Siku za muungano zinahesabika, Tanzania bara itaitwaje ukivunjika?

Kuna kazi kubwa hadi kieleweke Tanzania,matatizo teleeeeeeee udini,ukabila,wizi,ubabe,chuki za bure bure sijui tutafika lini kwanini tunakubali kugawanywa makundi watanzania?
 
Mungu wa dini ipi?tanzania haina dini wala uwepo wa mungu.

Kwani Mungu ni wa dini mkuu, Mungu si ni Mungu tuu dini iwepo au isiwepo Mungu anabaki kuwa Mungu?? Ila kizungumkuti ni pale utakapojikita kwenye dini inayomwamini mungu badala ya Mungu.
 
Nadhani serikali Tatu itafaa sana.
Ila ya Muungano gharama ni 50% each. Hatuangalii idadi wala nini!
Hakuna haja ya kukomoana!

Sidhani kama Zanzibar kutokana na udogo wake itakuwa tayari au hata kuweza kuchangia 50% ya gharama za serikali ya Muungano wakati huohuo ikiiendesha serikali yake yenyewe.

Tanganyika nayo kama itatoa mchango mkubwa basi fairly itadai kuwa ndiyo iwe na sauti kubwa kuliko
Zanzibar,Wazanzibar watajikuta kuwa hawana sauti ndani ya Muungano kitu ambacho wanataka kukimbia sasa hivi katika utaratibu wa serikali mbili.

Dawa ni kuuvunja tu.
 
  • Thanks
Reactions: HT
TANZANIA NI MUUNGANIKO WA NCHI MBIL = (Tanganyika na Zanzibar) sasa nje ya Tanzania ni Tanganyika na nyingine Zanzibar......TAFAKARI!
 
Naheshimu kauli ya baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere(RIP) kuwa atakaaeanza kuleta ubara na uzanzibar hiyo dhambi itamtafu (sory kama ntakuwa nimerefer tofauti kidogo)
 
Of course; kwanini tubadili jina? hata Zanzibar kuna Watanzania wengi zaidi kuliko Wazanzibari...

Mzee Mwanakijiji, unamaanisha nini?? Je inakuwaje Watz wengi ndani ya Zanzibar?? Katiba ya Zanzibar ya zamani( sio hii mmpya) ilisema Mtanzania yeyote akiishi Zanzibar zaidi ya miaka 6 mfululizo basi ana haki ya kuwa Mnzanzibar. Sasa labda hao Watz waliokaa huko muda mrefu wameshakua Wazenj.

Japo nami naunga hoja jina libakie TANZANIA, tumeshalizoea na tunalipenda
 
Back
Top Bottom