Siku Za Utawala Wa SMZ Na CCM Yake Zanzibar Zinahesabika... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku Za Utawala Wa SMZ Na CCM Yake Zanzibar Zinahesabika...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Oct 30, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na Jabir Idrissa
  NAFURAHI kuona Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma ameramba matapishi yake mwenyewe. Amegeuka.
  Hamza ameivua Marekani na tuhuma alizoitupia pale aliposema hadharani kuwa nchi hiyo imehusika katika matukio ya milipuko ya mabomu iliyokuwa yameshamiri kisiwani Pemba.
  Japo amefanya hivyo kwa kuzidisha udanganyifu – akidai kwamba yeye hajawahi kusema wamehusika – bado ukweli unabaki palepale kwamba “amejirudi kwenye uhalisia wa mambo.”
  Hamza alitamka hadharani na kukaririwa na vyombo vya habari ikiwemo Televisheni ya Serikali ya Mapinduzi, TVZ, akiituhumu serikali ya Marekani kufahamu kinachoendelea Pemba wakati wa uandikishaji wapiga kura, baada ya nchi hiyo kutoa taarifa kwa raia zake wasifike Pemba kwa kuwa yanayotokea yanaashiria ukosefu wa amani.
  Taarifa ya ilani ya Marekani iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje (State Department) mjini Washington na nakala ya taarifa hiyo kupatikana mjini Zanzibar, ilisema wazi kuwa ilitokana na utafiti walioufanya.
  Lakini hata pale msemaji wa wizara hiyo alipotoa taarifa ya pili akirejelea matamshi ya ovyo ya Hamza, alisisitiza kuwa Marekani imechukua hatua hiyo kwa maslahi ya raia zake wala haikuhitaji kumuuliza kiongozi yeyote wa Tanzania.
  Bila ya shaka matamshi ya ovyo ya Hamza yaliikasirisha Marekani, na hatua hii mpya ya waziri huyo kujirudi ndani ya Baraza la Wawakilishi inaonekana haikuwa hivihivi, bali ni kwa kuzingatia maafikiano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Tanzania.
  Tatizo la Hamza kuwa hataki kuwa muungwana katika kujirudi. Anajizonga kwa kuanzisha uhasama na vyombo vya habari; eti vilimsingizia. Hivi Hamza asingiziwe ili iwe nini? Anajulikana mkate wake umeongezeka siagi miaka hii kutoka ule wa kutegemea ushoni aliokuwa akitegemea Mikunguni.
  Ninaisema kwa makusudi hii ili akae vizuri na mtindo anaouanzisha wa kurudisha lawama kwa wasiohusika kwa kosa alilojitia mwenyewe, tena kwa hiari yake na raha zake.
  Lakini hii haikuwa mada yangu, ila nimelazimika kugusia hapo kwa kuwa nilipata kumsihi Hamza kuwa “hayawezi madhambi ya SMZ.”
  Leo nikitaka hasa kueleza hofu yangu kwamba kwa kuwa mwenendo wa dola haujabadilika; kwamba haijafuata ukweli kuwa inanyonga haki za wananchi; basi sitarajii mabadiliko yoyote uandikishaji wapiga kura utakapoingia Mkoa wa Mjini Magharibi.
  Ni dhahiri kwamba misimamo ya viongozi wa vyama vya upinzani itabaki ileile ya kukataa kushiriki katika mduara wa ushetani wa kuhalalisha maovu yanayotendeka dhidi ya mfumo wa demokrasia.
  Ninamaanisha kuwa hawatahamasisha wananchi wanaowatii kujitokeza kwenye vituo vya uandikishaji ili kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) la Zanzibar.
  Na siyo tu kwamba hawatawahamasisha watu kujitokeza vituoni, bali pia watawaelekeza kujipanga vizuri ili kuzuia wale waliopatiwa kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi wasiandikishwe.
  Naiona hali hiyo kwa sababu bado tatizo liliopo – ambalo limekwamisha uandikishaji wenye ufanisi kiasi cha kusikitisha wakuu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kama inavyodhihirika katika taarifa zake kwa umma – halijatatuliwa.
