Siku zote watu wangekuwa na mawazo kama haya

mayange

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
701
197
Hali inayoendelea ndani ya Chadema imezua taharuki kubwa kwa Watanzania wengi. Hiyo ni kutokana na matumaini makubwa ya chama hicho waliyoyaweka kwa wananchi.

Wengine wanasema sasa yametimia. Kwamba kama ilivyokuwa kwa NCCR Mageuzi mwishoni mwa miaka ya 1990 ndiyo yanakipata Chadema.

Kwangu mimi naona haya ni majaribu tu ambayo yanaweza kuiimarisha zaidi Chadema kama watatambua walipoanguka na kujirekebisha.

Migogoro katika jamii ni jambo la kawaida, kitu cha msingi ni kwa wanaogombana kurudi mezani na kuzungumza yaishe.

Katika suala hili la Chadema ambalo Zitto Kabwe, Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba wamevuliwa nyadhifa zao na Kamati kuu ya chama hicho cha upinzania, kila upande bado una nafasi ya kutafakari upya na kutafuta suluhu kwa lengo la kukijenga chama.

Vilevile kwa upande mwingine, Zitto na kambi yake watumie nafasi hii kutoa kauli zenye kusuluhisha siyo kujikweza.


Hata kama Zitto ana haki ya kugombea uenyekiti au cheo chochote, yeye au wanaomuunga mkono hawakupaswa wala hawapaswi kutoa kejeli kwa uongozi uliopo.


Kauli hizi za kukejeli elimu ya Mwenyekiti wao au ile kauli ya ‘akili ndogo kuongoza akili kubwa’ ambayo siyo tu imetolewa kwenye waraka huo bali pia imetumika mara nyingi kwenye mitandao ya kijamii hazipaswi kuendelezwa kwani zinaudhi na zinaukuza mgogoro.

Zitto na Dk Kitila wajue kwamba, uongozi uliopo madarakani uko kikatiba. Hata kama wamewazidi elimu au vipaji vya aina yoyote ile, bado wawaheshimu tu.


Wasubiri muda wa kugombea hivyo vyeo wanavyotaka watamwaga sera zao, lakini siyo kutukana na kukejeli.

Kimsingi ukisikiliza hoja za pande mbili utaona hiki chama kina udhaifu mwingi. Tatizo ni kwamba udhaifu huu unazungumzwa hadharani, badala ya wanaotofautiana kukubaliana na kukosoana.

Hii ni changamoto kubwa katika mfumo wa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Vyama mbalimbali vimeshindwa kuendelea kwa sababu ya ubinafsi, majungu na kutokuwajibika. Ni wakati sasa wa pande mbili hizo kukaa mezani na kusuluhisha tofauti zao, hapo Chadema itaepuka kikombe hiki cha vurugu.
 
Back
Top Bottom