Uchaguzi 2020 Siku zilizobaki kampeni ielekezwe kujibu hoja za Lissu na nini kitafanyika kuboresha maisha

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,457
1,440
Nimesikilza hoja nyingi za Mgombea wa Chadema kwenye kampeni zinashawishi kuwa Serikali iliyoko madarakani imeshindwa kujibu changamoto za watanzania kwa kuwapatia uhuru, haki na maendeleo yao kama binadamu. Hoja hizo zimejikita kwenye mambo yafuatayo:

1. kutokuwepo na uhuru wa kujieleza,uhuru wa kuhoji uwajibikaji wa serikali, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa bunge na mahakama kama mihimili na uzingatiaji wa haki za binadamu, uzingatiaji wa katiba na sheria zilizopo.je kuna ukweli kwenye hoja hizo? Au kinachotakiwa ni uhuru wa kiuchumi kwa njia ya kujitegemea au wa kuamua mambo yetu wenyewe? Au uhuru usio na mipaka?Ni eneo linalohitaji kuwa- challenge wapinzani. Nitalifafanua mbeleni

2. Haki na mifumo mbalimbali inazoendena na malipo ya mishahara, mafao,kutopata fidia za waliobomolewa majengo,vitambulisho vya ujasiriamali, sheria zinazominya haki za mlipa kodi,kubambikwa kodi, kunyimwa dhamana, haki ya kuishi na utesi na mauaji yanayohusishwa na wasiojulikana, nk

3. kukosekana kwa Maendeleo ya watu kutokana na mkazo wa vitu,mzunguko mdogo wa fedha, maisha magumu ya wananchi, kutokuwepo na ajira,huduma za elimu na afya zisizoridhisha , kupunguza zaidi riba ya mikopo ya wanafunzi na suala la mishahara, ubadhirifu na ufisadi kwenye miradi( ametoa mifano ya ukiukwaji wa sheria za ununuzi na maamuzi yasiyo sahihi)kuwa yanachangia uwepo wa maisha magumu yasiyotabirika.

Hoja ya Lissu ni kwamba akipata madaraka yote haya atayaondoa. Kwa msingi huo ni vyema hoja hizi zikajibiwa na chama changu ambacho kina wakongwe wa siasa. Hoja hizi zisiachwe hadi mwisho kwa vile zitaathiri idadi ya kura. Hoja hizi zote zinajibika na kwa vile nyingi hazina uthibitisho wa kivielelezo. Zinaweza kujibiwa kama ifuatavyo:

1. hoja ya uhuru imetengenezwa na upinzani kwa tafsri yao, lakini kimsingi ni vigumu kuzungumzia uhuru wa maeneo mbalimbali bila kurejea katiba na iwapo yapo mapungufu iwekwe wazi kuwa yatapitiwa na kurekebishwa na bila kuathiri utulivu na uhuru mwingineo.Hii itakuwa imemnyanganya hoja mgombea huyo iwapo tafsri sahihi itatolewa kwa uhuru tulionao watanzania kwa sasana ambao ambao unatokana na katiba ingawa una mipaka yake ili kuondoa upotoshaji

2. vivyo hivyo kuhusu haki mbalimbali kuna umuhimu wa kukanusha yale ambayo si ya kweli na kuahidi kurekebisha yale yaliyo ya ukweli kwa kutoa maelezo na ufafanuzi wa kina yatayaondolewa au kurekebishwa awamu ijayo

3. Kuhusu maendeleo ya watu ni wazi dhima ya Ilani ya CCM nayo inazungumzia maendeleo ya watu lakini yanayotokana na vitu. Hili ni kuliwekea msisitizo tu kuwa pamoja na miradi awamu ijayo itazingatia zaidi (micro economics) yaani maisha bora kwa mtu binafsi(in a short run) kuongeza wigo na fursa za biashara hususani kwa watanzania, ajira, kupandisha mishahara kwa mujibu wa PATO LA TAIFA na punguzo zaidi la PAYE,kuongeza mzunguko wa fedha, kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kupitia upya sheria za kodi na kazi ziwe rafiki zaidi ili kutengeneza wajasiriamali wengi(kwa maana ya entrepreneurial economy)na ikibidi mabilionea wakubwa,usalama wa ajira watumishi wa umma kwa wanaofanya vizuri kazi, usalama wa raia na mali zao na kuunda Tume ya kuchunguza namna nzuri ya kuzuia mauaji,utekaji na maeneo kadhaa ya kikatiba ili kuondoa changamoto zilizopo kwa maslahi ya wananchi. Hoja hizi zikijengwa vizuri kutoa ufafanuzi na kueleza mwelekeo mpya kulingana na mazingira ya sasa kisiasa itaua hoja na tuhuma zinazojengwa na upinzani badala ya kuziacha zinaelea ni hatari kwa ushindi wetu.Ni muhimu zipate majibu mapema kwa ufasaha na takwimu au vielelezo thabiti. Hiki ni kipindi cha kunyanganyana AGENDA.Mbinu hii ilisaidia sana CCM uchaguzi uliopita 2015. CCM OYEE
 
Back
Top Bottom