  Tatizo ni kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, ambacho kuanzia mwaka 2006, kimeingizwa katika sheria ya uchaguzi kama shurti kwa kila Mzanzibari kukimiliki ndipo atambuliwe na kuandikishwa kama mpiga kura, kingali kinatolewa kibaguzi kwa kuzingatia nani kura yake ataitia kwa mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
  Kwa yule ambaye machoni mwa wenye kulea mfumo wa kidhalimu, ataonekana si miongoni mwa wakereketwa au makada wa CCM, itabaki tu kuwa shida kwake kuruhusiwa kupata kitambulisho na hivyo kujikuta hapenyi kwenye wigo wa watu wema.
  Kwa mfumo wa utawala uliopo hadi sasa, watu wema ni wale tu ambao hata kama si hadharani, lakini wana sura ya kupigia kura mgombea wa CCM tu na si vinginevyo.
  Asiyekuwa na chapa ya CCM kwenye paji lake la uso, ajue kura ya 2010 ataisikia tu. Ataisikia kwa sababu kwa kuwa hana kitambulisho, hatapata kuandikishwa. Asipopata kuandikishwa, hatapata kupiga kura.
  Kitambulisho cha Mzanzibari kimekuwa dili. Baada ya kuanza kama maskhara, ingawa kilipingwa kwa nguvu nyingi kwa kuhofiwa kitatumika vibaya, tulipo kishathibitika kuwa kililetwa kwa dhamira mbaya hasa. Ukweli unaonekana.
  Kimeshasababisha maelfu ya watu kunyimwa haki yao ya msingi ya kuingia katika daftari la wapiga kura. Hawa wamekalia kuti kavu kwani nafasi kwao kuingia ni sawa na mbuni kupita kwenye tundu la sindano. Labda ipite kudra ya Mwenyezi Mungu kabla ya Oktoba mwakani.
  Ikija kudra hiyo basi ndipo ukweli utapodhihiri na uongo utapojitenga. Hapo ndipo mbivu itapoliwa na mbichi itaposubiriwa iwive ili nayo iliwe kwa wakati muafaka. Ni wakati huu nyuso za wakubwa zitakaposinyaa kwa aibu.
  Watatahayari maana yale waliyoyapanga kutokea ili kujinufaisha nafsi zao, yatakuwa yametenguka. Ushetani waliolenga kuufanikisha utakuwa umekomeshwa. Wamenyamazishwa. Na hii si wao tu, bali hata mawakala wao wanaojitahidi kutetea wanachokifanya.
  Uandikishaji utakapoingia majimbo ya wajanja na “wasemaji ovyo isivyomithilika” watunza takwimu za kupika wanaoishi kwa kujisuta, wataumbuka na kubaki kushangaa. Labda watatamani ardhi ipasuke wajifiche. Labda wataamua kuhama nchi. Sijui.
  Tushaona uandikishaji ulivyoleta aibu kwa wakubwa katika majimbo ya Kaskazini Unguja. Tushajionea namna mikakati ya kuvuruga uchaguzi inavyoandaliwa. Tushafahamu kumbe bado wakubwa hawajaamini kuwa siku hazigandi.
  Ukweli ni kwamba umma umeelewa dhamira hasa za viongozi wa CCM katika kuitisha uchaguzi. Kumbe ni kiinimacho na jambo la kudanganya ulimwengu. Masikini roho zao hawajui kwamba uchaguzi huru na wa haki si matamshi bali matendo.
  Masikini roho zao hawajui kuwa hawana wafichacho. Kila kitu kipo kweupeni zama hizi. Hawajui kuwa ndani ya ofisi za umma wanazotumia kufanikisha udanganyifu wamo watu wema kwa Wazanzibari wenzao na nchi yao waipendayo kama mboni za macho yao.
  Masikini roho zao viongozi hawa wahafidhina hawajui kwamba kwa sasa wanapuruziwa tu kamba kwani iko siku kila kitu kitabadilika na mambo yatageuka nyuma mbele, na wao watasaga mawe kama alivyofanya firauni na wenzake.
  Hata kama si kesho na keshokutwa, hakuna chenye mwanzo kikakosa mwisho. Nasema hakuna kinachodumu milele iwapo binadamu mwenyewe ataukata na kurudi alikotoka. Basi mambo yatabadilika tu Inshaallah

