Siku zote nitamuunga mkono Lissu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,282
2,000
Tofauti na kina Lowassa,Zitto na wengineo ambao wakati mwingine hujaribu kujitokeza hadharani na kutoa pongezi kwa watawala ingawa sikumbuki ni lini wao waliwahi kupongezwa na watawala hawa pale wanapofanya mazuri labda Zitto ingawa nae ilikuwa ni kipindi kile cha kuzindua Bunge baada ya yeye kuamua kumsikiliza Mkulu na kutotoka nje kama wenzake.

Sasa niambieni kwa haya yanayoendelea Dar-es-salaam ya kumuweka ndani Meya wa Ubungo na pia kutaka kuwakamata kina Sumaye,mtu unapata wapi moyo wa kuunga mkono hii serikali?

Kila siku ni kukamatwa na kuwekwa ndani alafu wakati huo huo wanataka tuungane kwa mambo ya kitaifa.Hii itawezekana vipi katika mazingira ya aina hii?!


Ni wazi tunahitaji wapinzani aina ya Lissu ambao siku zote husema ukweli na kuepuka kuwapaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom