Siku 💯 za uongozi wa Rais Mwinyi Zanzibar ni nyota njema kwa Wazanzibar

Oct 1, 2019
87
150
Salaam JF,

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi leo ametimiza siku 💯 tangu alipochaguliwa na Wazanzibar kuwa Rais wao, ukweli upo wazi kuwa Rais Mwinyi ameweza kufanya Mambo ya msingi na yenye tija kwa Wazanzibar na taifa lao kwa ujumla ndani ya kipindi hiki kifupi.

Rais Mwinyi ameweza kusimamia na kurejesha weledi na nidhamu katika uwajibikaji ndani ya mifumo ya utumishi wa umma, Aidha Mwinyi amekuwa na uongozi wenye falsafa zinazonuia kusimamia mifumo ya haki na usawa kwa Mantiki ya kuondoa urasimu ndani ya vyombo vya Kiserikali.

Kwa kipindi kifupi Rais Mwinyi amerejesha uhusiano kuntu baina ya Wazanzibar na serikali yao, Zanzibar ya Sasa amani imetawala na undugu umerejea tofauti na ilivyokuwa mwanzoni maana chuki na uhasama vilitawala miongoni mwa Wazanzibar, Pia Rais Mwinyi amekuwa ni Kiongozi mwenye kushaurika na kutimiza yale yote yanayoazimiwa na serikali ya umoja wa kitaifa.

Rais Mwinyi ameonyesha njia na nia ya dhati ya kutengeneza ajira mpya kupitia uchumi wa bahali, sekta Binafsi na eneo la utalii, hata hivyo Mwinyi ameonyesha kutambua nafasi ya wawekezaji ndani ya Zanzibar na kuziagiza mamlaka husika kutokwamisha vibali vya wale wanaotaka kuwekeza nchini humo, hii ni hatua njema na mwanzo mzuri katika ustawi wa uchumi wa Zanzibar.

Aidha Rais Mwinyi ndani ya siku 💯 katika utawala wake ameonyesha nia njema kwa wafanyabiashara kwa kuzielekeza mamlaka husika za kikodi kuepuka tozo kubwa za kodi kwa wafanyabiashara, hii ni hatua muhimu na rafiki kati ya wafanyabiashara na serikali.

Ndani ya utumishi wa siku 💯 za utumishi wa Rais Mwinyi ameonyesha nia chanya kadhaa katika masuala Kama afya, Elimu, uvuvi, ujasiriamali, uwajibikaji na uzalendo, Ni imani Rais Mwinyi ataweza kuifanya serikali yake ifikie malengo iliyojiwekea katika kuhakikisha Wazanzibar wananufaika na rasilimali zao na hivyo kuwa na uchumi Bora ngazi ya mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

Deogratias Mutungi
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,577
2,000
Such a humble, wise and an Intelligent Mr. President!
Kwanini asingekuwa Rais wa Tanganyika huyu Mwamba! Ni msikivu! Ni muungwana! Ana U-Presidencial Material ndani yake! Amekulia Ikulu!!

Kwa hili Wazanzibar wametupiga gap kubwa sana la kiuongozi sisi Wadanganyika. Ipo siku na sisi huenda tukaja kuwapata watu aina ya Dr. Shein na huyu Dr. Husein Mwinyi! Badala ya hawa watu wa 'kufoka foka'
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom