Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikuamini nilivyofika Njombe, kumbe Tanzania hii kuna sehemu kama hizi?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Lasway.Jr, Oct 29, 2017.

 1. Lasway.Jr

  Lasway.Jr Senior Member

  #1
  Oct 29, 2017
  Joined: Jul 25, 2015
  Messages: 172
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 80
  Katika mizunguko yangu ya kazi nilitoka Morogoro nikaenda Mbeya kufanya shughuli zangu za kilimo hasa umwagiliaji, basi nikiwa Mbeya pale kwa kuwa mimi ni mdadisi nitampigia jamaa yangu mmoja ambae ni mwenyeji wa Mbeya pia ni Mkulima, duh jamaa mcheshi sana na ni mshikaji sana japokuwa ni msomi mkubwa na mfanyabiashara

  Basi akanambia njoo huku Njombe,jioni ile nikapanda gari kuelekea huko, nilipofika nikakutana na jamaa ang mmoja niliesoma nae chuo akanipokea na akawa mwenyeji wangu.
  Nilipompigia jamaa angu huyu Mkulima akanambia bado hajafika mjini ndio anatoka shamba, kumbuka hapo ni saa nne usiku.

  Kesho yapo ikawa asubh , baridi ilikuwa kiasi japokuwa mwenyeji wangu alinambia ni wakati wa joto kwa sasa haaa haaaa Njombe kama ulaya vile

  Kama saa moja hivi jamaa angu alikuja akanichukua , tukampitia na mshikaji wake mmoja , na safari ikaanza ya kuelekea nisikokujua kwenye nchi ya maziwa na Asali kama Mwendo wa 80km tukaanza kukwepana na milima ya Lupembe na baada ya muda mshikaji wangu akanambia hapa ndio tunaingia shamba, kwa kuwa lilikuwa shamba jipya lenye milima na milima , na lilikuwa Shamba kubwa kiasi , haaa haaa sio kubwa kama unavyofikiria ww ila ni zaidi ya hekari 400+ Virgin land , hapo hapo nikaanza udadisi wangu na kuanza kukumbuka nilivyokuwa nafundishwa na Maprofesa wangu enzi hizo nasoma pale SUA ,

  Nilichoshangaa ni nn?
  Katika udadisi wangu niligundua kuwa ile Ardhi haikuwahi kulimwa , mimea iliyoota maeneo Yale iliashiria rutuba ya ajabu iliyoko katika udongo ule , hali ya hewa na baadhi ya vitu vilionyesha kuwa eneo lile linapata mvua kubwa sana kwa mwaka tatribani 2300mm per yr
  [​IMG]

  Organic matter layer ya Ardhi ile ni zaidi 40cm,
  Nilichoshangaa zaidi ni pale nilipoenda ndani ya Shamba zaidi na kuona kuwa kuna chanzo kizuri cha maji , nilitamani niende kwetu Rombo niwachukue wale wazee niwalete pale kwa sababu kule sijawahi kuona kitu kama kile .
  Bhasi nikaendelea na utafiti wangu nikagundua vitu vingi zaidi katika Ardhi ile na baada ya kukaa na kuangalia milima ikishangaa ujio wetu na muda ulikuwa umeenda , tukafanya baadhi ya kazi pale na kuanza kurudi

  Ninachotaka kusema ni kwamba
  Don't limit your mind to think
  Seed and not diamond will make Africa great
  Wekeza vzr kwenye kilimo
  Uzi utakao fuata nitawaeleza katika hyo Ardhi ni nini kimepandwa na kinawezaje kumlipa Mkulima tena bila stress , najua utafikiri ni miti ya mbao lakini sio kweli ....stay tuned
  Jumapili njema wana jamvi
   
 2. Expected Value

  Expected Value JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2017
  Joined: Mar 29, 2016
  Messages: 746
  Likes Received: 754
  Trophy Points: 180
  Yaani bongo tuna mavitu adimu mengi sana ya kufanya, sema watu watakwambia hawana "exposure".
   
 3. Lasway.Jr

  Lasway.Jr Senior Member

  #3
  Oct 29, 2017
  Joined: Jul 25, 2015
  Messages: 172
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 80
  Sio exposure tuu, pia watu ni wavivu kufikiri na kuchukua hatua
   
 4. NIGGA

  NIGGA JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2017
  Joined: Jan 23, 2013
  Messages: 1,253
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hali ya hewa ya njombe ni zaidi ya ulaya!ukanda ule wamebarikiwa sana
   
 5. darcity

  darcity JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2017
  Joined: Jul 20, 2009
  Messages: 3,925
  Likes Received: 5,412
  Trophy Points: 280
  Kwenye kuanza kilimo kuna kuwa na matumaini mengi makubwa mkuu. Matokeo ndio jibu sahihi la mafanikio au changamoto. Kila la kheri katika uwekezaji wako mpya
   
