Siku zote gharama ya mabadiliko ni kubwa na hayaji kirahisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku zote gharama ya mabadiliko ni kubwa na hayaji kirahisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PAMBANA, Sep 6, 2012.

 1. P

  PAMBANA Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wana JF salaam wote,

  Ndugu zangu naomba nianze kwa kusema kwamba kuung'oa mbuyu wenye umri wa miaka 50 si kazi ndogo ni kazi kubwa sana.Mbuyu wa umri huu ambo mizizi yake imeshajika katika sehemu kubwa ya ardhi inahitaji ujasiri na kufanya kazi ya kuakata mizizi bila kuchoka ili kuudhoofisha iliuweze kung'oka kwa urahisi.Pamoja kazi yote hiyo mwisho mbuyu huu hung'oka.

  Ndugu zangu naufananisha na mbuyu na CCM ambao wameshika dola ya nchi hii kwa takiribani miaka 50.Ni dhahiri kuwa mizizi yao ilishajikita sana na mzizi uliokuwa umefanikiwa kukua ni wao kutumia ujinga wa wanatanzania ili waendelee kututawala na kutunyonya lakini wanzania wameendelea kufunguka akili zao na kufahamu mambo yanavyoenenda katika nchi yao.Nami nitakuwa mnyimi wa fadhila nisipotambua mchango wamefanya kazi kubwa ya kututoa watanzania kwenye giza tulilokuwa nalo na hawa si wengine bali ni viongozi wa CHADEMA ambao wamekuwa wakifanya kazi zao za siasa kwa ushirikiano mkubwa sana.Na historia ya nchi itawakumbuka kwa kuchochea moto na ari ya mabadiliko kwa watanzania na mtu yeyote akayepinga hili basi huyo tumwache tu ana matatizo yake.Hii na uwezo wao mkubwa wa kusimamia na kuendesha movement wanazozianzisha.Mtakubaliana na mimi CHADEMA walianzisha operation sangara kipindi 2006-2010 na wote wote matunda yaliyotokana operation hiyo ambayo ni wabubge 23 wa majimbo na wabunge 25 wa viti maalum na haikuwa kazi rahisi kupatikana kwa wabunge hawa majimbo maana walipita kwenye miiba mimgi kipindi cha uchaguzi mpaka kufika hapo walipo.

  Mabadiliko yoyote ambayotumeshudia hapa duniani gharama yake ilikuwa kubwa hata kugharimu uhai wa watu.kwa mfano angalio upepo au vuguvugu la mabadiliko lililopita katika nchi za kiarabu kama vile Tunisia,Misri na Libya miaka ya hivi karibuni haikuwa rahisi maana iligharimu maisha ya baadhi yao.Na katika harakati hizo damu ilimwagika na kwa kuwa walishawasha moto wa mabadiliko hawakurudi nyuma mpaka kilipoeleweka.Watu wengi waluawa na damu ilimwagika.Na katika nchi hizo viongozi walitumia vyombo vya dola kama polisi na jeshi kupambana na wanabadilko lakini mwisho walishindwa.Hivyona mimi naungana na mwandishi mmoja wa gazeti la Mwananchi la jana tarehe 05/09/2012 aliyeandika makala yenye kichwa "Upepo wa mabadiliko ya Kisiasa hauzimwi kwa risasi na mabomu."

  Pia safari ya YESU KRISTO kuwa kutukomboa wanadamu haikuwa rahisi ilimgharimu uhai wake na damu yake kumwagika ili mwanadamu akombolewe.Na si hivyo tu hata katika safari ya wana wa Israel kutoka Misri kwenda Kanaani haikuwa rahisi maana wengi waliokuwa wabishi njiani Mungu aliwamaliza na pia walikutana na maadui wengi sana ambao ilibidi wapambane nao na wawashinde na kisha kusonga mbele.Hivyo siku zote gharama ya mabadiliko kubwa hasa waliopo madarakani wanapong'ang'ania nafasi waliyonayo.

  Nimalizie kwa kusema pamoja na CCM kutumia jeshi la polisi kuua wananchi kwenye mikutano ya CHADEMA na kuanza propaganda zao kuwa CDM ndio wanahusika, maana nia yao kuwatia hofu ili waogope kuhudhuria mikutano ya CDM lakini kamwe hataweza kuuzima moto wa mabadiliko uliowashwa ndani ya mioyo yetu watanzania na katu hatutarudi nyuma na hatuna hofu bali tunazidi kusonga mbele.

  "KADRI POLISI NA CCM WANAVYOZIDI KUUA WANANCHI NDIVYO WANAVYOZIDI KUCHOCHEA MOTO WA MABADILIKO KATIKA YA MIOYO YA WATANZANIA"
   
 2. a

  artorius JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wewe by 100%
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mbona polisi walivyowaua wapemba 34 kwenye maandamamo mlikuwa upande wa polisi.
   
Loading...