
  Joined: Jan 4, 2018
  Messages: 24
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  Broo tupeane michongo hiyo mm nipo himo Kilimanjaro
   
 6. pemgtoonet.com

  pemgtoonet.com JF-Expert Member

  #125
  Feb 19, 2018
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 515
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 60
  Ibukia Njombe,...Mbona mambo simpo tu
   
 7. DUBULIHASA

  DUBULIHASA JF-Expert Member

  #126
  Feb 19, 2018
  Joined: Nov 26, 2016
  Messages: 1,846
  Likes Received: 1,860
  Trophy Points: 280
  Waache wapoteze muda mkuu, madaraja hayawez yakapanda wala kuvuna chini ya utawala Wa shetani Magfl
   
 8. PatriceLumumba

  PatriceLumumba JF-Expert Member

  #127
  Feb 19, 2018
  Joined: Mar 9, 2016
  Messages: 399
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 80
  HABARI,
  Kamanda nina Ndugu yangu anataka kuja huko ana MIL.3.5 Zao gani la biashara litamfaa kuanzia aweze kurudisha pesa yake na Kuendelea na kilimo.

  LUMUMBA
   
 9. sengobad

  sengobad JF-Expert Member

  #128
  Feb 20, 2018
  Joined: Aug 13, 2017
  Messages: 828
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 80
  Hiv wewe unadhan mkulima mzungu aliyoko ulaya akija tz anaweza kuendeleza kilimo chake na akatajirika ? Serikali yako kama ni maskini na we mwananchi utakuwa masikin tuu!
   
 10. PatriceLumumba

  PatriceLumumba JF-Expert Member

  #129
  Feb 20, 2018
  Joined: Mar 9, 2016
  Messages: 399
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 80
  HABARI,
  "sengobad,
  Hayo maneno yako yana ukweli ndani yake ila si kwa ukubwa hivyo hapa tunazungumzia kilimo kuondoa umasikini,sio kuwa tajiri tunajua nchi za ulaya marekani na uchina kuna mambo ya ruzuku N.k.
  Hapa kwetu leo umeshuhudia wakulima wa korosho wanavyo pata hela ila najua wanaofaidika sana ni wafanyabiashara ambao ni walanguzi na wanyonyaji wakubwa sana.Tukubaliane swala la umasikini kilimo kinaondoa ila kutajirika hiyo ni jitihada nyingine lazima uwe tajiri ili uzidi kuwa tajiri kwenye kilimo.

  LUMUMBA
   
 11. TsafuRD

  TsafuRD JF-Expert Member

  #130
  Feb 20, 2018
  Joined: Sep 29, 2013
  Messages: 1,382
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Kwani kwa akili yako anatoka Kilimanjaro kwenda Njombe kulima kwa ajili ya njaa ya tumbo? Kwani ni lazima mazao ayasafirishe hadi Moshi? Kama ni mbao mbona soko la Mbao ni kumbwa zaidi Dar na kwingineko, kwa nini aende Moshi tena. Let us think outside the box na tusiwe waoga sana.
   
 12. pemgtoonet.com

  pemgtoonet.com JF-Expert Member

  #131
  Feb 20, 2018
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 515
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 60
  Kule dili kubwa kwa sasa ni kulima parachich,zinaenda ulaya kwa bei tamu.Na zinauzwa sana kwakua kipindi dunian kote,parachich znakuwa adimu,njombe ndo znakomaa.So ulaya na kwingneko wanahamia njombe
   
 13. pemgtoonet.com

  pemgtoonet.com JF-Expert Member

  #132
  Feb 20, 2018
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 515
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 60
  Au mbao,unajumua kwa 2500-4000,unauza kwa 6000 had 7000
   
 14. PatriceLumumba

  PatriceLumumba JF-Expert Member

  #133
  Feb 20, 2018
  Joined: Mar 9, 2016
  Messages: 399
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 80
  HABARI,
  "pemgtoonet.com,
  Asante zinachukua muda gani kupanda mpaka kuanza kuvuna na heka moja ni sh.ngapi.

  LUMUMBA
   
 15. pemgtoonet.com

  pemgtoonet.com JF-Expert Member

  #134
  Feb 20, 2018
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 515
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 60
  Miaka 3 unaanza vuna,eka kuanzia lak 2
   
 16. PatriceLumumba

  PatriceLumumba JF-Expert Member

  #135
  Feb 20, 2018
  Joined: Mar 9, 2016
  Messages: 399
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 80
  HABARI,
  Asante sana Kwa taarifa Hizo ni zile mbegu za muda mfupi ok sawa ila uhakika wa soko ni mkubwa? na wanunuzi wanafata shambani au Mlimaji unapeleka sokoni?.

  LUMUMBA
   
 17. pemgtoonet.com

  pemgtoonet.com JF-Expert Member

  #136
  Feb 21, 2018
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 515
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 60
  Wanafuata mzgo shamba,...Wanakuletea matrei ujaze humo,mnaenda nayo kupima ofisin kwao
   
 18. witnessj

  witnessj JF-Expert Member

  #137
  Feb 21, 2018
  Joined: Mar 22, 2015
  Messages: 7,544
  Likes Received: 9,539
  Trophy Points: 280
  Ni sehemu gani hiyo mkuu?
   
 19. PatriceLumumba

  PatriceLumumba JF-Expert Member

  #138
  Feb 21, 2018
  Joined: Mar 9, 2016
  Messages: 399
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 80
  HABARI,
  "witnessj,
  Ndugu huko ni njombe jaribu kusoma Heading ya post(kichwa cha habari cha ujembe)

  LUMUMBA
   
 20. witnessj

  witnessj JF-Expert Member

  #139
  Feb 22, 2018
  Joined: Mar 22, 2015
  Messages: 7,544
  Likes Received: 9,539
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kulima avocador zinachukua mda gani?
   
 21. PatriceLumumba

  PatriceLumumba JF-Expert Member

  #140
  Feb 22, 2018
  Joined: Mar 9, 2016
  Messages: 399
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 80
  HABaRI,
  "witnessj,
  Miaka mitatu unaanza kuvuna muda unavyozidi kwenda na mavuno yanaongezeka ni miche ya kubebeshwa ya muda mfupi,Hiyo ni fursa kama uko vizuri wahi,Soko lake wamesema Kuna watu wanazifata shambani zinakwenda Ulaya na america kwani kipindi cha msimu huko sehemu nyingine Duniani zinazozalisha Avocador msimu unakuwa umukwisha au bado.
  Mashamba eka moja kununua ni kuanzia laki 1-2,Nilimuliza mtaalamu mmoja toka SUA (chuo cha kilimo cha sokoine-morogoro)Akaniambia kwa heka moja unaweza kupanda mpaka miti 100.

  LUMUMBA
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...