  SOURCE:MWANAHALISI
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...mwezi wa tano 2010 waja!!!!
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Wamebakiza siku kidoooogo tu...karibuni tu Wazanzibar watatoka katika utawala wa kidhalimu wa CCM...Itabaki historia tu, karibuni waungwana...bendera ya utu wenu karibu itapepea...chem chem za muruwa wenu zimeanza kutiririka...hofu zenu zimeanza kupata tiba na utulivu wa nafsi unachukuwa nafasi...waungwana wamekupokeeni, karibuni Zanzibar...karibuni nchi yenu mliyoijenga kwa kucha na meno, mkatolewa kwa dhulma na shinde...rejeeni mkiwa mashujaa na watoto walee wanakusubirini kukupokeeni...karibuni sana tu.
   
 4. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Lisemwalo lipo na kama halipo laja .
   
 5. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,723
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  mnamkumbuka mama mouldin kastiko?

  alisema na hakupata kupingwa na viongozi wa SMZ, "sisi tumepindua hatuwezi kutoa nchi kwa vikaratasi".

  shida ya zanzibar ni ubaguzi wa rangi, hii ccm na cuf ni uchochoro tu wakupitia. ccm enzi hizo ni asp wanahisi walibaguliwa na ushirika wa znp na zppp wakiongozwa na serikali ya shamte, wakapindua...cuf zanzibar si bara...wanahisi walipinduliwa na kuondolewa madarakani sivyo halali....kilichofuatia mapinduzi...mauaji na unyanyasaji uliofanywa na asp kimeacha makovu mpaka leo...kitu kimoja tu kinaweza kuinusuru zanzibar...south african model...ukweli na maridhiano...watu wakae waangalie historia yao nani alifanya nini na kwanini ijulikane...na kisha wasameheane au adhabu zitolewe..na kisha wakubaliane a way forward...lakini kwa kura katu...
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Iam dying to see such beautiful changes in my age!
  Mungu ibariki Zanzibar!...Tunangoja hiyo HESHIMA ya juu kwa hamu!
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  you will die without it!:D
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  WW unaongea uwongo hapa...kwanza aliyesema maneno hayo si Moudline Castico bali ni Asha Bakari Makame ambaye sasa ni Mwenyikiti wa UWT(kama sijakosea), pili ni unafiki na upotofu kudai kuwa eti CUF ndio waliopinduliwa 1964...CUF haijawahi kushika madaraka...ila wamewahi kushinda uchaguzi mwaka 1995 n.k hawakupewa nchi...mawazo potofu kama yako ya kuhusisha mfumo wa vyama vingi wa sasa na historia za Mapinduzi,ujio wa CUF na uhuisano na ZNP&ZPPP na matatizo ya kisiasa ya sasa na historia hiyo ni unafiki ambao mtu wa mwanzo kuu-document...uzandiki huo ni Omar Ramadhani Mapuri...na ndiye mtu wa mwanzo aliyeleta siasa za kibaguzi za Uunguja na Upemba ambazo hazikuwa maarufu hata vipi katika kabla ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1991. Mapuri aliueneza na kuusambaza uongo wake kupitia kitabu chake cha historia ya Mapinduzi kiitacho "1964 Revolution and Its Achievements" humo mna mawazo kama hayo uliyoyaandika hapo juu na unafiki wa kugeuza akili za watu kuamini kuwa CUF wamekuja kulipa kisasi cha yaliyotokezea 1964, wakati hilo siyo lengo la kurejeshwa mfumo wa vyama vingi kwa mujibu wa katiba na CUF ni chama kiichosajiliwa kwa mujibu wa sheria za kuanzishwa mfumo huo kama vyama vyengine vyote, sasa nashangaa habari za "uhizbu" na "u-afroshirazi" zinakujaje tena!
  Mimi nilifikiri kadiri wazanzibar wanavyoelewa madhumuni ya mfumo wa vyama vingi kwa kadiri siku zinavyokwenda wameelewa sasa kuwa kumbe habari zile za Omar Mapuri zilikuwa ni uongo uliokusudia kujenga chuki na uhasama kati ya watu wa Unguja na Pemba ambao wameishi miaka yote hiyo hata baada ya Mapinduzi kwa udugu wa kufa na kuzikana.
  Wewe tunakujuwa bana umenyweshwa maji ya rangi ya kijani..kwa hiyo bado una waza "chanikiwichi" ie photosynthes
   
 9. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hata mimi nna matumaini sitofariki Zanzibar itakuwa ishajitoa katika makucha ya Tanganyika....kama itatokezea struggle hii kutofanikiwa hadi nikifariki basi wanangu wataendeleza vita hii dhidi ya Tanganyika.

  Tena bado wazanzibari hatujaanza na sera za Jihaad...tunavuta subra kidogo, lakini kujiripua mabomu hapo Manzese na Ilala ni halali kabisa!
   
 10. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Du!!!Waota ndoto za Nchana wewe.
   
 11. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Dodoma ndo mahala kwenu na huko ndo mustakabari wa Tz na Zanzibar unakopatikana,subirini muda tu CC ya CCM iwasaidie kupata rais
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Haya ww piga usingizi tu...kimbunga chaja
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mh! Haya bwana.
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wacha kujidanganya!
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hivi wa zenji hamuwezi kujiamria mambo yanu mpaka mje Dodoma ndo mpangiwe flani awe rais?
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tuna Kisiwandui
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  mbongo gani utamvalisha bomu??????? labda uanzishe chuo uanze kuwapiga sound hao wenzako kwanza
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  wacha kujipa moyo...ukirudi huku...Kisonge tushaigeuza dispensary,na jengo la Kisiwandui tunaligeuza shule ya sekondari.
  shule ya sekondari baadae
   
 19. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba unieleimishe yakhe. Hiyo CC ya CCM ni ipi na mchanganuo wa wajumbe wake uko vipi. Wewe unafahamu kuwa wamo wa kwetu humo katika CC. Na wakisema hawataki basi CC yako haiwezi kuamua dhidhi ya wasichokitaka? Historia ya za zama Nyerere ziweke kando ndugu yangu. CC yako haina ubavu kwa msimamo wa Zanzibar.. Hivi hujaelewa tu . Tafakari ya Dodoma na kadhia ya Muwafaka.
   
 20. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mueleze huyo. Na kwa kweli Kisiwandui ndiyo wanaoamua wakati mwengine hata Rais wa Jamhuri ya Muungano awe nani. Ama kweli Duniani kuna mambo!!!! na Dunia rangi rangile.
   
Loading...