Siku za muungano zinahesabika, Tanzania bara itaitwaje ukivunjika?

Intellect

Member
Apr 1, 2011
34
20
Ni dhahiri kwamba siku za muungano kati ya Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar) siku zake zina hesabika kwa maana hata hao wanaoutetea ukiwaambia wakupe faida zake utasikia " huu muungano wetu tumerithishwa na waasisi wa taifa hili" mara "amani" mara "watu wameoana" ili mradi wao waendelee kula matunda na wananchi wanaambulia kero tu.

Ukitizama kwa undani faida za muungano ni chache na nyingi hazina tija. Karume Angekua hai angeufutilia mbali na kama hoja ni kuoana mbona watu wameoa ulaya na sisi hatuna muungano na nchi za ulaya! Wazanzibari wanafikiri wananchi wa bara wanafaidi, wa bara wanafikiri waunguja wanafaidi kumbe ni watu wachache tu wanaoshikilia uongozi serikalini ndio wanafaidi na ndio maana ukiwahoji wananchi wa zanzibar watasema hawautaki, baraza la wawakilishi haliutaki ila viongozi wenye nyadhifa katika derikali ya muungano kama wabunge na mawaziri kutoka zanzibar pamoja na wana CCM wenye fikra mgando wao ndio kama wana hati ya muungano!

Binafsi sina tatizo na uvunjika kwa muungano, uvunjike tu, tatizo lango ni baada ya kuvunjika, je tanzania bara italirudia jina la tanganyika au itaitwa vipi?
 
je tanzania bara italirudia jina la tanganyika au itaitwa vipi?[/QUOTE]

jina "TANGANYIKA" halisound gud, ila kwa upande wangu ningesuggest uanzishwe mchakato wa kurename upya hii tanzania bara kma ilivyofanyika miaka hiyo ya nyuma ktk kupatia jina huu muungano wa sasa ambapo jina tanzania lilipatikana.
 
Nishauri iitwe Kilimanjaro ama Serengeti. Pia hii thread ishakuwepo hapa mwaka jana watu wakachangia sana tu
 
je tanzania bara italirudia jina la tanganyika au itaitwa vipi?

jina "TANGANYIKA" halisound gud, ila kwa upande wangu ningesuggest uanzishwe mchakato wa kurename upya hii tanzania bara kma ilivyofanyika miaka hiyo ya nyuma ktk kupatia jina huu muungano wa sasa ambapo jina tanzania lilipatikana.

Mkuu naona una mpango wa kutengeneza chanzo cha mapato kwa watu fulani, hii itatengenezea watu mamilioni hapa. Mchakato huu unaweza ukapata go ahead haraka sana hapo wakati utakapofika. TANGANYIKA poa tu!
 
Ukiita kilimanjaro, wachagga watajiona nchi ni yao. Na ukiita serengeti, ni jina haiubu kwa sababu Dunia nzima wanajua serengeti ni jina pombe na mbuga za wanyama. Jina TANGANYIKA TUU ndilo bora kupita majina yote . Mngoni angependa jina la Lukumbulu au serous! mfipa naye atataka jina la katavi! mnyiha naye atatka jina la ndolezi! mruguru naye atatka jina la mikumi(miten)!
 
muungano ukivunjika kutokana na articles of union mali yote ya jamhuri ya muungano itagawia 50% by 50% kati jamhuri ya watu wa zanzibar na jamhuri ya watu wa Tanganyika
 
Nafikiria Tanzania bara ikiiitwa Kilimanjaro, Watanzania tutaitwaje kwa Kiingereza? Kilimanjorese au Kilimanjaronians? Hivi tuliitwaje tulipokuwa Tannganyika, Tanganyikans? Na Serengeti je? Serengetians. Labda tuiite nchi yetu Tanzanite; then tunakuwa Tanzanitians?
 
Ni dhahiri kwamba siku za muungano kati ya Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar) siku zake zina hesabika kwa maana hata hao wanaoutetea ukiwaambia wakupe faida zake utasikia " huu muungano wetu tumerithishwa na waasisi wa taifa hili" mara "amani" mara "watu wameoana" ili mradi wao waendelee kula matunda na wananchi wanaambulia kero tu.

Ukitizama kwa undani faida za muungano ni chache na nyingi hazina tija. Karume Angekua hai angeufutilia mbali na kama hoja ni kuoana mbona watu wameoa ulaya na sisi hatuna muungano na nchi za ulaya! Wazanzibari wanafikiri wananchi wa bara wanafaidi, wa bara wanafikiri waunguja wanafaidi kumbe ni watu wachache tu wanaoshikilia uongozi serikalini ndio wanafaidi na ndio maana ukiwahoji wananchi wa zanzibar watasema hawautaki, baraza la wawakilishi haliutaki ila viongozi wenye nyadhifa katika derikali ya muungano kama wabunge na mawaziri kutoka zanzibar pamoja na wana CCM wenye fikra mgando wao ndio kama wana hati ya muungano!

Binafsi sina tatizo na uvunjika kwa muungano, uvunjike tu, tatizo lango ni baada ya kuvunjika, je tanzania bara italirudia jina la tanganyika au itaitwa vipi?
Nje ya muungano hakuna Zanzibar muungano ukivunjika zitatoka nchi tatu Tanganyika, Unguja na Pemba.

Natamani muungano uvunjike hata leo.
 
Kwa upande wangu ningeshauri tuitwe Republic of Tanzania kwani hata sasa sioni nafasi ya Zanzibar katika hili jina.. Simply tuondoe neno muungano then tusonge mbele tuachane na walalamishi' Z.....bar' waendeleze siasa zao za chuki.. Badala ya kufikiria ni jinsi gani ya kuboresha sekta ya utalii iongeze pato la taifa.. wanaendelea kulalamika tunawanyonya..ni Watanganyika wangapi wanamiliki hotel kubwa Zenji..very few..
 
Mimi hata leo nataka tuvunje huo muungano,sijawahi kuona faida yake toka nizaliwe
 
Kwani hii nchi ilibadilika jina lake lini? Tanzania ni muungano wa nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibar,sasa kwa nini tuwaze jina la nchi wakati lilikuwepo toka zamani?
Halafu natamani sana huu muungano uvunjike hata leo ili kina MS waende zao wakauane salama huko Zenji.
Go to hell TANZANIA!
 
Back
Top Bottom