Siku za Patrick Rutabanzibwa Wizara ya Ardhi sasa zahesabika...........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Nimetoka kumwangalia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi kwenye ITV Mheshimiwa Patrick Rutabanzibwa akijitetea kutokana na tuhuma nyingi zinazomkabili wizarani hapo.........................................

Amejitetea ya kuwa wanaomtuhumu yeye ni wale ambao yeye mwenyewe amewaripoti kwa DCI kutokana na tuhuma za uporaji wa viwanja vya mashirika ya umma na kuviuza kwa watu hewa ambao nao huviuza kwa wawekezaji binafsi.......................au wafanyabiashara wakubwa wakubwa..............................


Nionavyo mimi, Rutabanzibwa amekuwa akitajwa kwenye tuhuma nyingi tangia alipokuwa Wizara ya Nishati hususani tuhuma za kujadiliana na IPTL kutokana na mkataba feki wa kuliuzia taifa umeme kwa bei mbaya...................majadiliano hayo yaliyofanyika London uingereza yaliliacha taifa bila ya nafuu ya kujitosheleza...........................

Alipokuwa Wizara ya Maji pia tuhuma za miradi isiyo endelevu kama ule wa kuhamisha maji ya ziwa victoria pia ulimwandama...........ni mradi ghali sana usiobebeka hata chembe na hauna matunda ya kuhudumia wanavijiji wengi walengwa...................

Sasa hizi tuhuma zinazomkabili za uuzaji wa viwanja vya mashirika ya umma kitapelitapeli haziwezi kumwacha hivi hivi tu.............................His game is up...................na mwana wa Kaisari hatuhumiwi..............
 
Hivi mnamjua Patrick au unasikiliza habari za kishabiki? Wengi hawampendi kwasababu yuko clean na hana tamaa ya kujilimbikizia mali.
 
Hivi mnamjua Patrick au unasikiliza habari za kishabiki? Wengi hawampendi kwasababu yuko clean na hana tamaa ya kujilimbikizia mali.

Huyu jamaa ukisikiliza pande zote mbili unachnganyikiwa. Lakini nashawishika kukubali media imekuwa upande wa -ve zaidi kw ahuyu jamaa.
Huyu jamaa nasikia kuna vitu vingi aliwai kugoma kusign na matokeo yake wakawa wanamuhamisha wizara ili dili ziende. Pamoja na mabaya yake huyu jamaa ana siri nzito sana. Ndio maana pamoja na tuhuma zote sishangai hawafanyi japo sanaa ya kumfikisha mahakamani kama kina Mgonja

Na hata hivyo wanavyomuhusisha vingine unaweza kukuta anahushiswa sababu ni alikuwa kiongozi sio sababu aliweka sahihi?

Lets wait and see comedy ya kipindi hiki nani watahusika.
 
Hivi mnamjua Patrick au unasikiliza habari za kishabiki? Wengi hawampendi kwasababu yuko clean na hana tamaa ya kujilimbikizia mali.

Ni rahisi kumtetea utakavyo lakini wahenga husema......................panapofuka moshi panaficha moto...................
 
rutabanzibwa ni makin sana_kinachomuangusha ni kwamba yeye ni sungura ktk kundi la vicheche
 
Rutashubanyuma ... what is your position now? Patrick amestaffu 3 years AFTER your post that his time is up. Mbona umekaa kimya???
 
Kwa taarifa yako, mara baada ya kuhamishwa wabaya wake waliendelea kusaini deal alizookataa kusaini, je wajua nini liliwapata? Kamuulize Mramba na Yona .... wanafahamu.
 
Back
Top Bottom