Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi?

Nchi yote imebarikiwa sana basi tu sisi wenyewe akili zetu mgando
 
Mbona Lasway Kala Ban?? Uzi mzuri Sana huu. Kaharibu wapi??
 
welcome again mkuu and next time uje na warombo wenzio kama kumi ivi mfanye uwekezaji hamtojuta.
 
Ngoja niusubiri uzi wa tatu mie,huo wa pili haunihusu,ntasubiri uzi watatu utakao kuja nao kuhusu "UNAUZA SHAMBA LA HEKA 100 NJOMBE"
 
Katika mizunguko yangu ya kazi nilitoka Morogoro nikaenda Mbeya kufanya shughuli zangu za kilimo hasa umwagiliaji, basi nikiwa Mbeya pale kwa kuwa mimi ni mdadisi nitampigia jamaa yangu mmoja ambae ni mwenyeji wa Mbeya pia ni Mkulima, duh jamaa mcheshi sana na ni mshikaji sana japokuwa ni msomi mkubwa na mfanyabiashara

Basi akanambia njoo huku Njombe,jioni ile nikapanda gari kuelekea huko, nilipofika nikakutana na jamaa ang mmoja niliesoma nae chuo akanipokea na akawa mwenyeji wangu.
Nilipompigia jamaa angu huyu Mkulima akanambia bado hajafika mjini ndio anatoka shamba, kumbuka hapo ni saa nne usiku.

Kesho yapo ikawa asubh , baridi ilikuwa kiasi japokuwa mwenyeji wangu alinambia ni wakati wa joto kwa sasa haaa haaaa Njombe kama ulaya vile

Kama saa moja hivi jamaa angu alikuja akanichukua , tukampitia na mshikaji wake mmoja , na safari ikaanza ya kuelekea nisikokujua kwenye nchi ya maziwa na Asali kama Mwendo wa 80km tukaanza kukwepana na milima ya Lupembe na baada ya muda mshikaji wangu akanambia hapa ndio tunaingia shamba, kwa kuwa lilikuwa shamba jipya lenye milima na milima , na lilikuwa Shamba kubwa kiasi , haaa haaa sio kubwa kama unavyofikiria ww ila ni zaidi ya hekari 400+ Virgin land , hapo hapo nikaanza udadisi wangu na kuanza kukumbuka nilivyokuwa nafundishwa na Maprofesa wangu enzi hizo nasoma pale SUA ,

Nilichoshangaa ni nn?
Katika udadisi wangu niligundua kuwa ile Ardhi haikuwahi kulimwa , mimea iliyoota maeneo Yale iliashiria rutuba ya ajabu iliyoko katika udongo ule , hali ya hewa na baadhi ya vitu vilionyesha kuwa eneo lile linapata mvua kubwa sana kwa mwaka tatribani 2300mm per yr
f8e30fe5a8f17a71a09ce3f3cca203a6.jpg

Organic matter layer ya Ardhi ile ni zaidi 40cm,
Nilichoshangaa zaidi ni pale nilipoenda ndani ya Shamba zaidi na kuona kuwa kuna chanzo kizuri cha maji , nilitamani niende kwetu Rombo niwachukue wale wazee niwalete pale kwa sababu kule sijawahi kuona kitu kama kile .
Bhasi nikaendelea na utafiti wangu nikagundua vitu vingi zaidi katika Ardhi ile na baada ya kukaa na kuangalia milima ikishangaa ujio wetu na muda ulikuwa umeenda , tukafanya baadhi ya kazi pale na kuanza kurudi

Ninachotaka kusema ni kwamba
Don't limit your mind to think
Seed and not diamond will make Africa great
Wekeza vzr kwenye kilimo
Uzi utakao fuata nitawaeleza katika hyo Ardhi ni nini kimepandwa na kinawezaje kumlipa Mkulima tena bila stress , najua utafikiri ni miti ya mbao lakini sio kweli ....stay tuned
Jumapili njema wana jamvi

HABARI,
Lasway.Jr,
Hongera sana comrade kwa kuleta taarifa njema kwa wapenda maendeleo,mabadiliko na kujituma,Kitu ulichokileta hapa ni kikumbwa sana tena nadhani ni zaidi ya jinsi unavyo fikiria.
Pia nakupa hongera kwa kupita SUA kwani hauna tofauti na mada yako hapa MATUSI, KEJERI NA MANENO YOTE YA KUKUDHARAU ,Tafadhali yasikurudishe nyuma hizo ndizo changamoto na hao watu wapo kila sehemu sio huku tu.
Pia nikupongeze kwa moyo wako wa kuwashirikisha na wengine pale unapoona kuna fulsa.
Ulichokisema ni kweli kabisa ardhi ndio kila kitu wewe endelea kuleta taarifa za kutosha watu wengi wapo watajitokeza na mtafanya mawasiliano mtasonga mbele comrade..
Pia kwa eneo kama hilo ulilosema fikiriapia kulima kilimo cha maharage machanga(fresh beans)yana soko sana kenya,Ila pia nitaweka taarifa kuna ma agent wa makampuni toka QUTAR watakuja africa mashariki kutafuta vyanzo vya kupata mazao ya mbogamboga hasa kutokana na mgogoro wao wa kutengwa nchi za kiarabu kwahiyo kuna soko kubwa la mbogamboga la uhakika linakuja.

