Siku za Nape kuvuliwa ngozi na Lowassa zinahesabika

bushman

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,411
743
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini toka mkakati wa kujivua gamba umeanza, ninachokiona watu wanaogopana, wakati mwenyekiti anafunga kikao mjini Dodoma aliwaambia wajumbe tumekubaliana wote na mnayajua tuliyokubaliana yepi?

Kuvuana magamba,baada ya hapo comedy ikaanza kwa Nape ambaye alikuwa anahamu kubwa ya kubwatuka akaanza,kutoa notice kwa mapacha watatu,Katibu siku chache akakanusha hakukuwa na maazimio ya siku 90.

Lakini mwenyekiti ameshakutana Lowasa na akachimbwa bit, akanywea.

My Note.

Je nape atakuwa salama Lowasa akimgeukia?

Je anajua mwenyekiti aliingizwa ikulu kwa rafu za Lowasa Zidi ya wagombea wengine wa CCM km Sumaye,Mwandosya,Salim na John Malechela?

Anajua katika vita hii Kikwete wala Mukama hawapo vitani naye?

Anajua kuwa Jk pia ni mmoja wa watuuhumiwa wa ufisadi?

Anakumbukwa alivyokoswakoswa kuvuliwa UVCCM na mtandao wa Lowasa?

Je nafasi aliyopewa amepewa ili alipe kisasi na Jk? Lkn Je ANAAMUUNGA MKONO KATIKA HILO?

Anajua kuwa JK HANA MSIMAMO WA KIMAAMUZI?
 
ashaumia mjinga yule. hajui anafanya kitu gani,ni bora tu angeendelea kututukana cdm. ila huko kwenye magamba atapaweza kabisa!!!!!!!!!!
 
Kichaa kapewa rungu, anapita kwenye majengo ya vioo. Kitakachofuata ni kufungwa kamba.
 
Huyu kijana anashindwa kabisa kusoma alama za nyakati. Kuna kipindi alikua na mvuto sana hasa baada ya kuibua ufisadi wa jengo la uvccm, Tulimwona mpiganaji wa kweli na chupuchupu aingie cdm kwa wapiganaji. Akavimba kichwa akataka kumchalenji Mnyika Ubungo, chama cha magamba kikamvua gamba. Akahongwa u DC, na baadae akapewa mtihani ambao angekua na uwezo wa kusoma alama za nyakati ndio kiama chake kisiasa. Sidhani kama anajua kwamba EL na bosi wake (jk) bado ni maswaiba. Kupambana na EL ni kupambana na jk, hana maisha marefu kisiasa maana mizizi ya EL ni mirefu sana. Wake up Nape....! Mwenyekiti alipokutuma hakuwa siriazi, muulize Magufuli. Uwe kama mbayuwayu. Za kupewa changanya na zako.
 
Huyu kijana anashindwa kabisa kusoma alama za nyakati. Kuna kipindi alikua na mvuto sana hasa baada ya kuibua ufisadi wa jengo la uvccm, Tulimwona mpiganaji wa kweli na chupuchupu aingie cdm kwa wapiganaji. Akavimba kichwa akataka kumchalenji Mnyika Ubungo, chama cha magamba kikamvua gamba. Akahongwa u DC, na baadae akapewa mtihani ambao angekua na uwezo wa kusoma alama za nyakati ndio kiama chake kisiasa. Sidhani kama anajua kwamba EL na bosi wake (jk) bado ni maswaiba. Kupambana na EL ni kupambana na jk, hana maisha marefu kisiasa maana mizizi ya EL ni mirefu sana. Wake up Nape....! Mwenyekiti alipokutuma hakuwa siriazi, muulize Magufuli. Uwe kama mbayuwayu. Za kupewa changanya na zako.

Mkuu dazu,

Underlined Bold, hata kiuhai
 
Utapia Mulo Sio kitu kizuri NAPE kapewa Mlo na Mapacha watatu akala akashiba alivyokosa pilipili(Yaani Ubunge Ubungo) kamtapikia mojawa wa maPacha (Yaani EDU) sasa naye Hatakubali kukalia uchafu ni lazima Ajioshe , NAPE sasa amekuwa Kidudu mtu anaangaika ksevu ugali lakini njia hazijui. CDM ni chuma cha pua kitameruhi asipoangalia
 
Mie namshauri kwanza apige magoti amrambe EL miguu vingnevyo naamini huyu bwana mdogo atapata shiida sana,alafu asiogope asimame awaambie watanzania kuwa alichokuwa anakisema haikuwa mkakati wa ccm kujivua gamba bali mkakati ulikuwa kuwahadaa watanzania ili waubusu mzoga (CCM) unaotoa harufu kali,hvyo afute kauri.

Hapa ccm ilipo haiendi bila fisadi EL,(the CCM Dony), sasa mtulie pamoja hukohuko mjibu kwanini mmelifikisha hapa taifa letu (our beautiful mother land) kabla hatujawafuta kwenye uso wa dunia
 
Lowassa mshughulikie Nape kisawasawa in case utapata upenyo.

Kwa kumuua kama walivyopanga kufanya kwa Mwakyembe. Hivi nyie ni mabaradhuli kweli kushabikia jambazi akiua raia aliyemuibia? Hicho mnachodai nyie kwamba bwana mkubwa hayuko na Nape muendelee kuota lakini kwa bahati mbaya sana hata Lowassa anajua kwamba ni suala la muda tu kabla hajaaibishwa halafu tuone yeye ni nani! Mbona asifanye kama Raila Odinga anavyofanya akiudhiwa - Kuunda chama chake. Kwanza anao wafuasi wa kuanzia ambao ni mkewe na watoto wake na hawa washabiki wake JF?
 
Huyu kijana anashindwa kabisa kusoma alama za nyakati. Sidhani kama anajua kwamba EL na bosi wake (jk) bado ni maswaiba. Kupambana na EL ni kupambana na jk, hana maisha marefu kisiasa maana mizizi ya EL ni mirefu sana. Wake up Nape....! Mwenyekiti alipokutuma hakuwa siriazi, muulize Magufuli. Uwe kama mbayuwayu. Za kupewa changanya na zako.[/QUOTE]

Umemaliza mkuu, umenena sawia kwani inaonekana hajatia akili kichwani. Awe Mbayuwayu la sivyo kijana tutampoteza sasa hivi. Fisadi hana urafiki wa kudumu bali yuko tayari kwa lolote bora maslahi yake yamelindwa!
 
Back
Top Bottom