 6. mjumbe wa bwana

  mjumbe wa bwana JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2017
  Joined: Sep 19, 2016
  Messages: 3,392
  Likes Received: 2,753
  Trophy Points: 280
  kutoa mzigo hapo mbea mpk Kilimanjaro unakutana na wakala wangap wa misitu huko barabarani na ni hela kiasi gani utawaachia
  alafu pili refer wakulima wa mbaazi utajua kwa nn watu wengi wanalima kwa mitego mitego
   
 7. Mchoraji Cyper255

  Mchoraji Cyper255 JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2017
  Joined: Nov 21, 2012
  Messages: 1,436
  Likes Received: 5,113
  Trophy Points: 280
  Juzi Rais alisema, kuzaliwa Tanzania ni fursa. Watu wakaanza kumponda
   
 8. Saguda47

  Saguda47 JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2017
  Joined: May 1, 2016
  Messages: 5,459
  Likes Received: 5,787
  Trophy Points: 280
  hayo ndo mambo ya msingi asee!! sio kila siku vijana kujadili mambo ambayo hayana hata faida kwetu, bado tuna ardhi kubwa ambayo ni idle, tutafuteni fursa popote ndani ya ardhi ya Tanzania yetu yenye amani na upendo.
   
 9. chaliifrancisco

  chaliifrancisco JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2017
  Joined: Jan 17, 2015
  Messages: 3,900
  Likes Received: 5,737
  Trophy Points: 280
  Kwani ukilima Mbeya lazima usafurishe mzigo kwenda Kilimanjaro?
   
 10. Econometrician

  Econometrician JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2017
  Joined: Oct 25, 2013
  Messages: 8,686
  Likes Received: 7,991
  Trophy Points: 280
  itakuwa amelima chai, parachichi ,au Nanasi
   
 11. Ngushi

  Ngushi JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2017
  Joined: Jul 8, 2016
  Messages: 7,174
  Likes Received: 13,635
  Trophy Points: 280
  Ni kweli njombe Kuna ardhi nzuri sana!!
   
 12. Malcom Lumumba

  Malcom Lumumba JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2017
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 9,459
  Likes Received: 24,795
  Trophy Points: 280
  Mkuu Njombe cha mtoto sana mimi nafanya kilimo sehemu moja inaitwa Kidabaga iko Iringa huko. Ni balaa sana na hali ya hewa ni kama Ulaya, zamani Mahindi walikuwa hawapandii mbolea.

  Sema tunapana vikumbo na makampuni makubwa kama New Forest na wale wa One Acre Fund. Wanamiliki maeneo makubwa sana na Raisi Kikwete aliwapa tu; Inafika kipindi wananyanyasa wazawa na kuchoma mashamba yao ya miti kwa maksudi pindi ukikataa kuwauzia.

  Nawashauri vijana watembee na kuwekeza huko. It is a nice place to invest: jaribu kwenda kufanya utafiti mkuu

  NB: Kuna vibarua wengi sana wa bei nafuu na Wahehe wengi ni watu waaminifu sana endapo utawapa stahiki zao kwa wakati.
   
 13. luginyo

  luginyo JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2017
  Joined: May 26, 2013
  Messages: 1,259
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Lakini makete haijabarikiwa wilaya ya kikuda sana just take it from me
   
 14. busy bees

  busy bees JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2017
  Joined: Aug 26, 2016
  Messages: 2,265
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Na wengi wetu wanakesha mitandaoni wakilalamika eti MADARAJA MBONA HAYAPANDI .... ni ajabu sana
   
 15. jembelamkono

  jembelamkono JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2017
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 2,292
  Likes Received: 1,324
  Trophy Points: 280
  Hahaas mkuu umenchekesha sana,ati wilaya ya kikuda..
   
 16. busy bees

  busy bees JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2017
  Joined: Aug 26, 2016
  Messages: 2,265
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Nadhani hajasoma ile iitwayo ENTREPRENEURSHIP AND MARKETING .... lakin pia AKILI YA KUZALIWA na pia KUJIONGEZA vyaweza tumika
   
 17. busy bees

  busy bees JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2017
  Joined: Aug 26, 2016
  Messages: 2,265
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Challenge hiyo hasa KUCHOMEWA MAENEO ya hizo TAASISI waisemeaje kiongozi
   
 18. Ngushi

  Ngushi JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2017
  Joined: Jul 8, 2016
  Messages: 7,174
  Likes Received: 13,635
  Trophy Points: 280
  Ni eneo zuri sana mkuu! Kuna ardhi safi sana wilaya ya kilolo
   
 19. kawombe

  kawombe JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2017
  Joined: Mar 26, 2015
  Messages: 2,493
  Likes Received: 1,238
  Trophy Points: 280
  Iko poa sana
   
 20. melchior

  melchior JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2017
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 217
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Parachichi
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...