LUMUMBA
 
NEGATIVITY ni type ya ukipofu pia mkuu
pole sana
MAKETE is a good place take it or leave it
Makete INA uzuri gani bwana mbona hilo swala liko wazi kabisaa takataka tu kule, it not negativity it just a simple fact
 
Hapa nchini Tanzani kuna baadhi ya maeneo ni mazuri sana ya kuishi.
Vijana wengi wanaomaliza vyuo hapa nchini huwa wanapenda kuishi mijini. Kwakuwa nchi yetu Mtanzania anaruhusiwa kuishi popote pale, ilikua vyema kwa vijana wenye nguvu ya kazi wakachagua kuhama ktk maeneo yenye Ukame na kwenda kuishi ktk maeneo mazuri yatakayo wawezesha kuishi na kuzalisha.
 
Katika mizunguko yangu ya kazi nilitoka Morogoro nikaenda Mbeya kufanya shughuli zangu za kilimo hasa umwagiliaji, basi nikiwa Mbeya pale kwa kuwa mimi ni mdadisi nitampigia jamaa yangu mmoja ambae ni mwenyeji wa Mbeya pia ni Mkulima, duh jamaa mcheshi sana na ni mshikaji sana japokuwa ni msomi mkubwa na mfanyabiashara

Basi akanambia njoo huku Njombe,jioni ile nikapanda gari kuelekea huko, nilipofika nikakutana na jamaa ang mmoja niliesoma nae chuo akanipokea na akawa mwenyeji wangu.
Nilipompigia jamaa angu huyu Mkulima akanambia bado hajafika mjini ndio anatoka shamba, kumbuka hapo ni saa nne usiku.

Kesho yapo ikawa asubh , baridi ilikuwa kiasi japokuwa mwenyeji wangu alinambia ni wakati wa joto kwa sasa haaa haaaa Njombe kama ulaya vile

Kama saa moja hivi jamaa angu alikuja akanichukua , tukampitia na mshikaji wake mmoja , na safari ikaanza ya kuelekea nisikokujua kwenye nchi ya maziwa na Asali kama Mwendo wa 80km tukaanza kukwepana na milima ya Lupembe na baada ya muda mshikaji wangu akanambia hapa ndio tunaingia shamba, kwa kuwa lilikuwa shamba jipya lenye milima na milima , na lilikuwa Shamba kubwa kiasi , haaa haaa sio kubwa kama unavyofikiria ww ila ni zaidi ya hekari 400+ Virgin land , hapo hapo nikaanza udadisi wangu na kuanza kukumbuka nilivyokuwa nafundishwa na Maprofesa wangu enzi hizo nasoma pale SUA ,

Nilichoshangaa ni nn?
Katika udadisi wangu niligundua kuwa ile Ardhi haikuwahi kulimwa , mimea iliyoota maeneo Yale iliashiria rutuba ya ajabu iliyoko katika udongo ule , hali ya hewa na baadhi ya vitu vilionyesha kuwa eneo lile linapata mvua kubwa sana kwa mwaka tatribani 2300mm per yr
f8e30fe5a8f17a71a09ce3f3cca203a6.jpg

Organic matter layer ya Ardhi ile ni zaidi 40cm,
Nilichoshangaa zaidi ni pale nilipoenda ndani ya Shamba zaidi na kuona kuwa kuna chanzo kizuri cha maji , nilitamani niende kwetu Rombo niwachukue wale wazee niwalete pale kwa sababu kule sijawahi kuona kitu kama kile .
Bhasi nikaendelea na utafiti wangu nikagundua vitu vingi zaidi katika Ardhi ile na baada ya kukaa na kuangalia milima ikishangaa ujio wetu na muda ulikuwa umeenda , tukafanya baadhi ya kazi pale na kuanza kurudi

Ninachotaka kusema ni kwamba
Don't limit your mind to think
Seed and not diamond will make Africa great
Wekeza vzr kwenye kilimo
Uzi utakao fuata nitawaeleza katika hyo Ardhi ni nini kimepandwa na kinawezaje kumlipa Mkulima tena bila stress , najua utafikiri ni miti ya mbao lakini sio kweli ....stay tuned
Jumapili njema wana jamvi
Mbona amekula BAN
 
Back
Top Bottom